Tumkumbushe Nape Nnauye alikopitia mpaka alipofikia na anakoenda

MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Nov 28, 2015
28,707
71,003
Nape Nnauye ni mwasiasa kijana, hakuna atakayepinga kuwa Nape amesaidiwa sana na mzee JK mpaka kufika hapo alipo, sasa tumkumbushe mapito yake

■Nape alikuwa pale makao makuu ya UVCCM, Lowassa alipotenguliwa Nape alikuwa mstari wa mbele kumtukana Lowassa

■Baada ya matusi kuzidi mzee Makamba akiwa katibu mkuu wa CCM akamtimua Nape UVCCM na kumvua uanachama, na kumwambia huwezi kukata tawi la mti ulilokalia na ukabaki salama, ikatokea maneno maneno meeeengi kuwa nape sio mtoto wa mzee Nnauye, kuna mama mmoja akajitokeza na kusema Nape siyo mtoto wa mzee Nnauye n.k.

■Wazee wakongwe wa CCM kama mzee msuya wakapinga kuwa huo sio utaratibu wa CCM wa mtu mmoja kuwavua wanachama uanachama wa CCM, kuna vikao vyenye mamlaka hayo

■Mzee JK na wazee wengine wakamrudishia uanachama wake Nape

■Mzee JK akamteua Nape kuwa mkuu wa wilaya, sikumbuki wilaya gani

■Kwa kuwa mzee JK alikuwa anataka kumlea vizuri nape, akampa ukatibu mwenezi CCM

■Mzee JK hakuchoka, akamshauri nape kugombea ubunge na akamsimamia mpaka akawa mbunge, mpaka akapata na uwaziri

Baada ya mzee wa watu kurudi Msoga kupumzika, Nape si akasahau malezi yote mazuri ya mzee JK, akarudia tena urafiki na mzee Makamba, sasa kuna clip Nape anaongea na mzee Makamba anasema nyie wazee wetu mmefanya kazi kubwa ya kutuzaa tunashukuru tutaifanya hii kazi vizuri, amesahau yooooote yaliyompata

Wakuu naomba tuendelee kumkumbusha na kumshauri nape
 
Kweli nape ni mtata
Kipindi kile akiwa kijana mbichi kabisa kuelekea 2005 nape alisikika akimkejeli kikwete kuwa Ccm haiwezi kuongozwa na MTU muhuni na dhaifu kwa kifupi nape alikuwa hataki kabisa kikwete awe mgombea wa Ccm huku yeye akimpigia chapuo mwandosya

Kisa cha nape kumtukana magufuli kwenye simu sikushangaa hata kidogo nikijana ambaye anaongea kile anachoona kinafaa kwake

2005 kundi kubwa sana lilikuwa linampinga kikwete hadi kikaanzishwa chama mbadala cha siasa ili kupambana na kikwete
Ashukuriwe Lowasa aliyeamua kwa moyo mmoja kumpigania rafiki yake hadi akashinda.

Nape anakosa kitu inaitwa managerial skills yeye huwa haamini katika kuongozwa anachojua yeye ni kuongoza tu hii wanasiasa wengi huwa inawaangusha
 
Nape anachoangalia tumbo lake na cheo ndio maana yupo kufanya lolote hili mradi afanikiwe katika hayo
 
Nasoma comments hapo juu naona Lumumba mmejipanga kumkabili kijana Nape, poleni sana nyie harisheni saa yaja labda nanyie mnalipwa vinginevyo.
 
Shirika La Wachochea Kuni Tanzania [SHIWAKUTA] Linapenda Kuwapongeza Wanachama Wake Kwa Kazi Kubwa Ya Kuchochea Moto Waliyoifanya Mpaka Sasa! Hata Hivyo Shirika Linawakumbusha Wanachama Wake Kutosahau Kuongeza Kuni Na Kuchochea Ili Moto Uwake Zaidi.

Diasporajay

Katibu Mwenezi SHIWAKUTA
 
Kweli nape ni mtata
Kipindi kile akiwa kijana mbichi kabisa kuelekea 2005 nape alisikika akimkejeli kikwete kuwa Ccm haiwezi kuongozwa na MTU muhuni na dhaifu kwa kifupi nape alikuwa hataki kabisa kikwete awe mgombea wa Ccm huku yeye akimpigia chapuo mwandosya

Kisa cha nape kumtukana magufuli kwenye simu sikushangaa hata kidogo nikijana ambaye anaongea kile anachoona kinafaa kwake

2005 kundi kubwa sana lilikuwa linampinga kikwete hadi kikaanzishwa chama mbadala cha siasa ili kupambana na kikwete
Ashukuriwe Lowasa aliyeamua kwa moyo mmoja kumpigania rafiki yake hadi akashinda.

Nape anakosa kitu inaitwa managerial skills yeye huwa haamini katika kuongozwa anachojua yeye ni kuongoza tu hii wanasiasa wengi huwa inawaangusha
Kilaza yule. Anaswagwa tu kama Ng'ombe hajui kufanya analysis ya kitu anachoenda kukifanya. Ona kwenye simu anaongea kwa uhuru kabisa eti mshamba yule,anamwambia Makamba Baba eti hii vita mtuachie sisi nyie mlituzaa inatosha. Pumbavu kabisa huyu jamaa.
 
Shirika La Wachochea Kuni Tanzania [SHIWAKUTA] Linapenda Kuwapongeza Wanachama Wake Kwa Kazi Kubwa Ya Kuchochea Moto Waliyoifanya Mpaka Sasa! Hata Hivyo Shirika Linawakumbusha Wanachama Wake Kutosahau Kuongeza Kuni Na Kuchochea Ili Moto Uwake Zaidi.

Diasporajay

Katibu Mwenezi SHIWAKUTA
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom