Tumepona, kazi iendelee

Apr 8, 2023
26
17
Yamekuwa na nadhani yataendelea kuwa maoni yangu kwamba kubadili mitaala ya nchi ni moja ya mambo makubwa kabisa yanayoweza kuacha alama kwenye vizazi vyetu, na hivyo wakati Serikali inapofanya juhudi za kubadili mitaala ya shule zetu, ni vyema jamii kwa ujumla wake kujitolea kuchangia badala ya kufanya tu propaganda na siasa majitaka.

Ndiyo, nadhani ni vyema sasa kuamini kwamba juhudi za “kuiponya nchi” zimezaa matunda, na kwamba majeraha yamekuwa makovu na hivyo wale ambao bado yanatoka usaha, waachwe wajifie maana wamekataa kuwa sikio la kupona, asomaye na afahamu mimi hizi ni salaam tu nawasalimia.

Yako maeneo kadhaa makubwa zinakoelekezwa juhudi za serikali na ambako kusema kweli, ebu tulete pamoja vipawa, ujuzi, uzoefu na elimu zetu kusaidia, na mfumo wa elimu ni mojawapo, na kwangu nadhani ndiyo kipaumbele namba moja.

Huenda tusiweze kwa sasa kubadili mitaala ya “Elimu ya Juu” kwa vile huenda hatuna nyenzo wala rasilimali watu na fedha ya kufanya tafiti na kuanzisha yale tuyatakayo, lakini kuwa na mfumo wa elimu yenye watu wanaojitambua, wenye uzalendo kwa familia, jamii, taifa na bara lao, wenye ujasiri wa kuthubutu na kujadiliana kwa niaba ya watu wao, hili linawezekana sana kuliko tunavyodhani na matokeo yake yanawezekana kutokea haraka sana. Ni mambo yanaweza kuonekana ndani ya miaka kumi na tano tu bila kuchelewa.

Unasema nasema nini!? Kwani hujui kwamba Watanzania walitengenezwa kutokea makabila ya Tanganyika na Zanzibar kwa kupitia tu mfumo wa elimu ya msingi, sekondari na Jeshi la kujenga taifa!?. Bado huelewi nasema nini!?. Kimsingi baada ya uhuru hatukuwa na wasomi wengi na hata wazo tu la kuhakikisha walau watanzania wanajua zile K3 yaani Kusoma, Kuandika, na Kuhesabu ilikuwa kazi ngumu iliyofanya kuzaliwa walimu wa UPE na ingawa baadaye waliozalishwa na UPE walirejea na shukurani ya Punda kwa wazazi wao, lakini UPE ilitengeneza wengi wa viongozi tulio nao leo, tulia nikufundeni historia kidogo enyi wana maana mwaniapisha na miye naapa simo, tena simo kabisaa sihusiki!

Kisha kwa vile tulihitaji kutengeneza “taifa moja”, amri ikatolewa kwamba “lugha ya taifa” ni Kiswahili na kwamba kwenye taasisi zote za umma (ikiwemo mashule, hospitali na kwingineko) lugha ya mawasiliano itakuwa Kiswahili. Masomo yakawa yakifundishwa kwa Kiswahili na walau moja ya faida walizokuwa nazo wale waliomaliza Darasa la saba ni uwezo wa kuelewa na kuzungumza Kiswahili; ingawa kusema kweli hawakuweza kukichalaza kama cha Mheshimiwa Mwenyekiti wa CCM taifa, na miye humu nahusikaje!? Simo nasema.

Kule kwa wala Senene hadi leo bado wanapata taabu kutamka Ng’ombe na kusema kweli “ukiwaganganiza” kutamka Ng’ombe, mke nenda naye mahari imeshindikana kulipwa, ama unataka nikwambie Wakurya na Mama Ghati anayeuza “Ujhi” wa moto!!?.

Nasema mnitoe humu maana sihusiki. Kiswahili iliposimamiwa kuwa lugha ya Taifa letu, leo Watanzania hatuulizani makabila tunapokutana, lahaja zetu tu ndizo husema huyu ni Mmakunduchi, huyu Muha na huyu ‘Njomba Nchumali, Ntoto wa Chumuni, na bila shaka huyu atakuwa “Niangusage sambi sako mwenyewe” lakini ilikuwa ukimaliza darasa la saba unaweza kuzungumza “kitanzania” asomaye na fahamu, mimi hizi ni salaam tu nawasalimia.

Zilipoanzishwa ‘spesho skuli’ za Wavulana na Wasichana kama Bwiru, Tabora na Mtwara, ilikuwa pamoja na kuwaleta watu wa makabila, mila, tamaduni na desturi tofauti mahala pamoja kwa miaka minne, kwa vile iliaminika kwamba watakapoondoka, utamaduni mpya utakuwa umezaliwa , utamaduni wa kitanzania. Kisha kuna kile kilichokuwa kikifundishwa (content) ambacho ingawa sehemu kubwa kilikuwa na maandalio ya mkoloni, lakini ufundishaji wake na mazingira yake walau yalitusaidia kupata watanzania kama ilivyo leo.

Kisha tukaanza kutengeneza “Watanzania” literally kwa kuhakikisha kwamba Mulangira anakutana na Manka kupitia JKT au amepangwa na Musubhati kwenye kituo kimoja cha kazi kule Nakapanya na hivyo mtoto anayezaliwa anakuta humo ndani kinachozungumzwa ni “Kitanzania” na hivyo wawili hawa hawana budi ila kuzaa “Mnyamahanga” au “Chasaka” ambaye hasa huyu ndiye alikuwa Mtanzania na japo kusema kweli sina nijualo, hizi ni salaam nawasalimia.

Ni kwa msingi huo, na kwa sababu pia kwamba uongozi unazaliwa na kutengenezwa kutegemea na nini kimetangulia chenzie, tunahitaji kuanza upya kwa kuwa na “shule maalumu” tena za msingi na sekondari na mara hii nashauri “Paramilitary schools” kwa sababu nyingi tu (labda nitaweza kuandika zaidi huko mbeleni), lakini ni muhimu walau kila kanda au kila Brigade iwe na shule ya msingi na sekondari inayoendeshwa na majeshi yetu na ambayo kazi yake itakuwa ni kutengeneza special breeds kwa ajili ya Tanzania ya miaka 30-50 ijayo.

Pamoja na haya, nadhani tuondoe kwenye shule zote historia zilizoandikwa na wakoloni na kutumia historia zilizoandikwa na sisi wenyewe, wanetu waambiwe historia ya miaka 100 ya kupigania uhuru wa bendera hadi sasa, waambiwe mashujaa wetu, waambiwe maumivu, majeraha na uchungu wetu, waambiwe ushindi na mafanikio yetu, warithishwe ndoto za kesho yetu.

Ikiwa Wakoloni walifaulu kwa miaka 50 tu kufuta kabisa historia ya babu zetu kabla ya ukoloni, na kutuaminisha kwamba Waafrika hatukuwa utamaduni wenye nguvu kabla ya wao “kutugundua”, tunashindwa nini kuwaaminisha wanetu tofauti kwa kupitia mfumo wetu wa elimu!!?.

Nisikuchosheni maana najua “mambo ni mengi na muda ni mchache, lakini ni maoni yangu kwamba wakati huu, pamoja na kuandaa mitaala “ya kitaalamu”, nadhani wote kama jamii tuje pamoja, tume zinazofanya mambo haya zianzishe midahalo na makongamano na kuvuna maoni na mawazo ya Watanzania wenyewe juu ya kile wanachokitaka kwenye elimu ya watoto wao baada yao, badala ya “wataalamu” kujifungia ndani na kuja na mitaala ya “kitaalamu” kwa vile wameshalamba posho zao liwalo na liwe.

Watanzania wasio na “utaalamu” hata kidogo, wanajua kinachowastahili watoto wao kwa ajili ya kesho kwa sababu hata hivyo, wengi wa “Mashimba” sisi tusiosoma na tusio na utaalamu hata kidogo, tunao ujuzi na uzoefu kutoka kushindana na kule tulikotoka hadi kukaa meza moja kwenye majumba ya mashauri pamoja na “wasomi” wenye degree nyingi kuliko thermometer, na wengi wetu ndiyo tunaoendesha biashara na uchumi kwa kilimo na ufugaji, matokeo yanapaswa kusema zaidi kuliko makaratasi asomaye na afahamu, mimi hizi ni salaam tu nawasalimia!. Wasalaam!
 
