Tumrudishe Msigwa tena bungeni

Tumrudishe Msigwa tena bungeni

cantonna

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2013
Posts
1,120
Reaction score
439
Huu ni msemo ambao umetawala midomoni kwa WANAIRINGA wote wenye mapenzi mema na mkoa wetu wa IRINGA.

Huu ni msemo ambao unaleta hamasa kubwa ya kumtambulisha tena MH.MCHUNGAJI MSINGWA ambaye alikuwa mbunge wetu wa Iringa mjini!!

Ama hakika huyu ndiye Mbunge pekee ambaye wana Iringa tunaweza kujisifia,kwani alikuwa kipaumbele kuwatetea wana Iringa wote nje na ndani ya mbunge,tofauti na wabunge waliopita kama wakina Monika Ngezi Mbega,ambao hawakuweza kusimama na kuwatetea wana Iringa ndani na nje ya mbunge!!

Ni mbunge mwadilifu ambaye pia akisimama bungeni lazima bunge litikisike kwa kile atakaho kisema,wenyewe ni mashahidi kwani wote tunafahamu ni kwa namna gani hotuba zake bungeni zilikuwa zina tija gani juu ya maendeleo ya Iringa na nchi kwa ujumla!!

Ni moja ya wabunge machahali walioweza kuonyesha makali yao ndani na nje ya bunge kwa muda mfupi tuu!!

Hivyo wanaIringa wenzangu tusifanye makosa tumchague Msigwa tena kwa maendeleo ya mkoa wetu na nchi kwa ujumla!!

People's power!! MSIGWA TENA!!!
11183442_884394238274557_2726875856837609323_n.jpg

 
Natamani ningekuwa raia wa Iringa mjini nilichague Jembe hili!!
 
"Akili ndogo hazitawali kubwa"
"A problem caused by same mind can not be solved the same level of mind wchich craeted it"
Hata jk hajaweza kutoa sentens kubwa kama hii. Big up jembe la Iringa.
 
anadhalilisha taaluma ya uchungaji.. ni bora ieleweke kuwa ameacha uchungaj ni mwanasiasa kama dr slaa..! VITA VYAKE HAVIPASWI KUWA VYA ULIMWENGU HUU BALI VYAPASWA KUWA VYA KIROHO.. MATHAYO 7;21
 
hata mimi naunga mkono msigwa wanairinga wamrudishe bungeni pamoja na kuwa sio shabiki wa chadema achilia mbali kuwa mwanachana. Tuna mhitaji msigwa yule wa kipindi kagasheki akiwa waziri wa maliasili sio huyu wa kipindi cha nyalandu. we want strong opposition mp. wengine ni Zitto, Lisu, mdee, mnyika kafulila (kupitia ACT), machali, na wanaofanania na hao. hawa niliowataja ni watu wa hoja. mtu kama sugu, lema kibajaji, prof. maji mafupi, asumpta na wanaofanania tupe mbali kabisa kule.
 
Alifanyamsemo wa 'akili ndogo kutawala akili kubwa' kuwa maarufu na kutumiwa na pande zote za bunge letu na nje ya bunge.
 
anadhalilisha taaluma ya uchungaji.. ni bora ieleweke kuwa ameacha uchungaj ni mwanasiasa kama dr slaa..! VITA VYAKE HAVIPASWI KUWA VYA ULIMWENGU HUU BALI VYAPASWA KUWA VYA KIROHO..
MATHAYO 7;21

sindano ya nyuki;

Acha hizo porojo za kipuuzi. Hoja yako haina mashiko hata chembe. Sote tunaijua dini bwana. Hivi unafikiri Wachungaji, Maaskofu na Mapadre hawana sehemu au mchango wao katika siasa? Kwenye Biblia Takatifu tunasoma habari za Wafalme kina Daudi, kina Sulemani na wengine, hawa walikuwa ni watawala walikaa kwenye Ikulu na kuongoza watu wao.

Mbona hawahawa wana siasa wanapotaka kupata kura wanaenda kwenye nyumba hizo za ibada kuwaomba hawahawa Wachungaji na Maaskofu kushawishi watu wao wawape kura?

Msigwa anastahili kurudi Bungeni kwani ametoa mchango mkubwa sana kwenye hili Bunge lililopita. Msigwa anaweza kuwa sawa na Wabunge 50 wa CCM.
 
Back
Top Bottom