Tumkumbushe Mchungaji mtume Mwingira

NIMKUMBUSHE MCHUNGAJI MWINGIRA.

Na Elius Ndabila
0768239284

Wiki hii kumekuwa na video ambayo inazunguka ikimuonyesha Mchungaji Mwingira (mpakwa mafuta) akiwa kanisani akihubiri Waumini wake. Kipande nilichofanikiwa kukiona ni kile ambacho Baba Mchungaji MWINGIRA anahusishanisha upigwaji wa Risasi Lissu na mchakato tunaouendea wa Uchaguzi. "Lisu hajajenga flyover lakini watu wanamfuata" Pastor MWINGIRA.

Kabla sijamkumbusha mambo mengi Baba Mchungaji MWINGIRA, ninaomba nikiri kuwa mimi ni msomaji mzuri wa Vitabu alivyoviandika MTUME MWINGIRA. Vitabu vyake ambavyo nimebahatika kusoma ambavyo vimeandikwa kwa ustadi mkubwa ni TABIA YA KUTEMBEA NA MUNGU UVUNE, MTEMBEO WA MUNGU KWA HAO ALIOWARIDHIA NA MOYO WA KIONGOZI. Ninaomba nikiri pia kuwa ni mmoja ya watu tunaofuatilia magundisho yake na mara nyingi nimebarikiwa nayo sana. Lakini leo ninataka kumkumbusha mambo machache ili kukazia maarifa yake.

Baba Mchungaji (Mtume) MWINGIRA kwenye video yake kwa ufupi amesema Lisu anafaa kuwa Rais kwa kuwa pamoja na kupigwa Risasi nyingi lakini bado anaishi. MWINGIRA anasema kitendo cha Lisu kuendelea kuishi pamoja na risasi alizopigwa ni kusudi la Mungu kuwa anatosha kuwa kiongozi mkubwa wa nchi. Anaendelea kukazia hoja zake kwa kusema Lusu hajajenga Fly Over Kama wengine, lakini bado watu wanamfuata.

Wakati nikiwa ninamsikiliza Mchungaji MWINGIRA rafiki yangu mmoja amenitumia video ya mzee Wasira(Vijana wanamwiti Mwenyekiti wa waliokatwa kwenye mchakato) akisema kuwa kama sifa ya kuwa Rais ni kupigwa risasi, basi watu wengi watatamani wapigwe risasi ili wawe Marais. Hoja ya Mzee Wasira inanipa nguvu na inaongeza wigo wa kufikiria. Kwa mkutadha huo nimkumbushe Mchungaji MWINGIRA kuwa Lisu si mtu wa kwanza kupigwa Risasi nyingi na kuendelea kuishi. Wapo watu wengi ambao Dunia walishapigwa Risasi lakini hawakupata huruma ya kuwa Marais wala hawakuwahi kutamani kuomba hizo nafasi.

Hawakuomba hizo nafasi kwa kuwa walijua fika kuwa sifa ya kuwa Rais si kupigwa risasi bali ni uwezo, uzalendo, ushujaa na uhodari katika kukabiliana na majukumu ya nafasi hiyo. Waliowahi kupigwa risasi na hawakupa nafasi za uongozi ni:- Rapper 50 Cent alipigwa risasi zaidi ya tisa mwaka 2000 hakuomba Urais ila baada ya hapo alitoa albamu tatu.

Mwaka 2006 Joseph Guzman alipigwa risasi 19 hakufa na hakuomba nafasi ya Urais. Pia mwaka 1995 kuna mtu kutoka North Carolina alipigwa vibaya na risasi zaidi 20 hakuomba wala hakuwa Rais. Ninamkumbusha mtume MWINGIRA kwa kuwa ninajua huenda alikuwa hajui na kudhani Lisu ni mtu wa kwanza kupigwa.Hivyo nimtahadharishe Mchungaji kuwa Urais si hisani bali wapiga kura pamoja na kusikiliza sera wanazo haki za kuwapima wagombea na vyama vyao.

Hata hivyo Mchungaji MWINGIRA anafanya makosa, labda kama tu ni shetani ameamua kumtumia Mpakwa mafuta huyu kufikisha matamanio yake. Kanisani si mahali pa kufanyia siasa, ninatamani MWINGIRA atoke kanisani kama walivyotoka akina Bagoza, Gwajima n.ksi mahali pa kufanyia siasa, ninatamani MWINGIRA atoke kanisani kama walivyotoka akina Bagoza, Gwajima kupanda majukwaani. Kanisani ibaki ni sehemu ya kuabudia isiwe sehemu ya kufanyia kampeni.

Neno la Mungu ndilo chakula cha roho ambacho mtumishi wa Mungu anapaswa kuwapa watu kwa wakati wake. Ili uweze kulisha watu ipasavyo ni lazima kuelewa mahitaji yao na wakati sahihi unaofaa kuwalisha.

Mahubiri sahihi ni yale ambayo Yesu Kristo ni sehemu ya mahubiri hayo kwa lengo la kuokoa roho za watu, ndivyo walivyo hubiri mitume wote kwenye Biblia Takatifu. Lakini anapotokea Mchungaji anahubiri siasa ambazo si sehemu ya maandiko matakatifu ni kulifanya hekalu la Bwana kuwa pango la SHETANI.

Lakini hata hivyo si dhambi kwa wapakwa mafuta wa Mungu kufanya siasa, lakini ni DHAMBI kubwa kutumia nyumba ya Ibada kufanya siasa. Kuwa na aina hii ya watumishi wanaoweza kutumia nyumba za Ibada ni sawa na kugeuza hekalu la Mungu kuwa kijiwe cha wahuni.

Makanisa na misikiti toka zamani hayakuwa na milengo ya kisiasa, lakni kadri siku zinavyozidi kwenda ninaona tunaanza kuingiza siasa. Kwa kauli ya Mtume MWINGIRA watu wasio na mlengo wa kumchagua Lisu hawapaswi kuwa waumini wa kanisa hilo. Ushauri wangu ni kuwa MWINGIRA apande Majukwaani kumunadi Tundu badala ya kutumia eneo takatifu kufanya kampeni.
Mimi niliangalia huduma yake sikumoja nilichokiona kwenye kanisa ambalo ni tawi lakee kwaakwelii sitorudia tenaa.
 
Kwa hiyo Mwingira anataka abaki na waumini wafuasi wa chadema tu ? Wa CCM hawataki?

Wana CCM mnaosali kwa Mwingira mwachieni kanisa lake katafuteni Makanisa mengine waachieni Chadema
Gwajima amebaki na waumini ccm.
 
Sawa kabisa usemayo. Kwenye madhabahu si mahali pa kuzungumzia siasa kwa sababu waumini wanatoka pande tofauti za kisiasa ingawa kiimani wako pamoja. Mchungaji ana uhuru wa kumpenda mgombea fulani na ni haki yake ampigie kura mtu huyo. Lakini asimshabikie kwenye madhabahu kwa kuwa waumini wengine wanatofautiana naye kisiasa.

Hili ndilo kosa analofanya pia Askofu Bangoza. Mtu chagua kuwa mwanasiasa au kuwa mchungaji. Ukichagua siasa, hapo ndiyo una haki ya kumpigia debe unayempenda.

Lakini kama unachagua uchungaji, mapenzi yako kwa mgombea fulani yabakie moyoni mwako tu na si kuwashawishi wengine. Siku ya kura utatekeleza mapenzi yako bila watu wengine kufahamu umempigia nani.
Ila wale waliofanya kongamano kuipongeza serikali ya CCM walikuwa sahihi.
 
NIMKUMBUSHE MCHUNGAJI MWINGIRA.

Na Elius Ndabila
0768239284

Wiki hii kumekuwa na video ambayo inazunguka ikimuonyesha Mchungaji Mwingira (mpakwa mafuta) akiwa kanisani akihubiri Waumini wake. Kipande nilichofanikiwa kukiona ni kile ambacho Baba Mchungaji MWINGIRA anahusishanisha upigwaji wa Risasi Lissu na mchakato tunaouendea wa Uchaguzi. "Lisu hajajenga flyover lakini watu wanamfuata" Pastor MWINGIRA.

Kabla sijamkumbusha mambo mengi Baba Mchungaji MWINGIRA, ninaomba nikiri kuwa mimi ni msomaji mzuri wa Vitabu alivyoviandika MTUME MWINGIRA. Vitabu vyake ambavyo nimebahatika kusoma ambavyo vimeandikwa kwa ustadi mkubwa ni TABIA YA KUTEMBEA NA MUNGU UVUNE, MTEMBEO WA MUNGU KWA HAO ALIOWARIDHIA NA MOYO WA KIONGOZI. Ninaomba nikiri pia kuwa ni mmoja ya watu tunaofuatilia magundisho yake na mara nyingi nimebarikiwa nayo sana. Lakini leo ninataka kumkumbusha mambo machache ili kukazia maarifa yake.

Baba Mchungaji (Mtume) MWINGIRA kwenye video yake kwa ufupi amesema Lisu anafaa kuwa Rais kwa kuwa pamoja na kupigwa Risasi nyingi lakini bado anaishi. MWINGIRA anasema kitendo cha Lisu kuendelea kuishi pamoja na risasi alizopigwa ni kusudi la Mungu kuwa anatosha kuwa kiongozi mkubwa wa nchi. Anaendelea kukazia hoja zake kwa kusema Lusu hajajenga Fly Over Kama wengine, lakini bado watu wanamfuata.

Wakati nikiwa ninamsikiliza Mchungaji MWINGIRA rafiki yangu mmoja amenitumia video ya mzee Wasira(Vijana wanamwiti Mwenyekiti wa waliokatwa kwenye mchakato) akisema kuwa kama sifa ya kuwa Rais ni kupigwa risasi, basi watu wengi watatamani wapigwe risasi ili wawe Marais. Hoja ya Mzee Wasira inanipa nguvu na inaongeza wigo wa kufikiria. Kwa mkutadha huo nimkumbushe Mchungaji MWINGIRA kuwa Lisu si mtu wa kwanza kupigwa Risasi nyingi na kuendelea kuishi. Wapo watu wengi ambao Dunia walishapigwa Risasi lakini hawakupata huruma ya kuwa Marais wala hawakuwahi kutamani kuomba hizo nafasi.

Hawakuomba hizo nafasi kwa kuwa walijua fika kuwa sifa ya kuwa Rais si kupigwa risasi bali ni uwezo, uzalendo, ushujaa na uhodari katika kukabiliana na majukumu ya nafasi hiyo. Waliowahi kupigwa risasi na hawakupa nafasi za uongozi ni:- Rapper 50 Cent alipigwa risasi zaidi ya tisa mwaka 2000 hakuomba Urais ila baada ya hapo alitoa albamu tatu.

Mwaka 2006 Joseph Guzman alipigwa risasi 19 hakufa na hakuomba nafasi ya Urais. Pia mwaka 1995 kuna mtu kutoka North Carolina alipigwa vibaya na risasi zaidi 20 hakuomba wala hakuwa Rais. Ninamkumbusha mtume MWINGIRA kwa kuwa ninajua huenda alikuwa hajui na kudhani Lisu ni mtu wa kwanza kupigwa.Hivyo nimtahadharishe Mchungaji kuwa Urais si hisani bali wapiga kura pamoja na kusikiliza sera wanazo haki za kuwapima wagombea na vyama vyao.

Hata hivyo Mchungaji MWINGIRA anafanya makosa, labda kama tu ni shetani ameamua kumtumia Mpakwa mafuta huyu kufikisha matamanio yake. Kanisani si mahali pa kufanyia siasa, ninatamani MWINGIRA atoke kanisani kama walivyotoka akina Bagoza, Gwajima n.ksi mahali pa kufanyia siasa, ninatamani MWINGIRA atoke kanisani kama walivyotoka akina Bagoza, Gwajima kupanda majukwaani. Kanisani ibaki ni sehemu ya kuabudia isiwe sehemu ya kufanyia kampeni.

Neno la Mungu ndilo chakula cha roho ambacho mtumishi wa Mungu anapaswa kuwapa watu kwa wakati wake. Ili uweze kulisha watu ipasavyo ni lazima kuelewa mahitaji yao na wakati sahihi unaofaa kuwalisha.

Mahubiri sahihi ni yale ambayo Yesu Kristo ni sehemu ya mahubiri hayo kwa lengo la kuokoa roho za watu, ndivyo walivyo hubiri mitume wote kwenye Biblia Takatifu. Lakini anapotokea Mchungaji anahubiri siasa ambazo si sehemu ya maandiko matakatifu ni kulifanya hekalu la Bwana kuwa pango la SHETANI.

Lakini hata hivyo si dhambi kwa wapakwa mafuta wa Mungu kufanya siasa, lakini ni DHAMBI kubwa kutumia nyumba ya Ibada kufanya siasa. Kuwa na aina hii ya watumishi wanaoweza kutumia nyumba za Ibada ni sawa na kugeuza hekalu la Mungu kuwa kijiwe cha wahuni.

Makanisa na misikiti toka zamani hayakuwa na milengo ya kisiasa, lakni kadri siku zinavyozidi kwenda ninaona tunaanza kuingiza siasa. Kwa kauli ya Mtume MWINGIRA watu wasio na mlengo wa kumchagua Lisu hawapaswi kuwa waumini wa kanisa hilo. Ushauri wangu ni kuwa MWINGIRA apande Majukwaani kumunadi Tundu badala ya kutumia eneo takatifu kufanya kampeni.
Huyu mpakwa mafuta alipakwa kwenye masaburi?
 
Back
Top Bottom