Yamekuwa na nadhani yataendelea kuwa maoni yangu kwamba kubadili mitaala ya nchi ni moja ya mambo makubwa kabisa yanayoweza kuacha alama kwenye vizazi vyetu, na hivyo wakati Serikali inapofanya juhudi za kubadili mitaala ya shule zetu, ni vyema jamii kwa ujumla wake kujitolea kuchangia badala ya kufanya tu propaganda na siasa majitaka. Ndiyo, nadhani ni vyema sasa kuamini kwamba juhudi za “kuiponya nchi” zimezaa matunda, na kwamba majeraha yamekuwa makovu na hivyo wale ambao bado yanatoka usaha, waachwe wajifie maana wamekataa kuwa sikio la kupona, asomaye na afahamu mimi hizi ni salaam tu nawasalimia. Yako maeneo kadhaa makubwa zinakoelekezwa juhudi za serikali na ambako kusema kweli, ebu tulete pamoja vipawa, ujuzi, uzoefu na elimu zetu kusaidia, na mfumo wa elimu ni mojawapo, na kwangu nadhani ndiyo kipaumbele namba moja.
Huenda tusiweze kwa sasa kubadili mitaala ya “Elimu ya Juu” kwa vile huenda hatuna nyenzo wala rasilimali watu na fedha ya kufanya tafiti na kuanzisha yale tuyatakayo, lakini kuwa na mfumo wa elimu yenye watu wanaojitambua, wenye uzalendo kwa familia, jamii, taifa na bara lao, wenye ujasiri wa kuthubutu na kujadiliana kwa niaba ya watu wao, hili linawezekana sana kuliko tunavyodhani na matokeo yake yanawezekana kutokea haraka sana. Ni mambo yanaweza kuonekana ndani ya miaka kumi na tano tu bila kuchelewa.

Unasema nasema nini!? Kwani hujui kwamba Watanzania walitengenezwa kutokea makabila ya Tanganyika na Zanzibar kwa kupitia tu mfumo wa elimu ya msingi, sekondari na Jeshi la kujenga taifa!?. Bado huelewi nasema nini!?. Kimsingi baada ya uhuru hatukuwa na wasomi wengi na hata wazo tu la kuhakikisha walau watanzania wanajua zile K3 yaani Kusoma, Kuandika, na Kuhesabu ilikuwa kazi ngumu iliyofanya kuzaliwa walimu wa UPE na ingawa baadaye waliozalishwa na UPE walirejea na shukurani ya Punda kwa wazazi wao, lakini UPE ilitengeneza wengi wa viongozi tulio nao leo, tulia nikufundeni historia kidogo enyi wana maana mwaniapisha na miye naapa simo, tena simo kabisaa sihusiki!

Kisha kwa vile tulihitaji kutengeneza “taifa moja”, amri ikatolewa kwamba “lugha ya taifa” ni Kiswahili na kwamba kwenye taasisi zote za umma (ikiwemo mashule, hospitali na kwingineko) lugha ya mawasiliano itakuwa Kiswahili. Masomo yakawa yakifundishwa kwa Kiswahili na walau moja ya faida walizokuwa nazo wale waliomaliza Darasa la saba ni uwezo wa kuelewa na kuzungumza Kiswahili; ingawa kusema kweli hawakuweza kukichalaza kama cha Mheshimiwa Mwenyekiti wa CCM taifa, na miye humu nahusikaje!? Simo nasema. Kule kwa wala Senene hadi leo bado wanapata taabu kutamka Ng’ombe na kusema kweli “ukiwaganganiza” kutamka Ng’ombe, mke nenda naye mahari imeshindikana kulipwa, ama unataka nikwambie Wakurya na Mama Ghati anayeuza “Ujhi” wa moto!!?. Nasema mnitoe humu maana sihusiki. Kiswahili iliposimamiwa kuwa lugha ya Taifa letu, leo Watanzania hatuulizani makabila tunapokutana, lahaja zetu tu ndizo husema huyu ni Mmakunduchi, huyu Muha na huyu ‘Njomba Nchumali, Ntoto wa Chumuni, na bila shaka huyu atakuwa “Niangusage sambi sako mwenyewe” lakini ilikuwa ukimaliza darasa la saba unaweza kuzungumza “kitanzania” asomaye na fahamu, mimi hizi ni salaam tu nawasalimia.

