Tumuangushe Godbless Lema 2015

Tumuangushe Godbless Lema 2015

Status
Not open for further replies.
Kawambie magamba waliokutuma hatudanganyikiiiiii; hapa Arusha kazi ni moja ku-delete CCM; kama hukioni alichokifanya GJL hapa Arusha basi ni nahati yako mbaya kwa sababu GJL is here to stay; hutaki kajinyonge!
UKAWA kama kawa; UKAWA kama Dawa; UKAWA ni tumaini letu.

From CLIFF JANN
Ndugu wananchi naomba kupata wasaa wa kutembea nakuitazama TANZANIA ya leo katika kile tunachoita uhuru wa mawazo katika kila jambo pasipo kutizama muktadha wa nchi, muda mwingine kuvuma kwa upepo hakubadili kutokea kwa jua, TANZANIA imejaaliwa UPENDO NA AMANI....

MWANZO walivotujia tuliona vyema kubadili na kuwepo na USAWA kuwapa nafasi za uongozi katika vitongoji na kata na majimboni kwetu ili KULETA USAWA NA UTETETEZI WA WANYONGENA MASKINI WANAOUMIA mkapate kupaza sauti zao UMEKUWA KINYUME tena uvunjifu wa AMANI na maandamano yasiyokuwa na tija kwa taifa letu teule.

LEO KALAMU YANGU KWAKO MH GODBLESS JONATHAN LEMA. mwaka 2005 nilikuaa kinda nilipenda siasa zako msemakweli huchukiwa, msema uongo kama wewe ambao haudumu hushangiliwa ashakumu si matusi kwa sauti yako ya kimamlaka na hoja tengefu ila bahati haikuwa yako SIASA NI UPEPO NA KULINGANA NA WAKATI.

PUNDE UKAKIMBILIA CHADEMA PANGO LA MABADILIKO, VYANZO VYA VURUGU.

kwa sera zenye mashiko tulikukabidhi jimbo LAKINI HATA KIMOJA ULICHOTIMIZA, tangu ulipotuahidi kwenye kampeni zako 2010 , zimebaki simulizi kama za ALFU ULELA ULELA.

UMEKUWA HUISHI KUANDIKA WARAKA tena ZILIZOJAA UBAGUZI NA UNAFIKI WA DHAHIR. Umejaaliwa kuandika nakufananisha na JOGOO AMBAE HUAMKA MAPEMA LAKINI HAFUNGUI MLANGO.

UONGOZ NI MASHIRIKIANO NA UONGOZI ULIOPO KULETA MAENDELEO NI SI MIFARAKNO KWANI ARUSHA NI JIJI LA UTALII
 
Nataka kujua huyo MwanaCCM atakayethubutu kujipima UBAVU na Lema 2015?
Baltirida Burian?
Abdulhaman Kinana?
Mbona sipati picha
 
Huu ni wosia kwa wananchi wote wapenda maendeleo wa jimbo la Arusha Mjini.

Jimbo limepoteza hadhi yake ya utalii.Tusifanye makosa tena tutajuta.

Ungekuwa kweli MZALENDO ungetuambia watanzania tusiwachague hawa wala rushwa unatupigia makele tu.Usitukwaze bwana IPTL hamjamaliza kama mnaubavu pigeni kura ya kutokuwa na imani ns Prof wa Kichina
 
Kuandika mada upo ila dhambi yako kuu nikuwa fisadi na kuwaunga mkono mafisadi. Kura yako 1 na ya mafisadi wenzako km 10 hazitomsumbua Mh. G J. Lema. Lema forever.
 
Kwa maoni yangu, Godbless Lema ni mmoja wa wabunge wachache sana katika Jamhuri ya Tanzania, ambao wameingia katika historia ya mwanasiasa aliyeweza kuikosoa vilivyo serikali iliyoko madarakani na mamlaka zake. Ni mmoja wa wabunge vijana wenye kuthubutu kupambana waziwazi na uonevu, wizi wa mali ya umma na kupigania haki. Ni mbunge jasiri kwelikweli, mhamasishaji asiyeogopa na ambaye alifanikiwa kuteka imani ya watu wake wa Arusha, lakini hata zaidi ya Arusha. Nakumbuka siku moja alipokuwa ameshinda kesi yake ya Ubunge Court of Appeal Dar es salaam, wakati anarudi Arusha, barabara toka KIA mpaka Arusha mjini zilijaa wananchi kama vile anapokelewa Baba mtakatifu, na wala sitii chumvi. Watu wanampenda sana uchapaji kazi wake, ushujaa, ukarimu na ucheshi. Inasadikiwa katika namna nyingine, aliiamsha serikali kuijengea Arusha barabara nzuri. Kimsingi, maendeleo makubwa ya Arusha kwa muda mfupi, hiwezi ukayatofautisha (disassociate) nay eye na chama chake kwa sababu yalifanyika kipindi chake akiwa mbunge no matter who spearheaded the efforts. Ana cha kuonyesha/ kukitangaza kama mwanasiasa. Lakini pia tofauti ya kura zake (56,561)na za mpinzani wake (Ambassador Batilda Burian 37,640) zilikuwa kubwa mno (18,921), licha ya kwamba Batilda alikuwa Waziri wetu na alisaidiwa sana na dola na Chama tawala. Huyu si mtu wa kubeza kwa standard yoyote ile, hasa kwa sababu CCM bado hawajajipambanua kama Chama cha wanyonge au hata wananchi!

Kosa kuu ambalo CCM na Serikali yake walilolifanya Arusha ni kumhamisha Mkurugenzi wa jiji, Mama Spora Liana nadhani mapema 2014 baada ya kukataa kumpatia mkuu wa mkoa Bwana Muhongo Tshs 100,000,000 kwa matumizi yake. Lakini huyu mama inasadikiwa alinyanyua mapato ya jiji toka Tsh 400,000,000 mpaka 927,000,000 mwishini mwa 2013. Baada ya kukataa ufisaji wa mkuu wa mkoa, hatimaye Waziri mkuu alimhamisha kw maelezo kwamba hashirikiani na wenziwe vizuri. Ikimbukwe kwamba mama huyu ndie aliyenunua mitambo ya kutengenezea mabarabara Arusha hii leo wanayojivunia. Ni bahati nzuri kwamba alikuwa replaced na equally competent Mkurugenzi Juma Iddi. Itoshe kusema, hili lilikuwa ni doa kisilo na ulazima la CCM. Mwisho wa siki. Lema kama mwanasiasa, atadai alikuwepo wakati mapato Arusha yakiongezeka kuliko kipindi cha Mbunge mwingine yoyote. Lakini pia CCM Arusha wamejijengea chuki kubwa kwa wananchi (ki asili wananchi wa Arusha huwa hawatishiki na kudanganyika kirahisi). Kwa haraka sijamwona mtu wa kumn’goa Lema Arusha toka Chama chochote. Lema hana kashfa pia ilyoko wazi. Ndilo ninalilijua.

Nguvu nyingine ni ku capitalize kwenye mgawanyiko wa wana CCM jimboni arusha, bila shaka ni moja ya silaha zake. Pia negative attitudes za watu wa Arusha dhidi ya Abdulrahman Kinana na ndugu zake zita play role. Zaidi pia wakazi wa wilaya za jirani, ndio hao hao wa Arusha, kwa hiyo hayo ndiyo niyaonayo. NANGOJA KUKOSOLEWA.
 
Huu ni wosia kwa wananchi wote wapenda maendeleo wa jimbo la Arusha Mjini.

Jimbo limepoteza hadhi yake ya utalii.Tusifanye makosa tena tutajuta.


Huwezi kusema huyu ni mfupi pasipo kutuonyesha alie mrefu. Ingekuwa vyema ukatupa taarifa za kina kabla ya Lema na wakati huu wa Lema. Mfano watalii waliokuwa wakitembelea ARUSHA ni 23,000 kabla ya Mh, Lema, leo ni watalii 13,000 tu kwa mwaka. Ulichofanya ni maongezi ya kwenye KAHAWA mwenye SAUTI ndie anaeshinda.
 
Mtaangaika sana Arusha ni Chadema tumeanza na Mungu tupo na Mungu na tutamaliza na Mungu
 
mnacheza na mziki wa Lema arusha,utamu wa ngoma ingia ucheze,kaulize kilichompata mkuu wa mkoa Magessa akuhadithie.kilichompata.unachezeeeeea Lema wewe.
 
Sisi wa hapa chuga ccm kamwe hamuwezi kutudanganya na propaganda zenu na wakati tunaona mnavyouwa tembo wetu kupeleka china kila siku na ufisadi kia kona ya nchi hii
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom