Tumkumbushe Mchungaji mtume Mwingira

Elius W Ndabila

JF-Expert Member
Jul 17, 2019
322
645
NIMKUMBUSHE MCHUNGAJI MWINGIRA.

Na Elius Ndabila
0768239284

Wiki hii kumekuwa na video ambayo inazunguka ikimuonyesha Mchungaji Mwingira (mpakwa mafuta) akiwa kanisani akihubiri Waumini wake. Kipande nilichofanikiwa kukiona ni kile ambacho Baba Mchungaji MWINGIRA anahusishanisha upigwaji wa Risasi Lissu na mchakato tunaouendea wa Uchaguzi. "Lisu hajajenga flyover lakini watu wanamfuata" Pastor MWINGIRA.

Kabla sijamkumbusha mambo mengi Baba Mchungaji MWINGIRA, ninaomba nikiri kuwa mimi ni msomaji mzuri wa Vitabu alivyoviandika MTUME MWINGIRA. Vitabu vyake ambavyo nimebahatika kusoma ambavyo vimeandikwa kwa ustadi mkubwa ni TABIA YA KUTEMBEA NA MUNGU UVUNE, MTEMBEO WA MUNGU KWA HAO ALIOWARIDHIA NA MOYO WA KIONGOZI. Ninaomba nikiri pia kuwa ni mmoja ya watu tunaofuatilia magundisho yake na mara nyingi nimebarikiwa nayo sana. Lakini leo ninataka kumkumbusha mambo machache ili kukazia maarifa yake.

Baba Mchungaji (Mtume) MWINGIRA kwenye video yake kwa ufupi amesema Lisu anafaa kuwa Rais kwa kuwa pamoja na kupigwa Risasi nyingi lakini bado anaishi. MWINGIRA anasema kitendo cha Lisu kuendelea kuishi pamoja na risasi alizopigwa ni kusudi la Mungu kuwa anatosha kuwa kiongozi mkubwa wa nchi. Anaendelea kukazia hoja zake kwa kusema Lusu hajajenga Fly Over Kama wengine, lakini bado watu wanamfuata.

Wakati nikiwa ninamsikiliza Mchungaji MWINGIRA rafiki yangu mmoja amenitumia video ya mzee Wasira(Vijana wanamwiti Mwenyekiti wa waliokatwa kwenye mchakato) akisema kuwa kama sifa ya kuwa Rais ni kupigwa risasi, basi watu wengi watatamani wapigwe risasi ili wawe Marais. Hoja ya Mzee Wasira inanipa nguvu na inaongeza wigo wa kufikiria. Kwa mkutadha huo nimkumbushe Mchungaji MWINGIRA kuwa Lisu si mtu wa kwanza kupigwa Risasi nyingi na kuendelea kuishi. Wapo watu wengi ambao Dunia walishapigwa Risasi lakini hawakupata huruma ya kuwa Marais wala hawakuwahi kutamani kuomba hizo nafasi.

Hawakuomba hizo nafasi kwa kuwa walijua fika kuwa sifa ya kuwa Rais si kupigwa risasi bali ni uwezo, uzalendo, ushujaa na uhodari katika kukabiliana na majukumu ya nafasi hiyo. Waliowahi kupigwa risasi na hawakupa nafasi za uongozi ni:- Rapper 50 Cent alipigwa risasi zaidi ya tisa mwaka 2000 hakuomba Urais ila baada ya hapo alitoa albamu tatu.

Mwaka 2006 Joseph Guzman alipigwa risasi 19 hakufa na hakuomba nafasi ya Urais. Pia mwaka 1995 kuna mtu kutoka North Carolina alipigwa vibaya na risasi zaidi 20 hakuomba wala hakuwa Rais. Ninamkumbusha mtume MWINGIRA kwa kuwa ninajua huenda alikuwa hajui na kudhani Lisu ni mtu wa kwanza kupigwa.Hivyo nimtahadharishe Mchungaji kuwa Urais si hisani bali wapiga kura pamoja na kusikiliza sera wanazo haki za kuwapima wagombea na vyama vyao.

Hata hivyo Mchungaji MWINGIRA anafanya makosa, labda kama tu ni shetani ameamua kumtumia Mpakwa mafuta huyu kufikisha matamanio yake. Kanisani si mahali pa kufanyia siasa, ninatamani MWINGIRA atoke kanisani kama walivyotoka akina Bagoza, Gwajima n.ksi mahali pa kufanyia siasa, ninatamani MWINGIRA atoke kanisani kama walivyotoka akina Bagoza, Gwajima kupanda majukwaani. Kanisani ibaki ni sehemu ya kuabudia isiwe sehemu ya kufanyia kampeni.

Neno la Mungu ndilo chakula cha roho ambacho mtumishi wa Mungu anapaswa kuwapa watu kwa wakati wake. Ili uweze kulisha watu ipasavyo ni lazima kuelewa mahitaji yao na wakati sahihi unaofaa kuwalisha.

Mahubiri sahihi ni yale ambayo Yesu Kristo ni sehemu ya mahubiri hayo kwa lengo la kuokoa roho za watu, ndivyo walivyo hubiri mitume wote kwenye Biblia Takatifu. Lakini anapotokea Mchungaji anahubiri siasa ambazo si sehemu ya maandiko matakatifu ni kulifanya hekalu la Bwana kuwa pango la SHETANI.

Lakini hata hivyo si dhambi kwa wapakwa mafuta wa Mungu kufanya siasa, lakini ni DHAMBI kubwa kutumia nyumba ya Ibada kufanya siasa. Kuwa na aina hii ya watumishi wanaoweza kutumia nyumba za Ibada ni sawa na kugeuza hekalu la Mungu kuwa kijiwe cha wahuni.

Makanisa na misikiti toka zamani hayakuwa na milengo ya kisiasa, lakni kadri siku zinavyozidi kwenda ninaona tunaanza kuingiza siasa. Kwa kauli ya Mtume MWINGIRA watu wasio na mlengo wa kumchagua Lisu hawapaswi kuwa waumini wa kanisa hilo. Ushauri wangu ni kuwa MWINGIRA apande Majukwaani kumunadi Tundu badala ya kutumia eneo takatifu kufanya kampeni.
 
Alichofanya ni kuwaambia waumini wake maono aliyopewa. Kosa liko wapi hapo?

Lissu angeenda pale kisha akaanza kujinadi hapo ingekuwa kosa, lkn mbali na hapo unatupigia kelele tuu.

Mbona jeipiemu kapanda madhabahuni miaka 5 kujinadi lkn hukuona tatizo? Ama ndio mkuki kwa nguruwe, kwa binadamu mchungu?
 
Makanisa na misikiti toka zamani hayakuwa na milengo ya kisiasa, lakni kadri siku zinavyozidi kwenda ninaona tunaanza kuingiza siasa. Kwa kauli ya Mtume MWINGIRA watu wasio na mlengo wa kumchagua Lisu hawapaswi kuwa waumini wa kanisa hilo. Ushauri wangu ni kuwa MWINGIRA apande Majukwaani kumunadi Tundu badala ya kutumia eneo takatifu kufanya kampeni


Huu ujumbe muhimu sana. Mwambie mwenyekiti na mgombewa wa ccm aache kutumia madhabahu na misikiti kama sehemu ya kupiga siasa. Akiacha natumaini na washindani wake wataacha akiwemo Mwingira
 
Ulizotoa si hoja ni vioja. Ukiwa na akili timamu huwezi kusema sijui 50 cent alipigwa risasi na hakugombea urais, hangetakaje urais wakati destination yake kubwa ni muziki?. Mlimpiga lisasi Lissu ili kuikabili nguvu zake za hoja katika siasa na sio muziki kama unaemtaja 50 cent.

Record zinaonyesha Lissu alishaanza kuwanyanyasa kina Kikwete, Makinda, Mkapa kabla hata hamjamdunga Risasi kama ambavyo Leo tunavyoshuhudia Magufuli anavyodhalilishwa.
 
Mkuu umeandika vizuri tena umesema mtume, mtume ni neno kubwa Sana mkuu ,hivyo sikushauri kupingana na maneno ya MTUME,na zaiidi WASIRA sio mtume,hivyo kumlinganisha WASIRA NA MTUME ni kubisha bila sababu mkuu,WASIRA alisha kosa kibali Cha wananchi nae atulie basi
 
Wiki hii kumekuwa na video ambayo inazunguka ikimuonyesha Mchungaji MWINGIRA (mpakwa mafuta) akiwa kanisani akihubiri Waumini wake. Kipande nilichofanikiwa kukiona ni kile ambacho Baba Mchungaji MWINGIRA anahusishanisha upigwaji wa Risasi Lisu na mchakato tunaouendea wa Uchaguzi. "Lisu hajajenga flyover lakini watu wanamfuata" Pastor MWINGIRA....
Mwaka huu ccm out
 
Mtoa mada rudia kusoma ulichokiri mwenyewe. Hao wamepigwa 20 ndio kiwango cha juu. Lissu amepigwa 38 na 16 zilimpata na kati hizo anaishi nazo mwilin na anatembea nazo. Wewe unadhan ni jambo dogo.Angalia hy clip yote utamwelewa mchungaji.Jitahid upate clip ya dakika 5 sio hizo za chini ya hapo
 
Alichofanya ni kuwaambia waumini wake maono aliyopewa. Kosa liko wapi hapo?

Lissu angeenda pale kisha akaanza kujinadi hapo ingekuwa kosa, lkn mbali na hapo unatupigia kelele tu...
Jamaa yao miaka yote mitano alikuwa ni kama anaishi kwenye madhabahu za kila kanisa huku akisisitiza ''mniombee'' na kujifanya mnyenyekevu kupita hata malaika kumbe ndani ya moyo wake amejaa roho ya uuaji na ukatili. Watokemee mbali Masadukayo wakubwa hawa.
 
Mwigira achukuliwe hatua kali kwa uchochezi
Upi mkuu ,yaani tumefika mahali mtumishi wa mungu kwa Imani yake kuja na maoni yake juu ya taifa lake imekua uchochezi,
Basi mchukulieni hatua hata Yule mchungaji alietabiri juu ya lissu hata kabla ya kutangaza nia ya kugombea yuko mwanza,hacha kabisa maneno Kama aya,maana Mambo Kama aya ndo yamesababisha wananchi kuichukia ccm
 
Elius W Ndabila,
Tangu mwingira kasema ishu ya Lisu basi ujuaji umekuwa ni mwingi sana

Juzi tu hapa askofu gamanywa alisema magufuli ameletwa na mungu Kuja kuokoa Mali za tanzania

Hakuna mtu yoyote amesema anything hata ww ulikaa kimya kabisa kwa kuona Hilo alilosema ni sawa

Hakuna kitu mwingira amekosea coz ni kweli Lisu alipigwa risasi 16 na ni kweli Lisu amepona pia ni kweli watu wanamfata bila kutangazwa kwenye TV yoyote

Ww uoni kama huo ni muujiza?

Tuache kuleta ujuaji mwingi
 
Wiki hii kumekuwa na video ambayo inazunguka ikimuonyesha Mchungaji MWINGIRA (mpakwa mafuta) akiwa kanisani akihubiri Waumini wake. Kipande nilichofanikiwa kukiona ni kile ambacho Baba Mchungaji MWINGIRA anahusishanisha upigwaji wa Risasi Lisu na mchakato tunaouendea wa Uchaguzi. "Lisu hajajenga flyover lakini watu wanamfuata" Pastor MWINGIRA...
Mnaumia sana Mtumishi Mwingira kuwaambia ukweli eeeh?

Limezeni tu,Mungu tu ndani ya Lissu, hamtamuweza Lissu kamwe kwa sababu Mungu keshamfanya mshindi.

Mshauri tu Magufuli aanze kupaki vitu vyake pale Chamwino. Safari ya Chato imewadia 😂😂
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom