mabuba
Senior Member
- Dec 5, 2006
- 133
- 90
Tumeliachia soko wanetu
Malezi ni msingi wa elimu kwa vijana wetu. Tokea mfumo wa soko huria malezi ya watoto wetu tumeliachia soko liwalee. Ni aibu kwa Taifa letu. Msingi uliokuwepo hapo kale wa kufanya mtoto zao la jamii umeshindiliwa msumari wa moto na soko huria. Sasa mtoto analelewa na soko.
Walimu wamepunguza malezi kwa wanafunzi kwasababu, wazazi tumewasusa watoto. Walimu hawajivunii tena kuwa na wanafunzi bora, bali huona kuwa na bora wanafunzi ili mkono uingie kinywani. Tumeliachia soko wanetu ngoja litulelee.
Wazazi, wamewasusa watoto wao wa kuwazaa, wazazi hatufuatilii maisha ya wanetu, mtoto tokea aanze shule mzazi hajawahi kufika huko shuleni. Mzazi hajawahi kukagua hata siku moja daftari la mwanae anapotoka shule, mzazi huyu huyu hajui mwanae hafiki shule, mzazi huyu huyu hajui kuwa mwanae sasa amejiingiza kwenye matumizi ya dawa za kulevya. Mzazi huyu ndie anayempatia mtoto nauli ya kwenda shule, na mtoto anageuza nauli ile, pesa ya kununulua mzigo. Tumeliachia soko wanetu ngoja litulelee.
Serikali za vitingoji, mitaa, vijiji, kata, tarafa, wilaya, mkoa na Taifa. Wanaona watoto wanaharibika lakini kimya. Watoto wanashinda mitaani kwetu pasipo kwenda shule, lakini viongozi wa mtaa husika huona haiwahusu, sio watoto wa mtaa wao. Tumeliachia soko wanetu ngoja litulelee.
Ni mimi tu kuwakumbusha hii habari.
Mabuba FKM