Tumsaidie huyu... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tumsaidie huyu...

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by mtoto mpole, May 20, 2011.

 1. mtoto mpole

  mtoto mpole JF-Expert Member

  #1
  May 20, 2011
  Joined: Mar 22, 2010
  Messages: 679
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  kuna binti mmoja ana mpenzi wake anampenda kwa dhati na kujitaidi kumfanyia kila lililo ndani ya uwezo wake... na wana mipango mingi na endelevu ndani ya mahusiano yao..sasa basi kuna siku moja huyu binti alipatwa na matatizo akalala nje ya nyumba yao bila kukusudia na mpenzi wake alijua hili na ndo alikua msaada mkubwa saanaa kwa mpenzi wake(huyo binti)....sasa baba wa huyo binti ni mkali usipime ilivotokea hiyo situation ya binti kulala nje ya nyumba alikasirika sana kiasi cha kumuadhibu kama mzazi kumbe haikuishia hapo mzazi akawa anataka mtoto wake aende akasome india mwezi wa tisa akachukue masters ambayo atakaa huko miaka 3...huyo binti akaamua amshirikishe mpenzi wake ila mpenzi wake akawa hataki binti aende kwasababu anampenda sana na anamalengo nae sana tuu..akamwambia bora uapply hapa tz na atamlipia ada na kila kitu.. binti akaliwasilisha hilo kwa mzazi wake kwamba anapenda kusoma TZ na ada atajilipia sasa baba yake akawa hataki coz hana uhakika na tabia ya mwanaye ya hivi karibuni wala uhakika wa binti kujilipia ada anadai bora amtenganishe na marafiki zake aliokua nao coz hawaamini sana ili akaanze moja huko india.....huyu binti anaumia sana hataki kumuacha mpenzi wake sababu mpenzi wake alisema haezi msubiri for three years anything can happen.....huyu binti hayupo tayari kumpoteza mpenzi wake..afanyeje kumridhisha baba yake ili akubali yeye kubakia TZ??? NAWASILISHA KWENU WADAU....MWISHO
   
 2. M

  Marytina JF-Expert Member

  #2
  May 20, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  najisikia kuchoka bora nisichangie ntakuharibia bure uzi wako
   
 3. Kaka Mpendwa

  Kaka Mpendwa JF-Expert Member

  #3
  May 20, 2011
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 771
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  hapo maana yake ni either kumtii baba au boyfriend??

  Je huyo binti ana umri gani?..maana hii itamsaidia kutoharikisha kuolewa kama umri wake utakuwa kwenye range nzuri mfano 22,23 ukijumlisha na miaka 3 ya kusoma itakuwa ni 25 au 26. Anaweza akatimiza ndoto zake za kusoma.

  Pia kijana naye ana umri gani...maana kama yuko 30, kusubiri itamuwia vigumu..

  Kumtii mzazi ni bora zaidi, na haimanishi ndio mwisho wa maisha yake ya mapenzi. Lakini inaonesha mzazi wake ana mtawala sana.. hivyo binti hana nafasi ya kuamua atakalo.. Huyo mzazi anafikiri India ndio hataharibikiwa, amepotea kabisa..mtu kama ni kuharibika, ataharibika popote pale..

  Binti aitishe kikao na baba yake na boyfriend, wakae meza moja waongee, ili wafikie muafaka, sasa kama walikuwa wanafanya kisirisiri, ndo wakati wa kuyaweka wazi, huenda mzazi akaelewa. Jamaa aelezee wasiwasi wake, na binti aeleze anachojifikiria, then mzazi afikie conclusion..
   
 4. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #4
  May 20, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,640
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Hapo binti inabidi mwenyewe apime ni kipi muhimu sana katika maisha yake. Na kuenda India inamaana hata likizo atakuwa harudi? Hapo hata ukisema apeleke posa, mshenga na kijana wote wanaweza uziwa kesi.
  Cha muhimu, kama binti anampenda jamaa basi anaweza kataa kwenda huko India na akamuelewesha baba yake kwamba hata wahindi ni binadamu kama wa tz na anaweza fikiri anawakwepa watz akakutana na wahindi waliowachafu kabisa. Au haoni uozo wanaofanya wahindi hapa?
   
 5. God bell

  God bell JF-Expert Member

  #5
  May 20, 2011
  Joined: May 13, 2011
  Messages: 581
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 45
  Ingekuwa ni wewe mpenzi wako anaenda kusoma india ningekupa msitari ya kwenda kumwambia. But am afreid to tell usije ukaongeza chumvi.
   
 6. Chapa Nalo Jr

  Chapa Nalo Jr JF-Expert Member

  #6
  May 20, 2011
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 6,361
  Likes Received: 3,193
  Trophy Points: 280
  Kumsubiri mtu miaka mitatu wakati naona muda wangu wa kuoa tayari!, no hata mimi siwezi, aamue kwenda shule tu atapataga mwingine kuliko kwenda akabaki kujiaminisha eti ameacha mpenzi Tanzania
   
 7. Da Womanizer

  Da Womanizer JF-Expert Member

  #7
  May 20, 2011
  Joined: May 24, 2010
  Messages: 1,561
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Huyo mzee kama anasoma hapa basi ajue huyo binti akienda india inaweza kula kwake kuliko anavyodhani. Hivi anatumia kitu gani kufikiria, kwani huko India anaenda kuishi na miti???!!!!!!!! Wazazi wengine bana, kaaaaaaaaaazi.
   
 8. e

  ejogo JF-Expert Member

  #8
  May 20, 2011
  Joined: Dec 19, 2009
  Messages: 994
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Masters India 3 yrs!! ya nini hiyo? Binti kama amemaliza bachelor maana yake anaweza kkujitegemea na kujipangia maisha mwenyewe. Kwasasa nadhani baba yake hatakiwi kumlazimisha kufanya jambo bali anatakiwa kumshari.
   
 9. B

  Bendera ya bati Senior Member

  #9
  May 20, 2011
  Joined: Apr 6, 2011
  Messages: 179
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ALIYEUZA CHENI KAPEWA HELA YA BANDIA NA ALIYETOA HELA KAPEWA CHENI YA BANDIA. Tafakari chukua hatua.
   
 10. YoungCorporate

  YoungCorporate JF-Expert Member

  #10
  May 20, 2011
  Joined: Apr 30, 2010
  Messages: 388
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  haya mambo yanahitaji umakini mkubwa, jamaa yangu aliwahi kutosa skolaship ya kusoma ulaya kwasababu ya binti flani hv, binti alivyoanza chuo mwaka mmoja tu jamaa akapigwa kibuti...
   
 11. S

  Sharo hiphop JF-Expert Member

  #11
  May 21, 2011
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 662
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Aache ulimbukeni, akasome.
   
 12. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #12
  May 21, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,237
  Likes Received: 3,654
  Trophy Points: 280
  Nasikia usingizi,wazazi wengine bwana!!
   
 13. ENZO

  ENZO JF-Expert Member

  #13
  May 21, 2011
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 4,057
  Likes Received: 552
  Trophy Points: 280
  watoto w kike bana! kweli wana akili z kuvukia barabara tu.yani usipande pipa kisa mapenzi!! .....naomba mungu kesho mwisho w dunia ukifika wanaume 2baki iwachukue wanawake wote kasoro mama ze2 na demu wangu
   
 14. Big One

  Big One JF-Expert Member

  #14
  May 21, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 759
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  we jamaaa umevuta kidogo nn
   
 15. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #15
  May 21, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,507
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  demu wako na mama yako sio wanawake?sasa utakuta huyo demu wako ndo ana akili za kupumulia tu,hata za kuvukia barabara hana!
  anyways,mtoa mada,mwanaume kama anatoa masharti juu ya maendeleo bado hajakuoa,akimuoa tu huyo dada matisho yataendelea.that is manipulation,u don have to make ur partner make choices over u.u can just advice bana!
   
 16. Susy

  Susy JF-Expert Member

  #16
  May 21, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 1,450
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  kwani tz hakuna vyuo?? kwani huyo mzazi kumpeleka India hakuna wanaume wengine huko?? aaaaaaaaaa

  ingekuwa mimi ndio huyo binti, ningemwambia baba nimeshakua ninauwezo wa kujua kizuri na kibaya, nina nafasi ya maamuzi India siendi!!, na apply Mzumbe University ka-masters kangu nasoma, najua atakasirika mwanzoni tu, ila badae atanielewa tu!!
   
 17. L

  Loloo JF-Expert Member

  #17
  May 24, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 214
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  mtoto hakui kwa mzazi kwana natamani nengepata hiyo bahati kweli kwenye miti hapana wajenzi.mapenzi hayachoki kusubiri hata miaka kumi kama Mungu kamwandikia huyo ndo mume atakuwa sio kujibananisha na akilogwa akakataa kwenda kusoma kisa sharobaro laana ya mzazi itampitia
   
 18. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #18
  May 24, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Jamaa si ana pesa ya kumsomesha mtoto Tz? Ina maana pia ana pesa ya kwenda kwa girl India. Mridhishe mzazi kwa kwewnda India, na wakati huo huo jamaa aanze taratibu za posa. At the end of the day, jamaa atapata mke! Period!!!!
   
 19. 4

  4 PRINCE Senior Member

  #19
  May 24, 2011
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 144
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Huyo binti asiwe mjinga,huyo mwanaume hamfai,kipimo cha kwanza,ni kitendo cha huyo mwanaume kusema kuwa hawezi kumsubiri miaka mitatu.hapo inaonyesha huyo bint anampenda zaidi mwanaume kuliko mwanaume anavyompenda binti.

  Amsikilize baba yake,aende akasome,elimu kwanza,mapenzi baadae.
   
Loading...