Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 39,997
Tatizo la Viapo: Mojawapo ya mambo ambayo yamenitibua sana na yanaendelea kunitibua hili la watu kula viapo kwa ajili ya kupata kazi tu lakini si kwa ajili ya kuvisimamia! Wote tumewasikia wakila kiapo tena mbele ya hadhara na wanasema kabisa kwa majina yao na mbele ya Mungu wao tena wakiwa na macho meupe kabisa, sauti za upole na zenye kusikika (ili walioko nyumbani warekodi vizuri) kuwa wanaapa "kuilinda, kuihifadhi na kuitetea" Katiba za vyama vyao.
Samahani wanaapa kutetea misimamu ya vitabu vyao vya dini walivyoshikilia; au marafiki na ndugu zao! Hapana, wanaapa kuilinda, kuitetea na kuhifadhi Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tumewasikia na tena siyo kwa jumla (maana wengine wangeweza kumung'unya maneno) bali mmoja mmoja tena wakiitwa mbele. Tumewasikia.
Tatizo wanajua uzito wa kiapo hicho? Na je wanamaanisha? Fikiria kwa mfano, watu wanaapa kuhusu hiyo hiyo Katiba halafu wanaanza hapo hapo kuipuuzia! Hawakuapa kuvikubali na kuvilinda vipengele vya Katiba wanavyovipenda; au vile ambavyo vimewafanya wawe wabunge na nafasi zao; wameapa kulinda Katiba yote!
Nina uhakika wa kutosha tu (kwani historia ni mwalimu mzuri) watu hawa hawa ambao tumewaona wakiapa kuilinda, kuitetea na kuihifadhi Katiba Hii hii watakuwa wa kwanza kujaribu kuivunja kama walivyofanya katika Bunge lililopita ambapo walijaribu kuifuta bila kuwa na mamlaka kufanya hivyo (kitu ambacho binafsi naamini ilikuwa ni uhalifu mkubwa - high crimes). Unaweza vipi kutaka kufuta Katiba ambayo uliapa kuihifadhi na bado ukabakia na uhalali wa kuwa huko Bungeni?
Ugomvi wetu mkubwa katika miaka hii mitano ijayo ya Bunge hili la 11 ni jinsi gani itabidi tuwakatalie na kuwakumbusha ndugu zetu hawa juu ya kiapo chao hiki; kwamba kina matokeo. Na kama wanaona hawakubaliani sana na hii Katiba - ni lazima wajiuzulu! Pamoja na ubovu wake wote leo tumewaona wameapa kuitetea, kuihifadhi na kuilinda.
Sasa wasipoitetea, kuihifadhi au kuilinda nani mwingine afanye hivyo? Sisi wengine tunaweza kusema vyovyote juu ya Katiba hii hatufungwi na viapo hivi; wao wenzetu hawawezi. Wamejifunga.
Isipokuwa kama walikuwa wanatupigisha porojo tu!
MMM