Tumia M-Pesa at your own Risk!

Tumia M-Pesa at your own Risk!

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2014
Posts
17,551
Reaction score
28,508
Nimelazimika kulalamika katika mtandao huu wa JF maana naona M-Pesa sasa hivi ni very risky.

Jana nimemtumia mtu pesa kwa M Pesa akiwa dukani(pharmacy) ili anunue madawa muhimu sana kwa mgonjwa. Jamaa dawa kazipata zote na zilikuwa na gharama kubwa. Nikatuma hela kwa M-Pesa immediately.

Baada ya nusu saa meseji hajapata kuwa pesa imeingia kwake. Nikawapigia M Pesa kwa huduma ya jamii, namba 100. Jibu standard, tunatuma ujumbe mwingine.
Baada ya nusu saa tena meseji ya kutoa hela haijaenda.

Nikapiga tena no 100 huduma kwa wateja, jibu bado standard, tutatuma meseji tena. Baada ya masaa mawili bado meseji ya kuchukua fedha haijaenda, nikawapigia MARA YA TATU! Jamaa wa Voda M-Pesa wananiambia , tutatuma meseji tena, tukusaidie tatizo jingine?

I blew my top.
Nikawaambia -Rudisheni hela yangu immediately, kama mmeshindwa kutuma. Jamaa wa M Pesa anajibu, itabidi usubiri within 24hrs!

Leo napiga no 100 huduma kwa wateja , wananijibu, inabidi usubiri siku nne kurudishiwa pesa!!
Mgonjwa wangu kue yuko hoi bin taaban.
Ilibidi nipeleke fedha physically maana hali ilikuwa tete.

USE VODACOM M-PESA A YOUR OWN RISK!!
Mimi najitoa.

UPDATE:

Sasa tuone MAAJABU
Nimepata message hii sasa hivi saa 8.04 mchana huu.

Hii ni baada ya kuwapigia simu no 100 (huduma kwa wateja) mara kadhaa, sasa hivi wamenitumia ujumbe(sionyeshi no za utambulisho)

"4JU******* Imethibitishwa, muamalawa kurudisha shughuli 4JU******* umefaulu na pesa kurudishwa mnamo 30/10/17 saa 4.41PM na sh570,000.00 zimeingizwa kwa akauni yako ya M-Pesa Baki yako mpya ya M-Pesa ni 610,000.00"

Message hii nimeipata saa 8.04mchana!!

Please note: time 4.41PM!!!! time ambayo haipo, hivyo si kompyua inayofanya input, ni mtu aliyepanic!
Conclusion: Ni kweli kabisa kuna employees wanachezea accounts za wateja .

VODA M-PESA SI MAHALI SALAMA
 
Nimelazimika kulalamika katika mtandao huu wa JF maana nana M-Pesa sasa hivi ni very risky.

Jana nimemtumia mtu pesa kwa M Pesa akiwa dukani ili anunue madawa muhimu sana kwa mgonjwa.
Jama dawa kazipata zote na zilikuwa na gharama kubwa.
Nikatuma hela kwa M-Pesa immediately.
Baada ya nusu saa meseji ajapata kuwa pesa imeingia kwake.
Nikawapigia M Pesa kwa huduma ya jamoo, namba 100.
Jibu standard, tunatuma ujumbe mwingine.
Baada ya nusu saa tena meseji haijaenda.
Nikapiga tena no 100 huduma kwa wateja, jibu bado standard, tutatuma meseji tena.
Baada ya masaa mawili bado meseji y kuchukua fedha haijaenda, nikawapigia MARA YA TATU!
Jamaa wa Voda M-Pesa wananiambia , tatuma meseji tena, tukusaidie tatizo jingine?

I blew my top.
Rudisheni hela yangu immediately, kama mmeshindwa kutuma.
Jamaa wa M Pesa , itabidi usubiri withi 24hrs!

Leo napiga no 100 huduma kwa wateja , wananijibu, inabidi usubiri siku nne kurudishiwa pesa!!
Mgonjwa wangu kue yuko hoi bin taaban.

USE VODACOM M-PESA A YOUR OWN RISK!!
Mimi najitoa.
POLE MI KUNA KIPINDI WALINISUMBUA NIKAINGIA TWITTER NIKAWATUNISHIA MISULI WITHIN SECONDS PESA IKARUDI KWENYE SIMU YANGU LAKINI HAPO NILISHAKAA SIKU ALMOST 6 ZA KAZI
 
Ukiwa unaongea nao wao wanaona ni simple tu na wanakujibu simple tu kuwa kuna matatizo ya mtandao pesa yako itarudishwa baada ya masaa 72.Ila kiukweli ni kwamba kat ya wale macustomer care tunaoongea nao kuna mtu wenye uwezo wa kufanyia kazi tatizo husika na kuna wale wenzangu na Mimi.Fika vodashop iliyo karibu nao huku ukiendelea kufanya mazoezi ya kuwapigia simu kila wakat
ukiambiwa usubiri na ukasubiri kweli itafika tar 10 mwez ujao.Wasumbue sn upate pesa yako
 
Ni wakati wa Watanzania kuyashitaki haya makampuni yanapotokea matatizo kama haya maana wametuzoea mno hawa watu..

Washtakiwe kwa nani? Hawayaoni hayo matatizo? Unapiga simu Huduma kwa wateja basi kwanza full matangazo, kisha wanakutajia huduma. Mfano Halotel Inachukua hadi nusu saa mpaka saa 1 kuweza kupata kuwasiliana na huduma kwa wateja, choices zao hazipo clear, unaguess tu. Tigo nao ndo mashaka ya roho, ukibonyeza namba ya kuwasiliana na mhudumu tu apo apo unaambiwa asante kwa kupiga tigo simu inajikata.

Transactions zao hazipo instant, magumashi matupu. Halotel unatia vocha kujiunga kifurushi mara unaambiwa salio halitoshi, hapo ulikuwa ushazima Data na hujapiga wala kutuma sms. Ukibahatika kuwapigia huduma kwa wateja wanakwambia umetuma sms kwenda na namba ya international, hii ilishantokea mara 2, na wamekataa kunambia namba ipi, wanasema niende ofisini kwao.

Kwa kifupi, TCRA haina mashuhulikiaji kwenye hii mitandao, inajifanyia inavotaka tu na si kwamba labda hawajui wanajua vizuri tu.
 
Washtakiwe kwa nani? Hawayaoni hayo matatizo? Unapiga simu Huduma kwa wateja basi kwanza full matangazo, kisha wanakutajia huduma. Mfano Halotel Inachukua hadi nusu saa mpaka saa 1 kuweza kupata kuwasiliana na huduma kwa wateja, choices zao hazipo clear, unaguess tu. Tigo nao ndo mashaka ya roho, ukibonyeza namba ya kuwasiliana na mhudumu tu apo apo unaambiwa asante kwa kupiga tigo simu inajikata.

Transactions zao hazipo instant, magumashi matupu. Halotel unatia vocha kujiunga kifurushi mara unaambiwa salio halitoshi, hapo ulikuwa ushazima Data na hujapiga wala kutuma sms. Ukibahatika kuwapigia huduma kwa wateja wanakwambia umetuma sms kwenda na namba ya international, hii ilishantokea mara 2, na wamekataa kunambia namba ipi, wanasema niende ofisini kwao.

Kwa kifupi, TCRA haina mashuhulikiaji kwenye hii mitandao, inajifanyia inavotaka tu na si kwamba labda hawajui wanajua vizuri tu.
TCRA wanashindwa kuwajibika, watu wanapoteza au kucheleweshewa amana zao, wao wamefumba macho.
 
Kutumia mitandao ya simu kwa ajili ya ktuma pesa yahutaji moyo unaweza ukawa na shida na usipate wakala sana sana usiku
 
Hapa nilipo natamani kupiga mtu yeyote wa Voda!
HEE MKUU TULIZA JAZBA HUWA WANAUDHI MI NILIGHAFILIKA SANA KWAKWELI NIKAWAPA MAKAVU LIVE KULE TWITTER WAKARUDISHA PESA ZANGU NA NILIANZISHA THREAD YA KUKAMPENIA WATU WASITUMIE MPESA HAHAHAHA WAKARUDISHA MAANA NILISHINDWA KABISA KUWAVUMILIA HALAF CUSTOMER CARE WANAKUJIBU KAMA WAPIGA RAMLI CHONGANISHI MAANA HATA HAWAELEWI ...A WALA B
UKIZIDISHA MASWALI WANAKUKATIA SIMU
 
Mimi tarehe 25/10/2016 nilituma 30,000/ mgonjwa alikuwa Kairuki, tena case sentive kweli, hadI leo haijafika. Ikifika SAA 11:00 jioni sijaona naweka transaction detail humu! Voda rekebisheni bana, mnabore!
 
Wanaiba pesa za wateja kuzitumia huku wakizungusha na kusubiri mwingine atoe hiyo pesa ili wakurudishie.. huku huyo mwingine watamzungusha kama wewe..

Ni kitu kinashangaza sana. Kama upo Dar nenda makao yao makuu ukapige kelele hadi kieleweke.
 
Back
Top Bottom