Lowasa hastahili kuwa raisi japo anajua na ni jasiri kuongoza hii inatokana na kupenda kwake visa na visasi kitendo cha kumfanya vile mwakyembe sidhani iwapo atakua rais mbeya itaendelea kuwa sehemu ya Tanzania!!!Alafu atamshinda nani maana anaogopwa kama ukoma labda apindue nchiKwenye mijadala 100 ya kwenye jukwaa hili amini usiamini mijadala 98 ndani yake halikosi kutajwa jina la Edward Lowassa kwa mema, mabaya kwa kuungwa mkono au kwa kupingwa. Lowassa imethibitika kuwa ndiye nguzo ya siasa zetu hapa Tanzania. Ukimshambulia au kumsifia Lowassa ni lazima utavuta hisia (attention) za jamii ziwe chanya au hasi dhidi yako.
Leo hii Lowassa akiacha siasa kitakachofuatia ni mjadala mwingine kama aachwe apumzike au ashitakiwe. Ndani ya CCM makundi yanayotajwa ni ama wanaomuunga mkono Lowassa au wanaompinga, na nje ya CCM mwanasiasa anayetajwa kama atashindwa kirahisi au atawashinda wapinzani wake ni Lowassa. Inavyoonekana kwenye siasa za Tanzania kumuepuka Lowassa haiwezekani.
Lakini kama taifa tunatakiwa tutoke kwenye mkwamo huu wa jinamizi la Lowassa, kwani kwa hali ilivyo sasa inaonekana kama vile Lowassa ni "Control Machine" ya maisha yetu ya kisiasa. Tuamue kushughulika na Lowassa leo na milele (once for all) ili tubakie na kazi ya kuijenga nchi yetu.
Haiwezekani ionekane kama kwa nchi nzima Lowassa anao uwezo wa kufanya chochote halafu sisi kama taifa tunabaki kumwangalia, kulalamika na kuwayawaya kama swala aliyekoswakoswa na simba. Kama analimiki bunge, mahakama, Serikali na chama chake basi asitumiliki na tusiofaidika na mfumo aliouweka.
Kama hatuna cha kumfanya Lowassa basi tujue huko tuendako kama taifa hatuna heri hata kidogo!!
EPA,richmond na zingine zote ilikua kwa kazi ya uchaguzi, hakula lowasa. Amebeba mzigo kwa makubaliano.
angeeleza hayo maPema ningemwelewa.though sijawahi kufikiria akiLini mwangu kuwa lowasa sio mwizi toka niielewe kauli ya mwlm jknepa,richmond na zingine zote ilikua kwa kazi ya uchaguzi, hakula lowasa. Amebeba mzigo kwa makubaliano.
Kwenye mijadala 100 ya kwenye jukwaa hili amini usiamini mijadala 98 ndani yake halikosi kutajwa jina la Edward Lowassa kwa mema, mabaya kwa kuungwa mkono au kwa kupingwa. Lowassa imethibitika kuwa ndiye nguzo ya siasa zetu hapa Tanzania. Ukimshambulia au kumsifia Lowassa ni lazima utavuta hisia (attention) za jamii ziwe chanya au hasi dhidi yako.
Leo hii Lowassa akiacha siasa kitakachofuatia ni mjadala mwingine kama aachwe apumzike au ashitakiwe. Ndani ya CCM makundi yanayotajwa ni ama wanaomuunga mkono Lowassa au wanaompinga, na nje ya CCM mwanasiasa anayetajwa kama atashindwa kirahisi au atawashinda wapinzani wake ni Lowassa. Inavyoonekana kwenye siasa za Tanzania kumuepuka Lowassa haiwezekani.
Lakini kama taifa tunatakiwa tutoke kwenye mkwamo huu wa jinamizi la Lowassa, kwani kwa hali ilivyo sasa inaonekana kama vile Lowassa ni "Control Machine" ya maisha yetu ya kisiasa. Tuamue kushughulika na Lowassa leo na milele (once for all) ili tubakie na kazi ya kuijenga nchi yetu.
Haiwezekani ionekane kama kwa nchi nzima Lowassa anao uwezo wa kufanya chochote halafu sisi kama taifa tunabaki kumwangalia, kulalamika na kuwayawaya kama swala aliyekoswakoswa na simba. Kama analimiki bunge, mahakama, Serikali na chama chake basi asitumiliki na tusiofaidika na mfumo aliouweka.
Kama hatuna cha kumfanya Lowassa basi tujue huko tuendako kama taifa hatuna heri hata kidogo!!
Anyongwe!
Nashauri kama kweli anautaka uraisi aende kwenye media atangaze JK alihusikaje kwenye EPA na Richmond na jinsi alivyotumika,aeleze dhamira yake kuwa ni safi
Lowassa anapaswa kujiulaumu kwa kutooana mbali kiasi cha kujiruhusu kutumiwa na Kikwete. Lowassa kweli ana madoa tangu enzi za Mwalimu, lakini hili la kutumika kama nepi ya kusafisha uchafu wa Kikwete itamgharimu maisha yake yote. Kugombea urais japo ni haki ya kikatiba ya kila mtanzania, hili Lowassa asahau. Anaweza kulazimisha chama chake kumteua ili kishindwe vizuri ingawa anaamini kuwa pesa aliyochuma kwenye ufisadi inaweza kumletea ushindi kama mshirika wake Kikwete alivyotumia pesa ya EPA. Wakati umebadilika. Ni mihumu kulielewa hili hata kama hakubaliani nalo.
Mtu haadhibiwi kwa ushahidi wa kufikirika.
Kuna watu wameshikwa kwa ushahidi ulio timilifu na wanapeta...Chenge amekamatwa na mabilioni ya wizi benki. Tungekua na nia dhabiti ya kupinga ufisadi tuanzie hapo tulipo na ushahidi wa kutosha.
Lowasa angekua fisadi angeomba rushwa CityWater ili waendelee na mkataba wao.