Tumia M-Pesa at your own Risk!

POLE MI KUNA KIPINDI WALINISUMBUA NIKAINGIA TWITTER NIKAWATUNISHIA MISULI WITHIN SECONDS PESA IKARUDI KWENYE SIMU YANGU LAKINI HAPO NILISHAKAA SIKU ALMOST 6 ZA KAZI
Customer care hawana msaada full longo longo. Mbinu uliyotumia niliwahi kuitumia tigo, kwenye akaunti yao ya FB pesa ilirudi baada ya dk kadhaa.
 
M-pesa kesi za wateja wao ni nyingi sana,wanatakiwa wajitathimini au waachane na hiyo huduma ya m-pesa!
 
Kweli kabisa wasumbufu sana, niliambiwa nisubiri baada ya saa 24 pesa itarejeshwa, muda wa saa 24 ukapita bila hata senti kurejeshwa. Nikapiga tena nikaambiwa itarudi baada ya saa 72, muda ukafika hola! Jamaa wasumbufu sana.
 
Kabisa wanakata simu hata mimi imenitokea wamenikatia simu zaidi ya mara mbili. Halafu wako baadhi yao hawana ufahamu wa kazi yao wapo wapo tu.
 
Wanaiba pesa za wateja kuzitumia huku wakizungusha na kusubiri mwingine atoe hiyo pesa ili wakurudishie.. huku huyo mwingine watamzungusha kama wewe..

Ni kitu kinashangaza sana. Kama upo Dar nenda makao yao makuu ukapige kelele hadi kieleweke.
At least huku unaweza kueleweka sio kuleeeee! Yani kule huwa unavuruga hatari [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Kabisa wanakata simu hata mimi imenitokea wamenikatia simu zaidi ya mara mbili. Halafu wako baadhi yao hawana ufahamu wa kazi yao wapo wapo tu.
karibia woote hawaelewi wako hapo kwa kazi ipi hawana majibu sahihi kwa wateja wakati mwingine unaweza kufikiri wale walinzi wa makampuni ndo wanapokea hizi simu
 
Mpesa ilikuwa zamani sio sasa mabraza men na machek sister kibao ofisini ngojeeni maumivu mnaotumia mpesa
 
Hilo ni wazo jema!
Mnishauri mwanasheria wa ku pursue!

Wiki iliyopita nilituma pesa kwa M Pesa, mpokeaji akawa akisubiri notification ya pesa kuingia. Akaamua kucheki salio akakuta pesa imeingia na notification hadi leo hajaipata.

Tukumbuke hii ni teknolojia na saa yeyote inaweza kutofanya kazi kabisa kwa muda fulani au kutegemea na ukubwa wa transaction mambo ya security na verification yanaweza kuchelewesha muamala au notification. Hizi flaws za teknolojia zipo kwenye taasisi za fedha, ila sio lazima zitokee na zinaweza kuzuilika.

Hivyo kabla ya lawsuit, ni vema kujua chanzo cha tatizo ili kujiridhisha kama sababu ni wizi, uzembe au ajali ya kiteknik.
 
Hizo ni hasira tu mkuu. Hapana shaka umekua ukitumia huduma ya mpesa kwa muda ss matatizo madogo ya kimtandao ndo yakupe uhakali wa kutoa matamshi hayo? Nonsense!

Ninajua jamaa wana utaratibu na hela yako haipotei. Kumbuka kuna systems na wanadamu na vyote haviko 100% ktk utendaji japo ni jukumu lao kuhakikisha mteja anapata huduma bora. Mfano mm tangu nimejiunga na huduma za vodacom nikiwa chuoni 2004 sijawahi juta nimesgatumia pia tigoline yaani hakuna ambako hakuna changamoto hilo uelewe. Kama haikukupata ww basi mwingine. Na hizo changamoto ndizo zinawafanya wazidi kuboresha huduma.

Hv umewahi kujiuliza mchango wa moesa kwenye uchumi wa nchi? Unajua mpesa inazungusha hela ngapi kwa siku? Unajua kuwa kuna usimamizi mkali toka benki kuu kwenye hizi huduma za kifedha au unadhani ni holela?

Kibinadamu najua uliumia kwa kutopata huduma in real time lkn haifai kutoa matamshi hayo. Mpesa ina zaidi ya watumiaji mil6 Tz. Je ukijisema ww pekeyako unajua ni % ngapi ya watumiaji?
 
Ni wakati wa Watanzania kuyashitaki haya makampuni yanapotokea matatizo kama haya maana wametuzoea mno hawa watu..
Yani Nataka issue kama hii inikute waone na huy umasikini unaotutawali naona Ni wakati wankutumia taalima kutajirika...kama vip Mzee niuzie hiyo Kesi tutakula nusu kwa nusu!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…