Tumpongezeni JK kwa Uhuru huu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tumpongezeni JK kwa Uhuru huu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Malaria Sugu, Jul 8, 2009.

 1. Malaria Sugu

  Malaria Sugu JF-Expert Member

  #1
  Jul 8, 2009
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 2,653
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nadhanu wa tz hatuna budi kumpongeza Utawala wa JK kwa kutupatia uhuru wa kusema, kujadili na kuamua hatma ya nchi yet. nadhani na tukubali kwamba sasa tz imetoka kwenye utawala uliokuwa kila kitu kwao mwiko, sasa bunge letu limeimarika Kihoja, Vyombo vya habari nusu ya uhuru na sio robo ya robo ya awamu ya 3, Taasisi za Dini nazo zinasema, kwakweli naweza kusema ukombozi mpya (Uhuru mpya wa TZ baada ya ule 1961 )
  Jee kama Jk angalikuwa kama utawala uliopita haya yote ya Richmond na mengine tungaliyajua?
   
 2. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #2
  Jul 8, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Kuelekea 2010 watatumwa wengi humu JF..lolz
   
 3. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #3
  Jul 8, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Haikuwa matakwa yake bali ni za alama za nyakati.EL aliwazuia Wabunge kwa vimemo kuhusu Richmond lakini aliishia wapi.Hata ya ufisadi anayalea yatagota tu mahali.
   
 4. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #4
  Jul 8, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Huyu naye naona kajiunga JF juzi juzi tu.
   
 5. Tatu

  Tatu JF-Expert Member

  #5
  Jul 8, 2009
  Joined: Oct 6, 2006
  Messages: 1,081
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Tumpongeze JK au Mwenyenzi Mungu kwa kutupa UTASHI.

  Kazi ya Mungu haina makosa ila binadamu kwa matakwa yao ndio wanajaribu kudhibiti na kubadili maana ya madhumuni yake.

  Uhuru wa kujadili jambo lolote lile ni HAKI YA BINADAMU wote.
   
 6. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #6
  Jul 8, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Umpongeze JK kwa lipi? Vp unaota nini?
   
 7. Kwetunikwetu

  Kwetunikwetu JF-Expert Member

  #7
  Jul 8, 2009
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 1,544
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Tumpongeze kwa lipi, hata akitaka kuzuia uhuru huu hawezi....! Kweli mpaka tufike 2010 wengi waliotumwa watajiunga humu JF
   
 8. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #8
  Jul 8, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hii ni hatari sana kwa taifa.
   
 9. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #9
  Jul 8, 2009
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,504
  Likes Received: 2,744
  Trophy Points: 280

  Hakuna kitu cha kumpongeza. Watu walishaanza kusema hata wakati wa Mkapa. BCS watu tulilonga sana mpaka Nyaurawa (RIP) akaifunga, JF imeaanza enzi za Mkapa lakini ilifungiwa wakati wa Kikwete.

  Kwa hiyo hayo unayoyasema ni swala la muda tu kwamba huwezi ukawanyima watu uhuru wao wa kutoa mawazo yao isipokuwa hawavunji sheria. Hata China, Cuba na Urusi watu taratibu wanaaza kupata uhuru wa kutoa mawazo yao.

  Kuhusu uvujaji wa siri za serikali ni ishara kuwa JK na serikali yake hawana usimamizi wa kutosha. Kama JK alikuwa anataka tuyajue mambo ya Richmond, EPA n.k. inakuwaje leo Hawa Ghasia analalamika kuhusu uvujaji wa siri na doc. za serikali.

  Swala hapa ni kwamba serikali ya sasa ni legelege na haiwezi kazi. Na kwa kuwa kila mtu anfahamu hilo ndiyo maana mambo mengi yanavuja.
   
 10. kinepi_nepi

  kinepi_nepi JF-Expert Member

  #10
  Jul 8, 2009
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 870
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  hiki ni kichefu chefu cha mwaka.
  Labda umpongeze kwa kutumia kodi zetu kupanda ndege kukimbia kazi aliyopewa.
  hafai hata kwa kuvundika.
   
 11. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #11
  Jul 8, 2009
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Hongera Kikwete kwa kutupatia uhuru wa kuongea
   
 12. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #12
  Jul 8, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Kwa nini upongeze nusu uhuru wakati unatakiwa kupata uhuru kamili? Huoni kwamba huu ndio wakati muafaka kudai hiyo nusu nyingine?
   
 13. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #13
  Jul 8, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Kweli mbaya halisi na wema hakosi.
  Fikiria kama tungekuwa enzi zile za Mwalimu halafu kuna kitu kama hichi JF? hata kama angekubali kuwepo kwake asingekubali mjiite Great thinkers( mkijiita hivyo, halafu yy ajiite nani?) na ndo maan vyombo vya habari vilikuwa vya serikali tu, ukitaka habari huru usikilize BBC kama mawimbi unayapata na redio yako ya mkulima ina betri za kutosha au wenzetu wa mipaka ni kaskazini kule wadowee mageziti ya Kenya na Uganda kupata habari huru. Hapo ilikuwa RTD, Uhuru, Mzalendo,Mfanyakazi, Dailynews, karibu yote ya serikali. Habari ni ujamaa na kujitegemea. Mwalimu pekee ndo ana feature. Hakuna kauli mbadala na zake.
  Hakuna aliyejuw sku hizo kuwa ugomvi wake na Mkapa katika mkutano wa baraza la mawaziri ni kuwa, Mkapa alikosoa utaratibu fulani wa Mwalimu kwa nia njema tu, yaliyomkuta!! salama akafurushiwa ubalozini Canada na akaambiwa Tanzania utaiyona kwenye ramani tu kwa kidomodomo na ujuwaji wako. Kama si kuja kupiga magoti kwa Mwalimu amsamehe, jina lake lisinge kuwa katka hisoria iliyopo sasa na pengine kashfa za migodi ya kiwira zingekuwa kwa mtu mwengine na si yeye.
  Kwahiyo uhuru wa habari kama alivyose Lord Camden karne ya 18, kuwa "inherent necessity to the mass". Watz wasiache kumshukuru JK walau kwa hili linaloonekana dogo tu lakini kubwa kwa wanaojuwa umuhimu wake. Kuna watu wamenyongwa na kupata mateso makubwa kwa kukosekana uhuru huu tu, watu kama Kasella Bantu, Elli Anangisye,L.Mwijage, marehemu Ali M. Nabwa n.k walipata manyanyaso makubwa na uhuni wa kupindikia. Hakukuwa na wa kuwasemea wala kuandika dhuluma ya mwanyanyaso na mateso walioyapata katika kambi za mateso za siri za Mw. Nyerere kwa kuwa hakukuwa na vyombo huru vya kusema siku hizo. Leo tumeona wafanyabiashara wa Mahenge waliouliwa na Askari Polisi kwa kuwa tu vyombo vya habari vipo huru na vimesema na hatua zimechukuliwa.
   
 14. Mazingira

  Mazingira JF-Expert Member

  #14
  Jul 8, 2009
  Joined: May 31, 2009
  Messages: 1,837
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  It might be true huyu ndugu kajiunga jana tu hapa. Ngoja tuendelee kusikilizia zaidi huenda ndo kampeni zimeanza hivyo.
   
 15. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #15
  Jul 8, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280

  kwanini tusimshukuru kwa kutupa uhuru wa kuabudu? Kwanini tusimshukuru kwa kutupa uhuru wa kula na kunywa? Kwanini tusimshukuru kwa kutupa uhuru wa kulala na kulalana? Kwanini tusimshukuru kwa kutupa uhuru wa kuona na kuonwa? Na wakati tunafanya hivyo kwanini tusimshukuru kwa kutupa uhuru wa kuwa Watanzania?
   
 16. Obhusegwe

  Obhusegwe JF-Expert Member

  #16
  Jul 8, 2009
  Joined: Dec 28, 2008
  Messages: 232
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  mzeewahoja
  Junior Member
  Join Date: Tue Jul 2009
  Posts: 9
  Thanks: 0
  Thanked 1 Time in 1 Post


  We unaejidai mzee wa hoja, acha kutuzingua na mambo ya JK! Umejiunga humu juzijuzi sasa unakuja na hoja za kufagilia uozo. Tushakustukia mamluki wewe, tuachie jamvi letu... kikomo cha mafisadi!!

  ....MAPAMBANO YANAENDELEA!
   
 17. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #17
  Jul 8, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,840
  Likes Received: 1,099
  Trophy Points: 280
  Haki haitolewi na mtu, mtu anapata haki kwa kuwa tu amezaliwa mwanadamu, hizi ndiyo zinaitwa haki za binadamu. Uhuru wa kuongea/kusema, kula, kuona, kuabudu, kulala nk. ni haki. Hivyo unapoipata huna haja ya kumshukuru yeyote.

  Kutoa shukrani eti kwa kuwa umepewa haki, kunadhihirisha fikra kandamizi, yaani kujawa na fahamu za kuwamtawaliwa (colonized) kiasa cha kumshukuru mkoloni (kifra) kwa kutokukunyima baadhi ya haki (kukuachia upenyo fulani). Mtoa hoja (kutokana na fikra tawaliwa) anaona kwamba Kikwete alipaswa kutuzuia kusema na kwakuwa hajazuia basi anastahili pongezi.

  Kataa kukubali (hali ya kifra) kuwaumetawaliwa (colonized). Haki ni haki wala si upendeleo.

  maelezo ya ziada: haki = rights. Hata mahakama hazitoi haki bali justice (sijui neno la kiswahili).
   
 18. Sekenke

  Sekenke Senior Member

  #18
  Jul 8, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 132
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Congrats to who? I bet you want to send shout outs to former President Mwinyi who changed Tz politics from monoparty to multiparty? And remember, the citizenry had just voted against multiparty? Huh, you didn't know that? Now you do.

  Bottomline. There is a wind of change, a gradual but steady, and a very strong one. There are also self inflicting wounds on the Govt fuelling the change. The president has only once choice, the better choice. If he chose otherwise, he becomes part of the drain.

  And stop congratulating someone for doing a job they are employed and being paid up for. What they are fulfilling is/was stipulated in the constitution years back.
   
 19. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #19
  Jul 8, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Hata kama angekuwa hataki asingeweza kuzuia "NO ONE CAN RESIST HUMAN RIGHTS" ni haki yetu kuwa huru... kwahiyo hatuna haja ya kumfagilia mtu...akizuia haki hii tutamwandama kwa njia yeyote ile mpaka ipatikane whetever it takes???
   
 20. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #20
  Jul 8, 2009
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,711
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  haya ni mambo ya nyakati ambayo haya usiani na nyerere, mwinyi, mkapa au kikwete. yeyote yule ingebidi akubaliane nayo maana yake ukiyapinga tiyari unakuwa unatafuta vita nyingine isiyokuwa ya maana

  huwezi kupingana/kushindana na technologia
  enzi za nyerere internet/computer vilikuwa vitu adimu hata ulaya, sasa hivi kila kitu kimeshuka bei na haijasababishwa na raisi yeyote yule wa TZ....

  huwezi kumshukuru mtu kwa kupata kile tunachostahili, kama angekuwa anatufanyia msaada na hatupaswi kupata then tungemshukuru kwa ajili ya favour
   
Loading...