Tumkumbuke marehemu bi. Dharura Bint Abdulrahman mwanamama mwana-TANU mpigania uhuru

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,915
30,259
Leo asubuhi nimepokea ujumbe kutoka kwa msomaji wangu mmoja naweka huo ujumbe hapo chini:

‘’Naomba pia fanya utafiti Mkoa wa Tabora, wakati mimi mdogo nilikuwa pale Tabora Mtaa unaitwa Ngoma, kuna nyumba moja walikuwa wanaingia sana kina mama na mabaibui yao ya kizamani, hiyo nyumba mwenyewe alikuwa anaitwa Tatu au Zarula Abdulrahman na alikuwa mwanaharakati sana wa TANU.

Hebu tafiti huyu mama maana simsikii hata jina lake wakati alikuwa anauza kadi za TANU akizificha uvunguni mwa kitanda chake na wakati huo alikuwa ni msichana tu.’’

Nikamjibu kumwambia kuwa Bi. Dharura bint Abdulrahman nimemtaja katika kitabu cha Sykes.

Msomaji wangu huyu akaniandikia tena:

‘’...kiukweli sasa nikwambie huyo Binti Abdulrahman alikuwa shangazi yangu, wakati huo ananilea nilikuwa sijui kitu, ila nilikuwa namuona anachukua zile kadi uvungu wa kitanda na kuandikia watu kwa siri...’’

Sasa hebu tumtafute Bi. Dharura bint Abdulrahmani hapo chini:

‘’Vikundi vya taarab mjini Dar es Salaam na nyimbo zao, vyama vya wanawake wa mjini kama Saniyyat Hubbi, Goodluck, Coronation, Bomba Kusema na vikundi vya lelemama ambavyo vilikuwa na udugu na vikundi vya taarab kama Al-Watan au Egyptian, vilitoa mchango mkubwa sana katika kuwaamsha watu kuiunga mkono TANU.

Waliounganisha na kuviongoza vyama hivi vya wanawake na harakati za kudai uhuru walikuwa Bibi Titi Mohamed na bibi mmoja wa Kimanyema, Hawa binti Maftah. Bibi Hawa binti Maftah, kama kiongozi wa lelemama, alijulikana kwa jina la ‘’Queení.’’

Hakuna hata mtu mmoja Tanganyika nzima, mbali na Nyerere mwenyewe, aliyeweza kuifanya TANU kuwa maarufu kama Bibi Titi Mohamed.

Bi. Hawa Maftah ndiye aliyeiingiza kwa mara ya kwanza nyimbo za lelemama ziimbwe katika mikutano ya TANU kama mbinu ya kuhamasisha wananchi kukipenda chama.

Vyama vya wanawake Nujum ul Azhar, Waridatil Hubb na Egyptian Club vilivyokuwapo mjini Tabora chini ya wanawake kama Nyange binti Chande na Dharura binti Abdulrahman.

Vyama hivi vya akina mama vilisaidia sana kuipa TANU nguvu katika Jimbo la Magharibi. Muziki na ujumbe katika nyimbo zilizotungwa maalum kuinua mioyo ya wanachama wa TANU vilikuwa na athari kubwa, hususani katika wakati ule ambapo serikali ya kikoloni ilimpiga marufuku Nyerere kufanya mikutano ya hadhara.

Ili kuepuka kadhia hiyo TANU ilikuwa ikiandaa taarab na Nyerere alikuwa akikaribishwa kama mgeni wa heshima.

Nyerere alikuwa akisimama kufungua hafla na katika kufanya hivyo alisema maneno machache.

Kwa namna hii ule moto wa kudai uhuru ulibaki ukiwaka. Kwa njia hii Nyerere aliweza kuwasiliana na wananchi.

Halikadhalika kupitia taarab TANU ilikusanya fedha kwa ajili ya harakati. Kulikuwa na wimbo mmoja wa lelemama ambao uligeuzwa kuwa kama ndiyo mwimbo wa Nyerere, mwimbo huu na ulikuwa akiimbiwa yeye tu.

Mwimbo huo ulikuja kuwa maarufu sana kiasi kwamba ulipoimbwa katika mikutano ya TANU watu wote waliimba kwa pamoja.

Mashairi yake yalikuwa kama hivi: ‘’Muheshimiwa nakupenda sana, wallahi sina mwinginewe Insha Allah Mungu yupo, Tanganyika tutajitawala.’’
 
Leo asubuhi nimepokea ujumbe kutoka kwa msomaji wangu mmoja naweka huo ujembe hapo chini:

‘’Naomba pia fanya utafiti Mkoa wa Tabora, wakati mimi mdogo nilikuwa pale Tabora Mtaa unaitwa Ngoma, kuna nyumba moja walikuwa wanaingia sana kina mama na mabaibui yao ya kizamani, hiyo nyumba mwenyewe alikuwa anaitwa Tatu au Zarula Abdulrahman na alikuwa mwanaharakati sana wa TANU.

Hebu tafiti huyu mama maana simsikii hata jina lake wakati alikuwa anauza kadi za TANU akizificha uvunguni mwa kitanda chake na wakati huo alikuwa ni msichana tu.’’

Nikamjibu kumwambia kuwa Bi. Dharura bint Abdulrahman nimemtaja katika kitabu cha Sykes.
Msomaji wangu huyu akaniandikia tena:

‘’...kiukweli sasa nikwambie huyo Binti Abdulrahman alikuwa shangazi yangu, wakati huo ananilea nilikuwa sijui kitu, ila nilikuwa namuona anachukua zile kadi uvungu wa kitanda na kuandikia watu kwa siri...’’

Sasa hebu tumtafute Bi. Dharura bint Abdulrahmani hap chini:

‘’Vikundi vya taarab mjini Dar es Salaam na nyimbo zao, vyama vya wanawake wa mjini kama Saniyyat Hubbi, Goodluck, Coronation, Bomba Kusema na vikundi vya lelemama ambavyo vilikuwa na udugu na vikundi vya taarab kama Al-Watan au Egyptian, vilitoa mchango mkubwa sana katika kuwaamsha watu kuiunga mkono TANU.

Waliounganisha na kuviongoza vyama hivi vya wanawake na harakati za kudai uhuru walikuwa Bibi Titi Mohamed na bibi mmoja wa Kimanyema, Hawa binti Maftah. Bibi Hawa binti Maftah, kama kiongozi wa lelemama, alijulikana kwa jina la ‘’Queení.’’

Hakuna hata mtu mmoja Tanganyika nzima, mbali na Nyerere mwenyewe, aliyeweza kuifanya TANU kuwa maarufu kama Bibi Titi Mohamed.

Bi. Hawa Maftah ndiye aliyeiingiza kwa mara ya kwanza nyimbo za lelemama ziimbwe katika mikutano ya TANU kama mbinu ya kuhamasisha wananchi kukipenda chama.

Vyama vya wanawake Nujum ul Azhar, Waridatil Hubb na Egyptian Club vilivyokuwapo mjini Tabora chini ya wanawake kama Nyange binti Chande na Dharura binti Abdulrahman.

Vyama hivi vya akina mama vilisaidia sana kuipa TANU nguvu katika Jimbo la Magharibi. Muziki na ujumbe katika nyimbo zilizotungwa maalum kuinua mioyo ya wanachama wa TANU vilikuwa na athari kubwa, hususani katika wakati ule ambapo serikali ya kikoloni ilimpiga marufuku Nyerere kufanya mikutano ya hadhara.

Ili kuepuka kadhia hiyo TANU ilikuwa ikiandaa taarab na Nyerere alikuwa akikaribishwa kama mgeni wa heshima.

Nyerere alikuwa akisimama kufungua hafla na katika kufanya hivyo alisema maneno machache.

Kwa namna hii ule moto wa kudai uhuru ulibaki ukiwaka. Kwa njia hii Nyerere aliweza kuwasiliana na wananchi.

Halikadhalika kupitia taarab TANU ilikusanya fedha kwa ajili ya harakati. Kulikuwa na wimbo mmoja wa lelemama ambao uligeuzwa kuwa kama ndiyo mwimbo wa Nyerere, mwimbo huu na ulikuwa akiimbiwa yeye tu.

Mwimbo huo ulikuja kuwa maarufu sana kiasi kwamba ulipoimbwa katika mikutano ya TANU watu wote waliimba kwa pamoja.

Mashairi yake yalikuwa kama hivi: ‘’Muheshimiwa nakupenda sana, wallahi sina mwinginewe Insha Allah Mungu yupo, Tanganyika tutajitawala.’’
Sheikh wangu Mohammed Said una vitu hatari sana Allah Karim akupe umri mrefu tuvune mengi zaidi toka kwako.
 
Sijui ilikuwaje Tabora sio Jiji mpaka leo, wakati ilianza harakati siku nyingi sana
 
Back
Top Bottom