Tumsaidie mtu huyu, amechanganyikiwa

Tumsaidie mtu huyu, amechanganyikiwa

Namlaumu huyo jamaa........anataka simu ya mwenzie ya nini......huyo dada yeye kataka yake........?.......wanaume wengine bana........
 
Kuoa au kuolewa si shuruti bali ni hiari.

Aepuke zigo la kujitakia angali mapema.
 
Haya ndio changamoto zinazowakumba vijana wasiweka mambo wazi tangu mwanzo i.e siku za mwanzo kabisa.
Sijui vijana wenzangu wanatumia vigezo gani hata kuridhia kufunga ndoa. Matatizo mengine ni ya kujitakia, na hii inatokana na kuweka tamaa za mwili mbele.
Inasemwa, hakuna mtu anakaye msaidia mtu aliyefanya maamuzi mabovu wakati wa kutafuta mwezi. Mwenye macho aambiwi tazama.
 
Nashangaa sana mapenzi ya sikuhizi! Yaani unaweza kumwamini mtu kwakumvulia nguo lakini siyo kumwachia simu! Very strange indeed!
 
Salamu wana JF. Kuna mtu mmoja ameniomba ushauri lakini nimeona ni vema kushirikisha wanajukwaa ili tuweze kumpatia jibu lililo sahihi. Suala lenyewe lipo hivi: Nina jirani yangu ambaye tunaelewana sana, hivi karibuni aliniambia hamwelewi mchumba wake wa kike anayetarajia kufunga naye ndoa hivi karibuni maana (mwanamke) hapendi jamaa ashike simu yake. Kila siku wanamke anatumia muda mwingi sana kuongea na watu mbalimbali ambao jamaa hawatambui, simu hiyo ipo bize mchana kutwa na hata usiku. Siku moja mwanake alipokuwa anaoga simu yake iliita zaidi ya mara 3, jamaa akaamua kuipokea, simu ile ilipigwwa na mwanamme ambaye alitaka kuongea na mwenye simu (mwanamke), jamaa akamwambia mwenye simu ametoka kidogo, yule jamaa aliyepiga simu akakata simu. Mwanamke aliporudi ndani akaelezwa kuhusu simu iliyopigwa. Mwanamke alikasirika sana kwamba kwa nini jamaa (mchumba wake) ameipokea ile simu, ugomvi ilikuwa mkubwa. Tukio lingine lilitokea siku moja wachumba hao walipokuwa wapo faragha meseji iliingia kwenye simu ya mwanamke, jamaa akataka kumjua aliyetuma meseji lakini mwanamke akamzuia na pia akafuta hiyo meseji, pakatokea tafrani ya nguo kuchanika kwa wapenzi hao. Kutokana na visa hivyo jamaa anaomba ushauri je huyo mchumba wake ana mapenzi ya kweli kwake? Kwa nini hapendi simu yake ichunguzwe na huyo mchumba wake? Jamaa anaomba ushauri afanyeje?

Pole kwa jamaa yako asiekuwa na maamuzi'', pole wewe pia kwakuaminiwa na jamaa yako lakini asijue kwamba kumbe huna maamuzi na ushauri kwa mambo madogo kama hayo!

Hua siku zote naamini kwamba maamuzi yoyote ya mambo binafsi yapo kwa mhusika nwenyewe' na ukiona mtu anaomba ushauri kwa swala dogo kama hilo ujue anampenda huyo mhusika hivyo anataka kufarijiwa tu' na ukimwambia ukweli kwamba huyo sio mke mnaweza mkagombana au atakuchukia bila wewe kujua.

Sina uhakika kama ushauri wa wadau hapa unaweza kubadilisha maamuzi ya jamaa yako'' ila kiufupi huyo mwanamke hampendi jamaa, mbaya zaidi kashajua jamaa amedata kwake ndo maana anakua na jeuri nakiburi kama hivyo! Hivyo huyo ni malaya kama malaya wengine tu na hafai kuwa mke wa jamaa yako" ingawa anaweza kuwa mke mwema kwa mtu wa type yake na atakayempenda yeye....!

Kila lakheri mkuu.
 
nini kilitokea hadi huyo mchumba akaanza hiyo tabia?
 
ukiona manyoya..................huyo dada siyo muaminifu akae azungumze naye wafikie muafaka ajue mbivu na mbichi
 
"ndugu mimi nina miaka minne na mke wangu, anaweza akaniachia hata simu yake siku nzima na mimi nampa uhuru wa kushika simu yangu."


hii safi, nami naona itanifaa, toa maujuzi mkuu wakipiga huwa unasemaje mama nanii katoka, simu ipo chaji, kaenda sokoni? Kisha unamaliziaje mi ndo baba watoto wake?

Naomba maujuzi maana naona staili yako inaweza kudumisha ndoa, isipokuwa pale nitakapo pokea sms za jirani nisiyempenda. Usisahau nina presha, kama mbinu hii inaongeza presha niachane nayo.
 
ndugu mimi nina miaka minne na mke wangu, anaweza akaniachia hata simu yake siku nzima na mimi nampa uhuru wa kushika simu yangu. Mwambie jamaa yako huyoi msichana hamfai.

safi sana mkuu na ndo inavyotakiwa! Maana kupitia simu mambo ni mengi. Shetani anatumia sana simu kuharibu.Mungu awape furaha daima.
 
Ebu jamani wana JF please wekeni vitu vya msingi kwenye jukwaa sio huu upumbavu km huu wa huyu jamaa yetu na hawara yake! Yaani hata kunya nako ufundishwe wakati choo unakiona..?!!!
Please do not post nonsense topics.

vya msingi kama vipi mmu,mkuu?
 
Je na zile laini mbili za mitandao mingine ambazo huwa zipo kwenye kale kapochi kadogo nazo huwa anakupa, huwa anaziweka ndaani ya pochi anafunga na zipu

we jamani ndo nini kumrusha roho mwenzio
 
Kuna dalili za huyo mwanamke kutokua mwaminifu. Kwa kuwa ni dalili tu (si jambo lenye uthibisho), afanye uchunguzi wa hzo cm/ sms kwanza ndipo achukue uamuzi.
ANGALIZO:
 
Swali gani la kuumiza kichwa hilo??? Huyo mwanamke ni kwamba ana wanaume kama SACCOS!!! Sasa ni wa nini huyo!!! Kitendo cha wapenzi wawili kufichana simu ni hatari sana!!! Hata mke/mume hutakiwi kumficha. Ikifika kuwa mmoja wa wapenzi au mke au mume anaficha mawasiliano basi jua hapo kitumbua kimeingia mchanga na mafuta ya taa!!! Hakiliki hicho!!!
 
Jaman hyo dada sio mesminifu kwani anajua kabisa hyo cm yake imejaa uchafu ndoa maana hataki mwenzi wake aiguse. Awe makini nae kwani wanawake wa cku hz wachache sana waaminifu..
 
Salamu wana JF. Kuna mtu mmoja ameniomba ushauri lakini nimeona ni vema kushirikisha wanajukwaa ili tuweze kumpatia jibu lililo sahihi.

Suala lenyewe lipo hivi: Nina jirani yangu ambaye tunaelewana sana, hivi karibuni aliniambia hamwelewi mchumba wake wa kike anayetarajia kufunga naye ndoa hivi karibuni maana (mwanamke) hapendi jamaa ashike simu yake.

Kila siku wanamke anatumia muda mwingi sana kuongea na watu mbalimbali ambao jamaa hawatambui, simu hiyo ipo bize mchana kutwa na hata usiku.

Siku moja mwanake alipokuwa anaoga simu yake iliita zaidi ya mara 3, jamaa akaamua kuipokea, simu ile ilipigwwa na mwanamme ambaye alitaka kuongea na mwenye simu (mwanamke), jamaa akamwambia mwenye simu ametoka kidogo, yule jamaa aliyepiga simu akakata simu.

Mwanamke aliporudi ndani akaelezwa kuhusu simu iliyopigwa. Mwanamke alikasirika sana kwamba kwa nini jamaa (mchumba wake) ameipokea ile simu, ugomvi ilikuwa mkubwa.

Tukio lingine lilitokea siku moja wachumba hao walipokuwa wapo faragha meseji iliingia kwenye simu ya mwanamke, jamaa akataka kumjua aliyetuma meseji lakini mwanamke akamzuia na pia akafuta hiyo meseji, pakatokea tafrani ya nguo kuchanika kwa wapenzi hao.

Kutokana na visa hivyo jamaa anaomba ushauri je huyo mchumba wake ana mapenzi ya kweli kwake? Kwa nini hapendi simu yake ichunguzwe na huyo mchumba wake?

Jamaa anaomba ushauri afanyeje?

huyo cyo dem
 
amwache maana hafai kuwa mchumba leave alone mke,maana ana siri nyingi na ni dhahiri ana marafiki wengi/mahawara...aachane naye kabisa
 
Back
Top Bottom