kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 12,319
- 12,622
Wazo la taifa kuhamishia shughuli zake Dodoma ni la siku nyingi tangu serikali ya awamu ya kwanza. Sababu kubwa ya kuhamia tuliyoelezwa ni kuwa Dodoma ni katikati ya nchi, hivyo Watanzania wengi ingewawia rahisi kufika Dodoma na kuhudumiwa kwa haraka.
Wakati wazo hili linatolewa miaka hiyo kulikuwa na maendeleo hafifu sana ya mawasiliano na usafiri kama ilivyo leo. Hivyo watu walihitaji kusafiri hadi makao makuu ya Wizara ili kupata huduma.
Kutokana na maendeleo ya njia za kupeana habari kama vile simu, internet, computer, redio, television, teleconference, ndege, reli na barabara za kisasa yalivyo sasa huenda sababu na gharama za kuhamishia makao makuu Dodoma ni ghali sana kuliko kuimarisha mifumo ya kidigitali hadi vijijini ili wananchi wahudumiwe hukohuko wakiwa mikoani, wilayani, tarafani, katani na vijijini kuliko kusafiri kwenda hadi Dodoma.
Huenda fedha za kukamilisha zoezi hili zingetosha kabisa kuimairisha miundombinu ya e-government (umeme, internet) nchi nzima hadi kwenye wilaya na vitongoji na kuondoa kabisa ulazima wa watu kusafiri hadi makao makuu ya Wizara Dodoma na kujikita zaidi kwenye zile activities zinazohusika moja kwa moja na kuongeza uchumi.
Je, wewe unaonaje, tuendelee na mpango huu wa kuwatayarisha watu kwenda Dodoma kuhudumiwa au tuimarishe e-government ili watu wahudumiwe bila kulazimika kwenda makao makuu ya wizara?