Zilipoanzishwa ‘spesho skuli’ za Wavulana na Wasichana kama Bwiru, Tabora na Mtwara, ilikuwa pamoja na kuwaleta watu wa makabila, mila, tamaduni na desturi tofauti mahala pamoja kwa miaka minne, kwa vile iliaminika kwamba watakapoondoka, utamaduni mpya utakuwa umezaliwa , utamaduni wa kitanzania. Kisha kuna kile kilichokuwa kikifundishwa (content) ambacho ingawa sehemu kubwa kilikuwa na maandalio ya mkoloni, lakini ufundishaji wake na mazingira yake walau yalitusaidia kupata watanzania kama ilivyo leo.

Kisha tukaanza kutengeneza “Watanzania” literally kwa kuhakikisha kwamba Mulangira anakutana na Manka kupitia JKT au amepangwa na Musubhati kwenye kituo kimoja cha kazi kule Nakapanya na hivyo mtoto anayezaliwa anakuta humo ndani kinachozungumzwa ni “Kitanzania” na hivyo wawili hawa hawana budi ila kuzaa “Mnyamahanga” au “Chasaka” ambaye hasa huyu ndiye alikuwa Mtanzania na japo kusema kweli sina nijualo, hizi ni salaam nawasalimia.

Ni kwa msingi huo, na kwa sababu pia kwamba uongozi unazaliwa na kutengenezwa kutegemea na nini kimetangulia chenzie, tunahitaji kuanza upya kwa kuwa na “shule maalumu” tena za msingi na sekondari na mara hii nashauri “Paramilitary schools” kwa sababu nyingi tu (labda nitaweza kuandika zaidi huko mbeleni), lakini ni muhimu walau kila kanda au kila Brigade iwe na shule ya msingi na sekondari inayoendeshwa na majeshi yetu na ambayo kazi yake itakuwa ni kutengeneza special breeds kwa ajili ya Tanzania ya miaka 30-50 ijayo. Pamoja na haya, nadhani tuondoe kwenye shule zote historia zilizoandikwa na wakoloni na kutumia historia zilizoandikwa na sisi wenyewe, wanetu waambiwe historia ya miaka 100 ya kupigania uhuru wa bendera hadi sasa, waambiwe mashujaa wetu, waambiwe maumivu, majeraha na uchungu wetu, waambiwe ushindi na mafanikio yetu, warithishwe ndoto za kesho yetu. Ikiwa Wakoloni walifaulu kwa miaka 50 tu kufuta kabisa historia ya babu zetu kabla ya ukoloni, na kutuaminisha kwamba Waafrika hatukuwa utamaduni wenye nguvu kabla ya wao “kutugundua”, tunashindwa nini kuwaaminisha wanetu tofauti kwa kupitia mfumo wetu wa elimu!!?.

Nisikuchosheni maana najua “mambo ni mengi na muda ni mchache, lakini ni maoni yangu kwamba wakati huu, pamoja na kuandaa mitaala “ya kitaalamu”, nadhani wote kama jamii tuje pamoja, tume zinazofanya mambo haya zianzishe midahalo na makongamano na kuvuna maoni na mawazo ya Watanzania wenyewe juu ya kile wanachokitaka kwenye elimu ya watoto wao baada yao, badala ya “wataalamu” kujifungia ndani na kuja na mitaala ya “kitaalamu” kwa vile wameshalamba posho zao liwalo na liwe. Watanzania wasio na “utaalamu” hata kidogo, wanajua kinachowastahili watoto wao kwa ajili ya kesho kwa sababu hata hivyo, wengi wa “Mashimba” sisi tusiosoma na tusio na utaalamu hata kidogo, tunao ujuzi na uzoefu kutoka kushindana na kule tulikotoka hadi kukaa meza moja kwenye majumba ya mashauri pamoja na “wasomi” wenye degree nyingi kuliko thermometer, na wengi wetu ndiyo tunaoendesha biashara na uchumi kwa kilimo na ufugaji, matokeo yanapaswa kusema zaidi kuliko makaratasi asomaye na afahamu, mimi hizi ni salaam tu nawasalimia!. Wasalaam!
Maelezo mengi hakuna la maana tangu tumebadili kipi kimetokea

USSR
 
Umesoma somo la misingi ya mitaala chuoni au nazungumza na bwege fulani

USSR
Mbona Makasiriko mengi sana!!? Huwezi kujenga na kuhoji hoja zako bila kashfa wala mitusi!!! Degree ya kwanza kabisa ilitolewa na asiye na Degree, kwa hiyo kunq tofauti ya "kusoma", kuelewa na kuelimika na inaonekana katika jinsi mtu anavyojiheshimu mbele ya wenzake
 
Back
Top Bottom