mumagoma
Senior Member
- Jan 15, 2014
- 186
- 95
MIPANGO ya Muda mrefu na MIPANGO ya Muda mfupi
Tunachokiona katika serikali hii ya awamu ya tano chini ya mh Rais John Magufuli ni Kuwa ilani inatekeleza mipango yake kwa kubalance ile ya muda mfupi kidogo na ya muda mrefu kwa sana...
Mipango ya muda mfupi huonesha Matokeo chanya muda mfupi, wananchi na wanasiasa wanapenda sana mipango hii kwani huwafanya wakubalike muda mfupi , lakini uhalisia watalamu wanasema mipango hii huwa inaziba tatizo na sio kutatua
Mipango ya muda mrefu ambayo ni njia muafaka ya kutatua shida na matatizo ktk jamii hufanyika na kutekelezwa kwa muda mrefu na ikisha timia huleta faida kubwa katika jamii
.... Ndege mbili zilizo nunuliwa ni mipango ya muda mrefu, faida ya hili ni ya muda mrefu Katika nchi yetu
... Bomba la mafuta linalotarajiwa kujengwa toka Tanga kwenda uganda ni mipango ya muda mrefu, itatoa ajira muda mrefu kwa watanzania
... Kuhakiki watumishi hewa ni kujenga msingi wa kutorudia kosa la kuwa na watumishi hewa, faida ya hili itakuwa serikali itakiwekea mfumo mzuri wa kuwabaini watumishi wake kiurahisi na itakuwa faida ya muda mrefu
... Reli inayotarajiwa kujengwa, Reli ya kati ya standard gauge itahudumia kusafirisha mizigo Tanzania na nchi zote za ukanda wa africa kati kutokea bandari ya Dar es salama, faida ya hili ikaonekana muda mrefu
... Kutoa vigezo stahiki vya kuwakopesha wanafunzi elimu ya juu lengo lake ni kuhakikisha wale wanaokopeshwa wanarejesha mkopo ndani ya muda baada ya kuhitimu, hili litafafanya board ya mikopo ijiendeshe muda mrefu bila kukwama, faida ya hili ni muda mrefu
Mh Rais amekuwa akitekeleza ilani ya chama kwa kuangalia mbali, faida ya hayo anayosimamia hatutaiona siku hio hiyo hiyo , faida yake tutaiona baadae, Ningependa na mimi niurudie ule usemi wa mh Rais kuwa "ingekuwa vyema Malaika wajitokeze wazime mitandao ya kijamii yote na ili baada ya miaka miwili au mitatu aje awashe tena ili wale wanaodanganywa na mitandao mbalimbali waone utofauti "
Ndani ya mwaka mmoja mengi na ya msingi yamefanyika na Serikali yetu tiifu kwa sisi wanyonge imekuwa ikitekeleza mipango chanya ya muda mfupi na muda mrefu, na huku ikitupilia mbali mipango hasi ya muda mfupi
MFANO wa MIPANGO hasi YA MUDA MFUPI
Mfano wa mipango hasi ya muda mfupi ambayo serikali hii sijaona ikiitumia na sijaona ikiweka kama kipaumbele ni...
... Kugawa fedha bure kwa wananchi wake hata wenye nguvu ya kufanya kazi, binafsi hili siliungi kwa kuwa hutatua shida ya siku moja na baada ya hapo shida huibuka tena na wananchi wanaendelea kutabika
...... Kuruhusu wanafunzi hata wasio na vigezo kusoma vyuo vikuu ili kupata wasomi wengi ndani ya muda mfupi, binafsi hili pia naungana na Serikali kulipinga maana ndio huwa baadae tunapata wasomi wasio na ubora
... Kuruhusu muda wote watu wafanye siasa ili kuwafurahisha wao badala ya kufanya kazi, ukiwaruhusu watu wafanye siasa muda wote utawafurahisha muda huo kwa kuwapa haki ya kukusanyika lakini furaha hiyo itaondoka mapema baada ya njaa kuingia badae maana watu hawakuzalisha, naungana pia na Serikali kupinga siasa za muda wote
... Kuwaruhusu wananchi wajenge mabondeni kwenye mafuriko ilihali unajua wakati wa mvua kutakuwepo na mafuriko, utawafurahisha muda mfupi lakini baadae watapata shida
... Kuruhusu watu wajenge kwenye road reserve ili kuwafurahisha muda huo mfupi ilihali unajua barabara baadae itatanuliwa ni mipango ya muda mfupi
Mipango hasi ya muda mfupi inatatua shida kwa muda mfupi lakini baadae shida inaibuka tena
My take....
tuiache serikali ifanye kazi iliyo tumwa na wananchi tuache kupotosha ukweli