Enzi zetu

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
54,655
58,972
Enzi zetu barua kama hii ilikuwa ukishaiandika, unatafuta nafasi ya umdhamiliae awe peke yake ili uweze kumkabidhi, kwa hiyo waweza kukaa nayo kwenye mfuko wa madaftari hata week nzima.
Na je utampatiaje hiyo barua?
Akishakuwa peke unachokifanya ni kumrushia usoni, halafu huyoo…unatimua mbio. Ukifika mbele kidogo unachungulia kama anaisoma.

Utajuaje kama amekukubali?
Ukiona anasoma halafu anatabasamu, ujue tayari .

Zawadi gani dada zetu walipendelea zaidi?
Ni kumnunulia mafuta ya Lady Gay au Yolanda (kama uko safi) au kandambili , hapo atakuona kweli unamjali.

Na je akionekana kutokukubalia?
Hapa sasa haangalii kama kuna wanafunzi gani, atakuporomoshea mitusi hiyo, utazomewa na shule hutahudhuria kwa week nzima.
 
Hapa unazungumzia darasa la ngapi vile ..:thinking:
 
Yeye anakujibu kwa barua iliyochorwa maua mengi namaandishi yaliyotengenezwa kwa umbo la moyo siku ya do ze nidf nisiku ya sabasaba au noeli disco toto lililofungwa na dj hapo kijijini mazungumzo niwakati mnasubiri dj arudi na betrii ya gari n120,afunge mitambo umechomea na chachacha! Shati la nylon linalovutika na chini umepitisha kamba linajaa upepo!au umechomea shati la pembe unachomekea nyuma mbele unapaacha kama ulimi tumetoka mbali achatu!
 
Kweli qwewe umetoka mbali
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom