Tumetoka mbali hasa tulianza shule miaka ya 1970s! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tumetoka mbali hasa tulianza shule miaka ya 1970s!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by NGULI, Sep 17, 2010.

 1. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #1
  Sep 17, 2010
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Tumetoka mbali hasa tulianza shule miaka ya 1970s!  Enzi zetu barua kama hii ilikuwa ukishaiandika, unatafuta nafasi ya umdhamiliae awe peke yake ili uweze kumkabidhi, kwa hiyo waweza kukaa nayo kwenye mfuko wa madaftari hata week nzima.

  Na je utampatiaje hiyo barua?
  Akishakuwa peke unachokifanya ni kumrushia usoni, halafu huyooÂ…unatimua mbio. Ukifika mbele kidogo unachungulia kama anaisoma.

  Utajuaje kama amekukubali?
  Ukiona anasoma halafu anatabasamu, ujue tayari .

  Zawadi gani dada zetu walipendelea zaidi?
  Ni kumnunulia mafuta ya Lady Gay au Yolanda (kama uko safi) au kandambili , hapo atakuona kweli unamjali.

  Na je akionekana kutokukubalia?
  Hapa sasa haangalii kama kuna wanafunzi gani, atakuporomoshea mitusi hiyo, utazomewa na shule hutahudhuria kwa week nzima.


  [​IMG]
   

  Attached Files:

 2. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #2
  Sep 17, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Unapulizia na marashi ndani ya bahasha kusudi akifungua akautane na harufu nzuri pia unaandika na lyrics za wimbo wowote mzuri wa mapenzi uliokuwa unatamba enzi hizo pia kwenye hizo barua unabandika na sticker za mapenzi :A S 8: ili akiiona uwe umeongezewa credit baada ya hapo ataenda kuwaonyesha rafiki zake wakati wa mapumziko mida ya saa nne utamnunulia mihogo na siku ukimletea zawadi ya mafuta ya Yolanda ndio utazidi kupendwa dah enzi hizo.
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Sep 17, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Shida haina ngojangoja......ooh shida,
  Uwe na mapesa mengi ......ooh shida,
  Hata siku ya Arusi.............oooh shida,
  Kwa masikini na matajiri....Ooh shida,
  Mpaka siku ya mwisho.......oooh shida!

  BTW, it was such a wonderful life then!...Na usiombe barua hiyo idondoshwe na yeyote kati yenu, basi itafika kwa mwalimu mkuu, na adhabu yake usipime!

  This oldest profession bana!:lol::lol:
   
 4. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #4
  Sep 17, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Mwalimu mkuu anaanza kwa kukwambia usome ulichoaandika kwenye hiyo barua mbele ya wanafunzi wa shule nzima dah baada ya hapo kila mwanafunzi ukikutana naye sasa aibu yako halafu pia sasa na yule msichana aliyeandikiwa hiyo barua. Wanaitwa wazazi wenu halafu unapigwa suspension ya wiki mbili ukae nyumbani kwanza huko na kwenye unakutana na timbwili la mzazi sasa them old days acha tu:becky::becky::becky:
   
 5. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #5
  Sep 17, 2010
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Halafu aikote mwal wa kike anaitwa Victoria na wewe ulimwandikia msichana anaitwa Victoria......
   
 6. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #6
  Sep 17, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  :laugh::laugh::laugh::laugh::laugh:Halafu itokee kwamba ni mama mtu mzima hiyo kesi yake :fencing:
   
 7. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #7
  Sep 17, 2010
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Then ukute huyo mwl ni mjamzito na ujauzito hukukupenda:eyebrows::lol:
   
 8. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #8
  Sep 17, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Du! Nimebaki nacheka tu kwani nimekumbuka mengi sana ya miaka ile.
   
 9. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #9
  Sep 17, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  :laugh::laugh::laugh:Shule utaiona chungu sana
   
 10. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #10
  Sep 17, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  We Babuyao ulikuwa mtundu sana..
  Unakumbuka kuwa kuna siku ilikuwa ulishushwa kwenye basi katikati ya pori?:lol:
  Na pia uliwahi kumpiga mwalimu ukalala polisi!:lol:
  Halahu uliwekwa korokoroni na mchumba wako wa enzi hizo..huh!:lol:
   
 11. RR

  RR JF-Expert Member

  #11
  Sep 17, 2010
  Joined: Mar 17, 2007
  Messages: 6,719
  Likes Received: 206
  Trophy Points: 160
  Nilijifanya kidume nikafanya hii kitu nikiwa darasa la pili.....infact sikua najua hata format ya barua....
  Niliandikia hivi ' kwa XXXX nimesikia kuwa nanhii (kwa kilugha - sikujau kiswahili chake) ni tamu sana'......end of the letter...

  Nikampa mshikaji ampelekee....akaichukua na kuipeleka kwa mwalim mkuu (alikua mwanamke).... kipondo kilifata na barua akapelekewa mzazi wangu...:A S 20::A S 20:
   
 12. J

  Jmpambije Member

  #12
  Sep 17, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Patamu Zaidi, kumbe na mwl Victoria naye alikuwa akikutamani!!!!!
  Si unajua tena enzi hizo utakuta mwl na mwanafunzi lika moja.
   
 13. Konakali

  Konakali JF-Expert Member

  #13
  Sep 17, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 1,508
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Ole wako ukute ulimwandikia Neema na wakati mwalimu mkuu au wa taaluma anamtamani au anatembea naye....! Nakuambia utakoma...! Ukikutwa kola ya shati ni chafu utaogeshwa mbele ya paredi...! Au ukute umejaladia, utavuliwa mbele ya wanafunzi wote na utaendelea kula fimbo....! Sasa ukute pia umevaa zileeeeee kaptula za kufungwa kwa vifungo, halafu na wewe umeanza kupata hisia zilizokuongaoza kuandika barua hiyo...!
   
 14. Fixed Point

  Fixed Point JF Bronze Member

  #14
  Sep 17, 2010
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 11,321
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  ha haaaaaaaaaaaaa. I miss those old ages.
  Barua zilikuwa utamu wake bwana. kasheshe ilikuwa ilikamatwa. nakumbuka kuna mdada shuleni alikuwa kila wiki lazima achapwe kwa ajili ya barua, na alikuwa anasema hawawezi kuniua ila satisfaction ninayopata kupitia hizi barua yatosha kuondoa maumivu ya viboko, ha haaaaaaaaa. siku hizi? sms, not long letters................
   
 15. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #15
  Sep 17, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Mbaya zaidi siku hizi kuna vitu vingine unamaliza thru sms
   
 16. Fixed Point

  Fixed Point JF Bronze Member

  #16
  Sep 17, 2010
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 11,321
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  mhhhhhhhhhhhh! huko sipo
   
 17. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #17
  Sep 17, 2010
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  ha ha ha ha mbavu zangu jamani
   
 18. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #18
  Sep 17, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Sijawahi kupitia Kipindi hicho nadhani maisha yalikuwa safi sana..
  Sasa kila kitu ni mambo ya fedha ooh sina cmu ya mkononi, ooh nitumie vocha , ooh ntaka nataka Rav 4 new model nimeiona sweet lotion naitamani mie

  Kweli mambo yanaenda yakibadilika sana
   
 19. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #19
  Sep 17, 2010
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  FL wewe utakuwa wale wa st. Marrys umekosa furha katika maisha yako enzi hizo ukimpenda mschana unamwambia kwetu tuna TV jana tulikula wali na nyama
   
 20. edwinito

  edwinito JF-Expert Member

  #20
  Sep 17, 2010
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 211
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Duh! Ee bana ee! Afadhali umeamua kutuondoa kwenye mambo ya sihasa angalau kwa muda!
  Mimi ilinitokea nimeandika barua (nikiwa standard six nakumbuka) kwenda kwa mdada mmoja wa standard five! Niliiandika usiku, si nikaisahau chini ya mto! Nikiwa shuleni nikawa nafikiria jinsi mama atakavyoingia chumbani kufanya usafi! Unajua ndivyo ilivyotokea!! Ile kurudi home mchana naangalia chini ya mto barua haipo (kumbuka kitanda kimetandikwa pia)!! Nikajua leo (siku hiyo) nimekwisha! Mshua kurudi, maza anamuonyesha barua! Dingi hakulaza damu, kaniita na kunitaka niisome mbele ya familia (wadogo zangu 3 wakubwa zangu 3 pembeni baba na mama) Kwa kweli kilichofuatia ni kipondo! Dingi yangu alikuwa anatembeza mkono mwanzo mwisho!!! Those days bana!!!
   
Loading...