Tumeshakusamehe Mh. Rais, karibu Kagera

Alexism

JF-Expert Member
Aug 14, 2011
3,423
2,045
Kwako Mh.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Pole na kazi na uwajibikaji unaofanya kila siku kwa ajiri ya Taifa letu.Mh. Rais, mkoa wa Kagera tulipata janga ambalo kweli itakua vigumu kusahaurika kwenye Historia ya mkoa wetu .Watu walipoteza maisha na malizao nyingi tu.

Serikali kweli iliitikia kilio cha waathirika kwa kuchangisha pesa na rambi rambi kwa ajiri ya waathirika ingawa michango hiyo kiukweli aslimia kubwa inawezekana zilikua ahadi na bado labda hazijatekerezwa maana waanga hawajafikiwa.Mh. Rais kumbuka pia ulikatisha safari kwenda Zambia kwa sababu ulitaka kuungana nasi katika matatizo yaliyotupata ingawa tunajua kua tetemeko halikuletwa na serikali.

Mh. Rais kumbuka hawali Chato ilikua wilaya ya mkoa wa Kagera na tuliishi nawewe kama ndugu na jirani mpaka ukawa unasema wewe ni ukoo wa Bahinda Abazila Enkende.

Mh.Rais wetu wa JMT mengi yamesemwa kuhusu pesa, rambi rambi na wewe kutofika kwenye eneo la tukio mpaka leo. Sisi wana Kagera wala hatuna hasira au kinyongo na wewe ila kwakua huko likizo kijijini kwako hapo Chato basi itakua vizuri ututembelee kabla ya kurudi Ikulu.

Tena nitakua mstari wa mbele kukuandalia uwanja wetu Gymkhana wengine wanapenda kupaita Lowassa Stadium bila shaka unapajua maana hiyo ni sehemu ambayo uliwaombea kura wana Kagera nawakakusikiriza.

Mh.Rais usije ukaogopa labda kwamba wana Kagera watakudai meli ambayo uliwaaidi ndani ya siku 60 maana ata walio kutangulia hawakutimiza ahadi hiyo.

Mh.Rais karibu Kagera tumeisha samehe. ..njoo tuzungumze Omuyango /Omuhinda Omuzila nkende
 
Hata msingesamehe asingekuja huko. Mlimpigia kura kwa mbwembwe sana, sasa sijui alaumiwe nani?
 
Tumemsamehe kabisa aje tu na hakuna atakaye dai meli maana watangurizi wake nao hawakutimiza hiyo ahadi...Karibu Gymkhana Omuyango Omuzila Nkende
 
Hivi.......
Huyu m-bobezi wa kemia ni member humu jf?
Bora hili bandiko ungelipeleka kule redio mawingu, ndipo hua snapendelea zaidi.
Samahani kwa kutoka nje ya mada....
 
Umeanza lini kua mshauri wetu
 
Aje ili iweje, akwende zake huko. Ubaya ubaya tu na yeye siyo Mungu wa Tz wala Kagera.
 
Tushikishe adabu mpaka tukome, ulipofika Bihalamuro, nilisubili office ya chama ili nisign fomu yako kukudhamini lakini walikukimbia kwa sababu nguvu zote waliwekeza kumdhamini Mamvi. sasa ndo wanaona unafaa eee. tushikishe adabu.
 
Huu ni muda wa kusamehe ndugu zangu huku tupo tayari kumpokea hapa Gymkhana aka Lowassa stadium wala asiogope kua tutauliza sijui rambi rambi au meli maana hayo yamepita labda wakiuliza wasio kupenda. .Omuyango Omuzila Nkende
 
Kwako Mh.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Pole na kazi na uwajibikaji unaofanya kila siku kwa ajiri ya Taifa letu.Mh. Rais, mkoa wa Kagera tulipata janga ambalo kweli itakua vigumu kusahaurika kwenye Historia ya mkoa wetu .Watu walipoteza maisha na malizao nyingi tu.

Serikali kweli iliitikia kilio cha waathirika kwa kuchangisha pesa na rambi rambi kwa ajiri ya waathirika ingawa michango hiyo kiukweli aslimia kubwa inawezekana zilikua ahadi na bado labda hazijatekerezwa maana waanga hawajafikiwa.Mh. Rais kumbuka pia ulikatisha safari kwenda Zambia kwa sababu ulitaka kuungana nasi katika matatizo yaliyotupata ingawa tunajua kua tetemeko halikuletwa na serikali.

Mh. Rais kumbuka hawali Chato ilikua wilaya ya mkoa wa Kagera na tuliishi nawewe kama ndugu na jirani mpaka ukawa unasema wewe ni ukoo wa Bahinda Abazila Enkende.

Mh.Rais wetu wa JMT mengi yamesemwa kuhusu pesa, rambi rambi na wewe kutofika kwenye eneo la tukio mpaka leo. Sisi wana Kagera wala hatuna hasira au kinyongo na wewe ila kwakua huko likizo kijijini kwako hapo Chato basi itakua vizuri ututembelee kabla ya kurudi Ikulu.

Tena nitakua mstari wa mbele kukuandalia uwanja wetu Gymkhana wengine wanapenda kupaita Lowassa Stadium bila shaka unapajua maana hiyo ni sehemu ambayo uliwaombea kura wana Kagera nawakakusikiriza.

Mh.Rais usije ukaogopa labda kwamba wana Kagera watakudai meli ambayo uliwaaidi ndani ya siku 60 maana ata walio kutangulia hawakutimiza ahadi hiyo.

Mh.Rais karibu Kagera tumeisha samehe. ..njoo tuzungumze Omuyango /Omuhinda Omuzila nkende
Wewe na nani? Jisemee
 
Kagera ni moja ya mikoa ya Tanzania na Rais wake ni Dr John Magufuli hakuna MTU wa kumzuia kutembelea eneo hilo.

Na alishasema mwanzoni kabisa tetemeko lilipotokea alipokuwa anamkabidhi Waziri Mkuu michango ya tetemeko kuwa atakuwa wa mwisho kufika huko.

Siku iliyopangwa kuja huko atakuja tu.

Tunashukuru kwa ushirikiano na kujali kwako.
 
Back
Top Bottom