Kuna la kujifunza kwenye mkasa wa Askari, Kijana na Baisikeli

Ushimen

JF-Expert Member
Oct 24, 2012
37,208
85,315
Kijana mmoja alikamatwa kwa kosa la uzururaji. Alipofikishwa kituo cha polisi alitakiwa atoe chochote ili aachiwe, yule kijana akagoma.
Kesho yake akapandishwa mahakamani, na kusomewa shitaka la kuendesha baiskeli isiyokuwa na taa. Akastaajabu iweje akamatwe kwa kosa jingine na mahakamani asomewe kosa jingine? Halafu katika maisha yake hakuwahi kumiliki baiskeli.

Lakini hakuwa na la kufanya. Akakiri kosa na kupigwa faini ya shilingi elfu mbili. Akalipa faini na badae akaenda kituoni kudai baiskeli yake.
Mkuu wa kituo alimuita askari aliyemkamata na kuagiza amrudishie baiskeli yake maana ameshalipa faini mahakamani. Askari akamuomba aongee na yule kijana pembeni. Waliposogea pembeni akamlaumu kwa nini anataka kumharibia kazi? Akamwambia unajua sikukukamata na baiskeli, sasa unadai nini?

Kijana akakomaa na kudai apewe baiskeli yake ambayo Polisi walisema wamemkamata nayo. Ili kulinda kibarua chake ikabidi yule askari atafute pesa na kununua baiskeli mpya ya kumlipa yule kijana.

Yule kijana alipokabidhiwa baiskeli mpya akafungua taa na kumkabidhi yule askari. Akamwambia "Afande baiskeli haikuwa na taa". Akapiga pedo na kuondoka zake.
 
Back
Top Bottom