Tumia hizi 48 Laws of power kwenye bishara yako part 2

Tumia hizi 48 Laws of power kwenye bishara yako part 2

youngkato

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2014
Posts
3,638
Reaction score
3,641

Tumia hizi 48 laws of power katika biashara yako part 2.png

13. Ask for help based on mutual gain.​

Huwa tunasema, ukitaka msaada toa msaada kwanza. Mfano mwenzako anauza vitamba ila ni fundi cherehani, mwambie utakuwa unanunua vitambaa kwake na yeye wakija wateja awe anawaelekeza kushona kwako.

Au kwa kuingia patnership ya kugawana wateja, Nakutangaza kwa wateja wangu na wewe unanitangaza kwa wateja wako). wote mnafaidi ila aliyeko chini anafaidi zaidi.

14. Observe your competitors like a quiet spy. (Pose as a friend, work as a spy)​

Jifunze mbinu za washindani wako au wafanyabiashara wenzako, angalia matangazo yao, njia wanazotumia kupata wateja, strategy zao. Jifanye rafiki yao, waibie njia zao.

15. Crush your enemy totally.​

Hakunaga urafiki kwenye biashara, ukiona mtu analeta mazoea kwenye biashara yako mpige chini, ukipata namna ya kumpoteza mpinzani wako mmalize kabisa mpoteze kwenye rmani.

Kwenye biashara hakuna urafiki wa kudumu (Mfanyakazi akizingua ondoa, mteja kikupotezea muda msubirie mwingine, mshindni wako akiingia kwenye anga zako muondoe kabisa.

16. Don’t overpost or oversell; let people miss your presence.​

Hii tunasema wateja wasikuzoee sana, usiwe mtu yuleyule kila siku, usikalilike. ndo maana huwa tunatengeneza offer, tunafanya rebranding, tunapandisha bei.

Hii tunafanya ili kupunguza mazoea kwa wateja wakatuona walewale kila siku

17. Be unpredictable.​

Mteja asijue moves zako, asijue unakaribia kutoa mzigo gani, asijue offer gani inakuja. Kila kitu kifanyike kwa suprise.

Hii inasaidia kuongeza ubunifu kwenye biashara yako.

18. Don’t isolate (isolation is dangerous)​

Jichanganye na wafanya biashara wwenzako ili kujua siri za biashara, hii inakusaidia kupewa taarifa mapema ikitoke tatizo lolote au ikitokea mtu kavamia soko lenu.

Dominate the market lakini usijitenge na wenzako

19. Know who you’re dealing with (Know your buyer before you pitch)​

Muelewe mteja wako kabla hujaanza kumuuzia, (Kuna wateja wenye hela, wateja hawana hela, wateja hawahui wanataka nini) Msikilize kwanza kabla hujaongea sana ili ujue huyo ni mteja wa aina gani.

20. Stay neutral in public​

Mfanya biashara unatakiwauangalie waoi kwenye faida. Kama ni ccm kuna tenda nenda, kama kuna tenda CHADEMA nenda, kama kuna tenda SIMBA au YANGA nenda.

Au usilete ubaguzi kwenye matangazo yako, hakikisha haujulikani wewe uko upand upi.

21. Play dumb to learn more in negotiations.​

Unapokuwa unaongea na mteja wako jifanye mjinga, usiwe mjuaji sana. Msikilize, muulize maswali, mfanye ajione yupo sawa hata kama anaongea ujinga.

Huwa nikiwa kwenye consultation na wateja wangu wengi wanataka ufanye wanachokiamini wao, kwahiyo huwa nakubaliana nao lakini naongezea ninachotaka kukifanya mimi kwenye mawazo yao.

22. Lose small to win big​

Kwenye mbinu za kupata wateja unatakiwa kuingia gharama kidogo ili upate wateja wakubwa. Mfano ndo unaanza leo huna shuhuda zozote au wateja ila unauza kwa bei kubwa. lazima uanze kwa bei ndogo ili kukusanya shuhuda na trust.

Mfano kuna mteja wangu ailwekeza $20 kwenye matangazo, ikamletea wateja wengi sana wa kumlipa zaidi ya 1M profit.

Kwahiyo kubali kuwekeza upate faida badaae.

23. Focus all efforts on one clear offer at a time.​

Huwa nawaambia wafanyabiashara wengi, anza na product moja kwanza iweke sokoni ipate jina ndo uendelee na nyingine.

Au anza na biashara moja kwanza ikishasimama ndo unaweza kufanya biashara nyingine.

24. Learn business etiquette, it closes high-end deals.​

kama mfanyabiashara lazima ujifunze skills nyingine za kukusaidia kupata wateja n kuuza.

Mfano skills za kuuza, kuandika copy, kurusha matangazo, kuongea na wateja, project management.

Ni skills nyepesi sana lakini zinakusaidia sana kwenye kuongeza sales.

25. Itaendeleaa​


Tumefanya biashara nyingi kukua kwa kutumia hizi sheria 48 za kukuza biashara yako tutakusaidia kufanya hivyo kwa kukuletea wateja, kuktangazia na kufanya branding kwenye biashara yako pamoja na kukufundisha mbinu za kuongeza wateja kwa kutumia hizi sheria 48. Tutafute whatsapp wa.me/+255693880325
 

Attachments

  • Tumia hizi 48 laws of power katika biashara yako part 3.png
    Tumia hizi 48 laws of power katika biashara yako part 3.png
    2.8 MB · Views: 27
24 ni ya kuwa nayo makini kwakuwa unaweza jikuta unajiexpose kwa TRA na uwe tayari kukubaliana nao
 
Kwenye hizo laws zenu, kuna mojawapo ya kuzuia chuma ulete, kijicho na husuda?
 
Back
Top Bottom