Tumeshindwana na aliyekuwa mpenzi wangu, nimempeleka mahakamani, sasa anaomba msamaha

Hayo umesema wewe , maana ufahamu wake ni mdogo unajua kufungua zipu tu lkn kufunga hujui pole sana
Dada,, usiseme hivyo.. Japo sina hela lkn nina uhakika ukiwa na mm siku nikijaribu kukutoroka utalia ufe.
 
Kumbe kuna wanawake wana roho mbaya hivi?/ya a ni umeshtaki amehumiwa bado unafungua na kesi ya madai? Sitaki kuamino
 
Kama walivyo wanaume wenye roho mbaya kama wewe
Kwanini usimsamehe tu dada? Achana naye dada, fanya mambo yako. Ukimsamehe kwanza utajikuta mwepesi na amani tele moyoni. Watu wengi huingia kwenye huu mtego wa kutokusamehe matokeo yake yanakuwa si mazuri maana unaweza kujisemea moyoni uko vizuri kumbe kuna kitu kinakuwa kinakukereketa. Just forgive him and move on, haikuwa ridhiki wala hakuwa wako na yeye akubali haukuwa wake. There wasn't a good chemistry between you two. Mwisho napenda kusema, kua uyaone mkuu.
 
Mi nipo tayari kumlipia kama kweli je unaweza nipa namba za huyo mwanaume!?
 
jiulize unamkomesha kwa lipi hasa?
kwa kutafuta mpenzi mwingine,
kwa kukublock,
au kwa kukupigia cm mara kwa mara.
au hayo yote jumlisha kukutamkia maneno machafu?
 
Habarini wanajamvi?

Nilikuwa na mpenzi ambaye tulikuwa na mpango wa kufunga ndoa hapo baadae.
Akaanza kunilalamikia kuwa anataka penzi langu lkn mimi sikuridhia kwasababu hii ni Sera yangu na nilimwambia mapema kuwa sitafanya mapenzi bila kuwa na ndoa na alikubali.

Alikuwa ananisumbua sana kila tukionana hana habari nyingne zaidi ya kutaka penzi nilimkatalia sana baadae akabadiri gia akataka niende kwake nikamfulie nguo.

Nilimkatalia nikamwambia Mimi bado si mkewe so siwezi fanya jukumu lolote la mke.

Baada ya kumjibu vile alinitishia kutafuta mwanamke mwingine ataye muhudumia pamoja na kumpa penzi.

Akanipa siku mbili nifikirie.

Nilimjibu hana haja yakunipa hata saa moja kufikiria yeye aendelee tu kutafuta.

Baada ya siku tatu akanipigia simu akaniambia ameshampata kwahiyo Mimi niendelee na maisha yangu.

Nikamshukuru kwa kunipataarifa nikaendelea na maisha yangu.

Anapoishi ni lazima apite kwangu ndipo afike kwake nikawa nawashuhudia wakiingia na kutoka na huyo mpenzi wake mpya.

Chakushangaza baada ya wiki tatu kupita akaanza kunipigia simu, sikutaka kupokea simu zake na akituma meseji nilikuwa nafuta kabla ya kuzisoma.

Akaona haitoshi akanivizia ile natoka tu kwenda kazini akapaki gari lake vibaya ilinishindwe kupita, nikamuomba apaki gari lake vzr nipite lkn akaniambia hawezi kuliondoa mpaka nimhakikishie kuwa nitakuwa napokea simu zake, kwasababu nilitaka kuwahi kzn ilinibidi ni mkubalie tu. Baada ya kukubali akaniruhusu niondoke.

Jioni yake akapiga simu Mara 25 sikupokea kbsa.

Kesho yake akaniblock tena, sikutaka kubishana nae tena niligeuza gari na kuirudisha home nikapanda boda boda na kwenda job.

Wakati narudi jioni nilimkuta mlangoni kwangu, sikujali nikafungua geti niingie ndani akanivuta na kunitoa nje.
Kabla sijasema neno alianza kunikashifu na kunitukana.

Alinitukana matusi yote , sikujibu neno.
Nilitulia nikisikiliza kwa makini matusi yake, alikuwa anatukana kwa sauti kiasi cha watu kujaa, walimsihi aache matusi lkn hakusikia.

Nikaona isiwe tabu nikaingia zangu ndani nakuendelea na shughuli zangu.

Kesho yake niliona vyema nikaripoti polisi, maana ushahidi nilikuwanao.

Akakamatwa tukaenda mahakamani kesi ikaendelea hukumu ikatoka akakutwa na hatia akahukumiwa kulipa faini ya sh. 2 au kwenda jela miezi 6. Akalipa fain na kuachiwa huru.

Nikafungua kesi ya madai ya fidia ya ghalama za kesi pamoja na fidia ya kudhalilishwa ametakiwa kunilipa ml 10

Pesa hana analia kama mtoto anaomba nsamehe.

Nimenuia kumkomesha ili iwe fundisho kwa watu wenye akili kama zake.

Nitakuwa nimekosea? naomba ushauri wenu hasa wanawake wenzangu.
 
Unajua dada pesa si kitu, iyo faini ya 10m achana nayo ila hakikisha usije kurogwa hata siku moja ukamrudia huyo kaka atakuja kulipiza kisasiii. Akichoka kukuona wewe ahame mji
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom