Kikombe1
Senior Member
- Feb 4, 2013
- 132
- 99
Natumaini kila mtanzania ameshtushwa na kifo cha mchapakazi na msomi wa sharia, Dr. Mvungi. Mazingira ya kifo chake ni yakusikitisha na yanawakilisha aina ya maisha aliyokuwa akiishi kama ilivyo kwa wasomi wengine wanaoishi maisha ya kawaida katika mitaa na majengo ya kawaida. Kujenga nyumba na kuishi eneo lisilo na umeme na nyumba inayoendelea kujengwa ni hali ya kawaida hapa Tanzania. Hivi kwanini eneo hilo lisiwe na umeme? hivi ni watanzania wangapi wanakutwa na wavamizi wenye mapanga katika maeneo kama hayo??