Tumia akili 2022 utafanikiwa

Song of Solomon

JF-Expert Member
Aug 5, 2021
2,733
5,490
Niliwahi kusoma kisa kimoja cha kijana aliyekamatwa na Polisi kwa kosa la uzururaji. Alipofikishwa kituo cha polisi alitakiwa atoe cho chote (hongo) ili aachiwe, yule kijana alikataa.

Kesho yake alipofikishwa mahakamani, yule kijana alisomewa shitaka tofauti, lilikuwa kuendesha baiskeli isiyokuwa na taa na kuhatarisha maisha ! Akakiri kosa na kupigwa faini shilingi elfu ishirini. Akalipa faini na badae akaenda kituoni kudai baiskeli yake.

Pale kituoni Mkuu wa kituo alimuita askari aliemkamata na kumfungulia mashtaka ili ampe baiskeli yake, askari akakiri kumkamata yule kijana ila akamuomba mkuu wa kituo aongee na yule kijana pembeni. Askari akamlaumu yule kijana kwa nini anataka kumharibia kazi? Kijana nae akakomaa na kudai apewe baiskeli aliyokamatwa nayo. Huku na huku, ikabidi yule askari akatafute pesa na kununua baiskeli mpya ya kumlipa yule kijana.

Yule kijana alipokabidhiwa baiskeli mpya akafungua taa na kumkabidhi askari. Akamwambia "baiskeli haikuwa na taa". Jitahidi kutenda haki bila kujali hali ya unaemtendea haki.
 
kwani waliofanikiwa 2021 kurudi nyuma hawakutumia akili bro?
 
Niliifungua kwa tashwishwi mada yako, nilichoambulia ndani sasa hahahahahah
 
Kama walimsingizia kuendesha baiskeli bila taa kwanini washindwe kusema baiskeli yake kapewa tayari wakati hajapewa
 
Back
Top Bottom