Tumetoka mbali hasa tulianza shule miaka ya 1970s!

Duh! Ee bana ee! Afadhali umeamua kutuondoa kwenye mambo ya sihasa angalau kwa muda!
Mimi ilinitokea nimeandika barua (nikiwa standard six nakumbuka) kwenda kwa mdada mmoja wa standard five! Niliiandika usiku, si nikaisahau chini ya mto! Nikiwa shuleni nikawa nafikiria jinsi mama atakavyoingia chumbani kufanya usafi! Unajua ndivyo ilivyotokea!! Ile kurudi home mchana naangalia chini ya mto barua haipo (kumbuka kitanda kimetandikwa pia)!! Nikajua leo (siku hiyo) nimekwisha! Mshua kurudi, maza anamuonyesha barua! Dingi hakulaza damu, kaniita na kunitaka niisome mbele ya familia (wadogo zangu 3 wakubwa zangu 3 pembeni baba na mama) Kwa kweli kilichofuatia ni kipondo! Dingi yangu alikuwa anatembeza mkono mwanzo mwisho!!! Those days bana!!!

:laugh::laugh::laugh::laugh::laugh:You just made my day ulisulubiwa mbele ya wadogo na wakubwa zako wote wakicheki mkanda live
 
Tumetoka mbali hasa tulianza shule miaka ya 1970s!

Enzi zetu barua kama hii ilikuwa ukishaiandika, unatafuta nafasi ya umdhamiliae awe peke yake ili uweze kumkabidhi, kwa hiyo waweza kukaa nayo kwenye mfuko wa madaftari hata week nzima.

Na je utampatiaje hiyo barua?
Akishakuwa peke unachokifanya ni kumrushia usoni, halafu huyoo…unatimua mbio. Ukifika mbele kidogo unachungulia kama anaisoma.

Utajuaje kama amekukubali?
Ukiona anasoma halafu anatabasamu, ujue tayari .

Zawadi gani dada zetu walipendelea zaidi?
Ni kumnunulia mafuta ya Lady Gay au Yolanda (kama uko safi) au kandambili , hapo atakuona kweli unamjali.

Na je akionekana kutokukubalia?
Hapa sasa haangalii kama kuna wanafunzi gani, atakuporomoshea mitusi hiyo, utazomewa na shule hutahudhuria kwa week nzima.

image001.jpg@01CB5645.7612B220

mhh...unamwekea katikati ya karatasi ya daftari lake la hesabu.... balaa ikamatawe na ticha... shule nziama watajua:confused2:
 
Tumetoka mbali hasa tulianza shule miaka ya 1970s!

Enzi zetu barua kama hii ilikuwa ukishaiandika, unatafuta nafasi ya umdhamiliae awe peke yake ili uweze kumkabidhi, kwa hiyo waweza kukaa nayo kwenye mfuko wa madaftari hata week nzima.

Na je utampatiaje hiyo barua?
Akishakuwa peke unachokifanya ni kumrushia usoni, halafu huyoo…unatimua mbio. Ukifika mbele kidogo unachungulia kama anaisoma.

Utajuaje kama amekukubali?
Ukiona anasoma halafu anatabasamu, ujue tayari .

Zawadi gani dada zetu walipendelea zaidi?
Ni kumnunulia mafuta ya Lady Gay au Yolanda (kama uko safi) au kandambili , hapo atakuona kweli unamjali.

Na je akionekana kutokukubalia?
Hapa sasa haangalii kama kuna wanafunzi gani, atakuporomoshea mitusi hiyo, utazomewa na shule hutahudhuria kwa week nzima.

image001.jpg@01CB5645.7612B220

DU UMENIKUMBUSHA MBALI SANAAAAAAAA MKUU SUPER STAR,sikiliza iyo ilivyo zamani izo nlipokua jeshini Ruvu Jkt pale mzeee nkamtokea mtoto;mtoto kanchomolea baada ya kunchomolea mi mzee nkajipinda nkaandika barua eti naanza kumtukana'kwanza huna shep'miguu ya kushoto'sjui kiuno kimepinda'huna lolote mwanamke atakua wewe'nimeona wanawake nini wewe'ile barua nikampa rafiki yake ampelekee'kweli akampelekea barua ikasomwa baada ya kusoma mzee ile barua ikapelekwa kwa Afande ikapigwa quikly biguller watu wakakusanyika mara moja bwaloni nikiwepo mimi'watu kama 1000 ivi mzee,nikaitwa jina mzee nikasimama toka mbele mzee chale zikaanza kunicheza,nikapewa ile barua soma kwa sauti mzee kigugumiziii,nikapewa bonge la bao mpaka chini akaichukua afande mwenyewe akasoma mzee kilichofuata apo ni historia kwangu mpaka leo,MAMBO YA ZAMANI AYO:A S-danger:
 
Copy and Paste at Power![
To be honest...I got no word to say...I wish I had but all I can say is...'thank you'...I know you are the best herein; at least you got to go through each and every topic...:confused2:
 
Duh! Ee bana ee! Afadhali umeamua kutuondoa kwenye mambo ya sihasa angalau kwa muda!
Mimi ilinitokea nimeandika barua (nikiwa standard six nakumbuka) kwenda kwa mdada mmoja wa standard five! Niliiandika usiku, si nikaisahau chini ya mto! Nikiwa shuleni nikawa nafikiria jinsi mama atakavyoingia chumbani kufanya usafi! Unajua ndivyo ilivyotokea!! Ile kurudi home mchana naangalia chini ya mto barua haipo (kumbuka kitanda kimetandikwa pia)!! Nikajua leo (siku hiyo) nimekwisha! Mshua kurudi, maza anamuonyesha barua! Dingi hakulaza damu, kaniita na kunitaka niisome mbele ya familia (wadogo zangu 3 wakubwa zangu 3 pembeni baba na mama) Kwa kweli kilichofuatia ni kipondo! Dingi yangu alikuwa anatembeza mkono mwanzo mwisho!!! Those days bana!!!

Jamani mbavu zangu mie.. Taratibu nyie watu...
Mimi nilimwandikia binti mmoja wajirani.. Kumbe Pacha wangu alishaombaga siku nyingi.. Binti akajibu 'wewe na ndugu yako wote mnanitaka..' Amueni wenyewe nani abaki na mimi! (RIP Pacha wangu alifariki 2006.03.27)
 
Hafu barua zenyewe zilikuwa za kurithishana, unamtafuta mshkaji mjanja mjanja kwa hivyo vitu anakushauri jinsi ya kuandika hiyo mistari. Heshima mbele.
 
Waungwana mumesahau mwendo wa kufoji stemp hasa bumu likiwa limekata nawe unataka mpendwa wako aupate ujumbe.
Stamp inafutwa kiufundi alafu unaipost kitu na box
 
Aah Mimi nimetoka kula uagali bwannaaaaaaaaaaaa ntaumwa bure. Jamani muwe mnaweka jionijioni sa za kwenda kudandia mabasi. Sasa unaona naumwa mbavu maana ugali umenibana kwenye dayaframu yangu!
 
Duh!!!!!!umenikumbusha mbali sana nakumbuka barua ya kwanza kuipata niliwekewa sh.7 nikairudisha kama ilivyo na majibu ambayo yaliandikwa na jopo la watu,,,sina mbavu ama tumetoka mbali:smile-big:
 
Waungwana mumesahau mwendo wa kufoji stemp hasa bumu likiwa limekata nawe unataka mpendwa wako aupate ujumbe.
Stamp inafutwa kiufundi alafu unaipost kitu na box
Mh,nilikuwa nafoji sana stamp yani kny desk langu ckosi gundi,sponchi,na sabuni!nadhani tulikuwa tunahujumu uchumi,,lol
 
Nilianza kitambo kidogo, Darasala tano hivi nakumbuka nilikuwa na mademu wawili tena nao ni marafiki! basi nawaandikia barua wote wawili wanasoma wanafurahi hao. Basi cku moja nikapewa denda na mmoja ilikuwa ugomvi ile mbaya! Wakagombana wao kwa wao. Yule mwenzie kanipa kabsaaaaaaaa. Da mbaaali sana aisee
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom