Tumpongeze Raisi Magufuli kwa hili jambo alilolifanya.

radika

JF-Expert Member
Jul 15, 2014
20,440
32,253
Neema Mwita Wambura alimwagiwa maji moto na Mume wake baada tu ya mume huyo kukasirika kwasababu Neema alichuma Mahindi mabichi na kuyapika bila kibali cha mumewe na baada ya hapo majeraha yamekua yakimsumbua…

Baada ya Rais Magufuli kumuona amefanya maamuzi ya kumpigia simu pamoja na kumuahidi matibabu pia kaahidi kusidaia familia ya mama huyo pindi atakapo kuwa kwenye matibabu.

Kishamsaidia pesa za matibabu na kiasi kingine kimepelekwa kuhudumia watoto wa huyo mama huo ni moyo wa kibinadamu kuguswa na mambo kama hayo hasa wanyonge wanapohangaika nampongeza sna mheshimiwa.
 
Kwaivyo huyo mama ndo nchi nzima yuko peke ake.....
Angeamua kusaidia wananchi walio ktk hali hyo sio mtu moja...
DOUBLE STANDARDS
kuja tu kwenye mediaaa....

Sikuizi media ndo mahakama
 
hilo tu ndo apongezwe wakati kiroba cha unga kinakinbilia elfu 30 kwangu mbando
 
Kick tu hamna chochote,hivyo ni vitu minor sana alitakiwa mkuu wa wilaya afanye hivyo sio rais kujifanya ngozi ya kondoo huku rohonu kila mtu anajua ni mtu wa namna gani
 
Yeye ni rais wa watanzania mil 50,maelfu anawatendea ukatili, mimi mil 10 zangu kazinunulia ndege kutoka mfuko wa PPF, bukoba aliwatukana, huyu mtu mmoja tu wengi anatuumiza ni sawa na hamna tu.
 
Mpenda sifa tu anasaidia 1 kwenye million 20 wenye shda hafu ndo aonekane ana moyo safi? Mnapozd kumpongeza ndo atakuwa anatafta mtu mmoja mmoja ili apate sifa na kusahau mamilion ya watu wanaolia kila kukicha,
 
Mpenda sifa tu anasaidia 1 kwenye million 20 wenye shda hafu ndo aonekane ana moyo safi? Mnapozd kumpongeza ndo atakuwa anatafta mtu mmoja mmoja ili apate sifa na kusahau mamilion ya watu wanaolia kila kukicha,
Hamna rais hajakosea wala sifa tuwe na moyo wa kupongeza muda flan
 
Ni jambo jema sawa lakini unyanyasaji wa namna hio ni maeneo mengi umeshamiri!!Kumsaidia huyo mmoja ni sawa na tone la damu baharini
my take is,Kama kweli ana nia njema na nzuri ya kusaidia kina mama wengi wanaopatwa na mtatizo ya namna hio ni vema serikali ingeanzisha asasi mbalimbali na taasisi za kutetea haki za binadamu,,zipewe mamlaka na nguvu ya fedha kufanya kazi nchi nzima!!

Bado hajanishawishi nimuone mwema kwa sababu;
1.Kavunja mkataba wangu mpaka leo sijapata ongezeko la mshahara la kila mwezi wa 7

2.Kasaini makato ya asilimia 15% bodi ya mkopo ile hali mimi mlipaji nilisaini asilimia 8%

3.Hakuna ajira mpaka sasa,,kupanda madaraja kwa watumishi,,uhamisho n.k

4.Sijalipwa malimbikizo ya mishahara yangu na stahiki zinginezo


HIVI MPAKA LEO MMESIKIA HATUA GANI IMECHUKULIWA JUU YA HAO WALIOSABABISHA UBADHILIFU WA FEDHA ZA SERIKALI KUPITIA WATUMISHI HEWA??NANI KAFUNGWA??

Thats why sijawahi na sitokuja kupenda chama kijani!!
 
Unafiki gunia tele! Aache kumuadabisha mtenda halafu kesho akija mwingine? Stupid nonsense. Katoahela yake au kodi yako? Think!!!!
 
Hakuna lolote apo ni usanii mtupu, hivi kumsaida mtu ni lazima iwe mbele ya waandishi wa habari wenye makamera makubwa makubwa, kwani ukimsaida tuu pasipo makamera Mwenyezi Mungu atakunyima thawabu kweli? au ndiyo makafara ya kimtindo hayoo?
 
Vipi kwa wana-BUKOBA!!
Ame swindle rambirambi na michango yetu kwa wahanga ndio unasema tumpongeze nduli huyu!
Hujanishawishi bado.
 
Back
Top Bottom