Tumekutana Instagram, amenitumia nauli niende kisiwa cha Malta tuonane

Yaan negative comment ni nyingi
Kuna kitu kinaitwa grooming kuna uwezekano mkubwa atakuwa anapangwa, kuna documentary moja niliiona nafikiri ni Aljazeera, ni binti mdogo miaka chini ya 20 , alikutana na mtu online wakaanzisha mahusiano, binti alikuwa Uingereza, jamaa yupo Syria na ni mpambanaji wa ISIS. Sasa mahusiano yalivyopamba moto binti akatoroka Uingereza kwa kutamani kuishi maisha ya Syria. Alivyofika kukuta mambo ni tofauti na matarajio akataka kurudi Uingereza, serikali nayo imekaza wanasema yeye ni tishio, ndio walikuwa wanamhoji analalamika, yupo tayari arudi hata kama mfungwa Uingereza☹️
images (1).png
 
Comment nyingi hapa hazitofautiani na wanakijiji wanapojadili kuhusu safari ya kwenda mjini kisha wengi wao wakashauriana kuwa bora wabaki kijijini kwa kuwa mjini kuna magari mengi barabarani hivyo ukifika huko utagongwa tu!

We jamaa nenda Malta. Kwenye hiyo akili iliyokuwezesha kumfanya mtu kukutumia pesa kwa hiari yake, ongezea upeo kidogo sepa kasake maisha ughaibuni kisha wekeza nyumbani.
 
Usiogope bana, kama mmeongea mtandaoni kwa muda wa kutosha wewe pekee ndio unaweza kujua kama umwamini huyo binti au la...hata Tanzania mbona kuna watu wamepotea kwenye mazingira ya kutatanisha na wengine walikuwa wanaibuka kwenye viroba, kwani unaogopa kukaa Tanzania ?....japo sipendelei sana kuanzisha mahusiano ya kirafiki/kimapenzi kwenye mitandao lakini najaribu kuwa open minded, wewe pekee ndio unaweza kujua kama kuna viashiria vyovyote vinavyoonyesha kwamba unajipeleka kwenye mdomo wa mamba.
maelezo yako ni sawa na wale wanaopima ukimwi kwa kumuangalia mtu alivyonenepa.
 
Naomba uage kabisa ndugu jamaa na marafiki; mali zako gawa kabisa wasije wakagombania ndugu. Usisahau kutuonesha eneo la kaburi, unataka iwe wapi. Hizi ni dalili za kunyonywa damu mwisho wa mwaka.

Mabinti wa Bongo milioni 27 huwaoni!??? Kweli mapenzi kipofu!!!
😂😂😂😂😂😂
 
Sema mim nimemuamini kwa sababu ni mdogo, pia tunapochat kupitia video call anakuwa free na hata kama nikimwambia nionyeshe sehemu fulani ya mwili ananionyesha,pia ananionyesha mpaka chuo alipo akiwa darasan ,akienda hostel ananionyesha,akienda beach na marafiki mpaka anawapa na sim wananisalimia kwa video,wawapo matembezini mjini,sjui lakini mimi nahisi mtoto yupo serious na Mimi na yupo in deep love
Tamaa mbele mauti nyuma .Mapenzi yapo sikatii lakini angalikuja yeye mwanzo baba kamkataza mbona haiingii akilini yy ni Mmalta original au ni mgeni tu miezi 5 ni kidogo sana kumjua mgeni ww endelea kuchat nae na hiyo pesa mrejeshee kwa west union.
 
Nisikilize mm sasa ww nenda mkuu usijali wala nn mbona Wana wengi washafanya hivyo Ila jaribu kuisoma zaidi hiyo sehemu Maisha Yao, tamaduni , Hali za kiuchumi na kadhalika km Maisha Yao si ghali na kuna fursa unaweza kujaribu Maisha Huko.
 
Sema mim nimemuamini kwa sababu ni mdogo, pia tunapochat kupitia video call anakuwa free na hata kama nikimwambia nionyeshe sehemu fulani ya mwili ananionyesha,pia ananionyesha mpaka chuo alipo akiwa darasan ,akienda hostel ananionyesha,akienda beach na marafiki mpaka anawapa na sim wananisalimia kwa video,wawapo matembezini mjini,sjui lakini mimi nahisi mtoto yupo serious na Mimi na yupo in deep love
Una umri gani?
 
😂😂😂😂

Mkuu amka toka usingizin, habari kubwa hapa bongo NI hamphrey polepole kaitwa ktk tume ya maadil ya chama,

na wiki lijalo NI Xmas..izi ndoto zitakupoteza Safari yakuushinda umaskin Bado NI ndefu
hhahahaha
 
Back
Top Bottom