Tumeshindwana na aliyekuwa mpenzi wangu, nimempeleka mahakamani, sasa anaomba msamaha

Cleopatra 2

JF-Expert Member
Oct 9, 2016
210
306
Habarini wanajamvi?

Nilikuwa na mpenzi ambaye tulikuwa na mpango wa kufunga ndoa hapo baadae.
Akaanza kunilalamikia kuwa anataka penzi langu lkn mimi sikuridhia kwasababu hii ni Sera yangu na nilimwambia mapema kuwa sitafanya mapenzi bila kuwa na ndoa na alikubali.

Alikuwa ananisumbua sana kila tukionana hana habari nyingne zaidi ya kutaka penzi nilimkatalia sana baadae akabadiri gia akataka niende kwake nikamfulie nguo.

Nilimkatalia nikamwambia Mimi bado si mkewe so siwezi fanya jukumu lolote la mke.

Baada ya kumjibu vile alinitishia kutafuta mwanamke mwingine ataye muhudumia pamoja na kumpa penzi.

Akanipa siku mbili nifikirie.

Nilimjibu hana haja yakunipa hata saa moja kufikiria yeye aendelee tu kutafuta.

Baada ya siku tatu akanipigia simu akaniambia ameshampata kwahiyo Mimi niendelee na maisha yangu.

Nikamshukuru kwa kunipataarifa nikaendelea na maisha yangu.

Anapoishi ni lazima apite kwangu ndipo afike kwake nikawa nawashuhudia wakiingia na kutoka na huyo mpenzi wake mpya.

Chakushangaza baada ya wiki tatu kupita akaanza kunipigia simu, sikutaka kupokea simu zake na akituma meseji nilikuwa nafuta kabla ya kuzisoma.

Akaona haitoshi akanivizia ile natoka tu kwenda kazini akapaki gari lake vibaya ilinishindwe kupita, nikamuomba apaki gari lake vzr nipite lkn akaniambia hawezi kuliondoa mpaka nimhakikishie kuwa nitakuwa napokea simu zake, kwasababu nilitaka kuwahi kzn ilinibidi ni mkubalie tu. Baada ya kukubali akaniruhusu niondoke.

Jioni yake akapiga simu Mara 25 sikupokea kbsa.

Kesho yake akaniblock tena, sikutaka kubishana nae tena niligeuza gari na kuirudisha home nikapanda boda boda na kwenda job.

Wakati narudi jioni nilimkuta mlangoni kwangu, sikujali nikafungua geti niingie ndani akanivuta na kunitoa nje.
Kabla sijasema neno alianza kunikashifu na kunitukana.

Alinitukana matusi yote , sikujibu neno.
Nilitulia nikisikiliza kwa makini matusi yake, alikuwa anatukana kwa sauti kiasi cha watu kujaa, walimsihi aache matusi lkn hakusikia.

Nikaona isiwe tabu nikaingia zangu ndani nakuendelea na shughuli zangu.

Kesho yake niliona vyema nikaripoti polisi, maana ushahidi nilikuwanao.

Akakamatwa tukaenda mahakamani kesi ikaendelea hukumu ikatoka akakutwa na hatia akahukumiwa kulipa faini ya sh. 2 au kwenda jela miezi 6. Akalipa fain na kuachiwa huru.

Nikafungua kesi ya madai ya fidia ya ghalama za kesi pamoja na fidia ya kudhalilishwa ametakiwa kunilipa ml 10

Pesa hana analia kama mtoto anaomba nsamehe.

Nimenuia kumkomesha ili iwe fundisho kwa watu wenye akili kama zake.

Nitakuwa nimekosea? naomba ushauri wenu hasa wanawake wenzangu.
 
sidhani kama hii story ya kweli eti sh. 2 au kwenda jera miezi 6 duuu. baada ya kuenda polisi jamaa alifunguliwa criminal case au vp kama ilikua criminal case ni cost zipi uliingia huku kesi za jinai zote zinasimamiwa na serikali maana makosa ya jinai ni against Republic ww unakua shahidi tuu hebu tueleze ni cost zipi uliincure huwezi hire ata advocate hapa
 
Sikuleta hii story ili wewe uamini rejea point yangu ya mwsho
 
sidhani kama hii story ya kweli eti sh. 2 au kwenda jera miezi 6 duuu. baada ya kuenda polisi jamaa alifunguliwa criminal case au vp kama ilikua criminal case ni cost zipi uliingia huku kesi za jinai zote zinasimamiwa na serikali maana makosa ya jinai ni against Republic ww unakua shahidi tuu hebu tueleze ni cost zipi uliincure huwezi hire ata advocate hapa
Utakuwa graduate wa kule nanihii wewe. Kwani mtu hawezi kufungua kesi ya madai baada ya ile ya jinai kutolewa hukumu? Kasema gharama ya kesi, hajasema ni kesi ipi wajuaje kama kazungumzia gharama za hiyo kesi yake ya madai?
 
Tatizo lenu nyinyi wanawake mliosoma sana kwenye mahusiano huwa hampendi kupangiwa ..jamaa alikuwa anakupenda sana alifanya yote hayo ilikukuvuta hisia zako.. Tatizo kubwa liko kwako..mwanaume anapenda kuheshimiwa...Ungekuja hapa kuomba ushauri kabla ya kwenda mahakamani...ulichokifanya ni sahihi ila si sahihii sanaa..
ASONONESHAE NAFSI ZA WATU HUMCHUKIZA MUNGU..
Ulipaswaa kumsameheee,
Sasa watu watakuogopa na kuolewa UTASUBIRI SANAA
 
ww umeona kunakesi ya madai hapo kataja, mm sijasoma sheria ila kunavitu tuu unatakiwa uvielewe au ww umeona kunasehemu amesema alifungua kesi mbili ya jinai na ya madai. yeye kasema baada ya kutolewa hukumu ya eidha jamaa kulipa sh. 2 au kwenda jela miezi 6 na jamaa kalipa faini ndo kesi ya gharama zake za kuendesha kesi ya kwanza kaenda fungua na jamaa anatakiwa kulipa mil 10. ndo nmeuliza gharama zipi alitumia ktk criminal kesi. ficha ujinga wako
 
Tatizo lenu nyinyi wanawake mliosoma sana kwenye mahusiano huwa hampendi kupangiwa ..jamaa alikuwa anakupenda sana alifanya yote hayo ilikukuvuta hisia zako.. Tatizo kubwa liko kwako..mwanaume anapenda kuheshimiwa...Ungekuja hapa kuomba ushauri kabla ya kwenda mahakamani...ulichokifanya ni sahihi ila si sahihii sanaa..
ASONONESHAE NAFSI ZA WATU HUMCHUKIZA MUNGU..
Ulipaswaa kumsameheee,
Sasa watu watakuogopa na kuolewa UTASUBIRI SANAA
Mkuu usiongee kwa kuangalia upande mmoja..embu jaribu kutazama na upande wapili
 
Back
Top Bottom