Tumetoka mbali.............

Tumetoka mbali.............

EJM_

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2011
Posts
3,836
Reaction score
2,119
Leo wakati najiandaa kwenda kibaruani kwangu nikakumbuka vitu vingi vilivyowahi kupita katika maisha yangu na its a nice memory asee;

Brands kama hizi;
Bodyline/Vaseline - Haya ndio yalikuwa mafuta maarufu home na kopo kubwa kabisa lilikuwa linakaa kwenye kiukuta cha sitting room au juu ya kabati for all to access kabla ya kwenda shule.

Top Society - Hii ilikuwa lotion ya kwanza mimi kutumia tena nilikuwa namuibia uncle wangu home najitundika mwenyewe na siku hiyo lazima shule watu wajue nimejipaka something different.

Cobra - Sina uhakika sana kama hii ilikuwa perfume au spray all in all mi nakumbuka ndio ilikuwa ya kwanza mi kuitumia kama perfume (Hivi bado ipo kweli?)

Dear Heart - Hii ilikuwa brand maarufu kwa watoto wa kike (Mwisho na house girl wetu nilimuona anayo)

Losso/DH - Hizi ziliwahi kuwa brand maarufu sana kwa wanafunzi hasa wa shule za msingi (enzi zetu hatukuwa na restriction ya aina wala rangi ya viatu) Nakumbuka watu walivipachika viatu vyenye nembo ya DH kama "Dingi Hana) Baadaye zikaja nyingine zilizokuwa na majina ya wachezaji wa enzi hizo kama Mogella, Kizota, Lunyamila na kadhalika. Losso was for girls anyway.

Enzi hizo hakukuwa na hizi shule za "Wazungu" zaidi ya IST (Kwa wale tuliokuwa Dar sina uhakika na mikoa mingine na huku shule za sekondari maarufu zikiwa Mzizima na Shaaban Robert. Nakumbuka Tambaza ya enzi zile iliwahi kufanya tukafunga shule kwa muda baada ya kuanzisha varangati ikabidi tufunge kashule ketu kwa siku hiyo mbio kwenda nyumbani.

Nakumbuka mwalimu mmoja jina lake lilijaa karibu kuta zote za majengo yaliyokuwa jirani na shule yetu na yote yalikuwa matusi na ahadi za kumdunda. Ah kabla sijasahau shule yetu ilikuwa na walimu wa kiume watatu tu kati ya jumla ya walimu 30 so wakajitafutia ka ofisi kao chini ya mkorosho.

Nakumbuka niliwahi kuwa kwenye ngonjera ya kuwaaga darasa la saba na cha kukumbukwa hapo ni kwamba ITV enzi hizo ndio imeanza tu walikuja kurecord (Nakumbuka dada mmoja alikuwa anaitwa Tumaini Meshack) ndio alikuwa presenter wa kipindi cha watoto enzi hizo.

Kibaya zaidi nakumbuka niliwahi kuongoza kwenye kura za "Nani anatoka na nani" Nilinusurika adhabu kwasababu mwalimu aliyekuwa anaendesha zoezi alikuwa anatufundisha hesabu na nilikuwa nafanya vizuri sana somo lake so akawa mshikaji wangu.

Dah nimetoka mbali..........................
 
Back
Top Bottom