Tumekosana na rafiki baada ya kumuokoa mkewe

Tumekosana na rafiki baada ya kumuokoa mkewe

mathew chance

New Member
Joined
Apr 21, 2015
Posts
4
Reaction score
7
Viongozi husikeni na somo hapo juu.

Rafiki yangu tulieshibana sana alipewa dawa na mchepuko wake akamuwekee mkewe kwenye chai au kinywaji chochote
Alidanganywa na mchepuko huo kuwa dawa hiyo ni kwa ajili ya kumthibiti mke asiwafuatilie kabisa kwenye mambo yao na haina madhara yoyote.

Wiki baada ya kufanya kitendo hicho mkewe alianza kuugua mfululizo, hakawa hatembei ni wa kubebwa tu, akavimba miguu na usoni ndugu walihangaika bila mafanikio. Mshkaji sasa akahamia kwa mchepuko akapotea home mm na yeye tukawa tunaonana town tu.

Mimi nikaona huruma maana mwaka mzima akawa kitandani tu nikaona niwaambie ukweli wazazi wa mkewe walishangaa sana hawakuamini ndipo wakaamua kutafuta tiba mbadala baada ya mimi kuwafunulia ukweli. Sasa hivi amepona bado miguu haijawa na nguvu sana lakini anaendelea vizuri anahuzuria ceragem.

Sasa kinyume na makubaliano yetu kwamba asinitaje kama mm ndo niliwastua kampigia simu jamaa na kumuita mchawi kwamba hawampati tena wamemshindwa ana mungu na akanitaja live kwa mshkaji. Infact sasa hivi kuna mgogoro mkubwa kati yao wakituhumiana uchawi.

Mimi na yule jamaa sasa ni paka na panya, tena kadai mimi na mkewe ni wapenzi kwamba imekuaje hadi nitoe siri kama hiyo kwa mkewe na mkewe kwa hasira siku moja kampigia simu jamaa kamwambia na hivyo unavyodai natembea na rafiki yako ni kweli sasa natembea nae sema unataka nini na maneno mengine mengi.Yaani wakuu tulipofikia na huyu jamaa as hivi tunatishiana maisha yeye na mchepuko wananitishia maisha.

Naombeni ushauri wenu
 
Wanawake hawana kifua wala moyo mpana wa kuhifadhi mambo...bora ungewaambia wazazi wake tu na kuwapa hiyo precaution..
 
kwanza umefanya dhambi ya kushiriki na huyo jamaa yaan hapo ni kama tu umefanya wewe, dhambi ya pili kuchelewa kusema. cha msingi hapo ni kutubu kwa mungu kwamba ww ndo umefanya hayo, na kuhusu kukutishia na inaonekana wanakutishia kwa uchawi, njia ya pekee ni ww kuingia kwa yesu, fanya hayo haraka
 
mmmh kwa nini usiwatumie tena hao wazazi wakamfunga mdomo binti yao...ila kama ukiona haachi nenda mahakamani kawashitaki kwa kuvunja makubaliano ya mkataba wa kutosema!
 
Jamani ni lini wanaume wenzangu mtakubaliana na kibonde????????????? MICHEPUKO SIYO DILI>>>OVER
 
Pole kwa yaliyokukuta kwanza nikutoe hofu umefanya kazi kubwa sana ya kuokoa maisha yaa mtu,pili unatakiwa utubu dhambi uliyoifanya yakushiriki kumtesa binadam bila huruma,usiwe na hofu kuhusu usalama wako kwa maana mungu atakulinda nawe utashinda lakini utakiwi kuwa na vita na iyo familia ata kidogo na utakiwi kujutia uamuzi wako kwani huyo shemeji aidha angekufa kwa utesi wenu wa kiuchawi nawe pia mhusika,xx chakufanya ni kukaa na wazazi wa huyo mwanaume nakuwaeleza ukweli wajue jinsi ya kumkomboa uyo rafiki yako.


Kwa maana uyo rafiki yako kashatekwa na mambo ya kichawi kwani huo mchepuko km umeweza kumfanyia jambo baya mke wa rafiki yako na akafanikiwa xx atashindwa nn kumzibiti uyo rafiki yako kwa maana uyo jamaa sio akili yake tena,huo mchepuko ni hatari sana,unajua kwann familia ya mke wa rafiki yako awajaweza kutunza siri kwa sababu ww pia muhusika ndio maana wameshindwa kukaa na siri,

Kwann nasema ivyo ni iv wakati unawahambia siri iyo walikuaid awataweza kusema sababu wanashida xx washapata ufumbuzi iyo shida ndio maana unaona wanajibizana na rafiki yako sababu wanajua awawezi tena kufanywa llt kuna usemi usema mtu ukijua jina hakupi tena shida jalibu kufanya ivyo ndugu
 
umeona ee huyu nae muuaji kweli kakaa kimya wakati mwenzie anateseka
ndiyo maana yake angetakiwa kusema mapema kuliko mama kateseka na ndugu zake kuhangaika hospital .. wamepoteza hela nyingi na mda huku wakijua wamemkorogea lisumu mwenzie hatari sana
 
Hahaha umeona eeh. Na dada wa watu keshamuombea waiver or excemption. Hakuna namna hapo

Na hadi jamaa kuchagua side ya mke dhidi ya best wake kwa vyovyote kuna emotions zilizojificha..
halafu rafiki wa kuua mkewe wa nini?
 
Mtafune huyo mwanamke ili kulinda heshima
 
Mwanamke ukitaka asiropoke basi usimwambie kua hiyo ni siri na asimwambie mtu utaharibu.
 
Unaonekana hiyo sumu ilikuwa na Mambo ya ushirikina ndani yake, sumu gani haiponi kwa dawa za hospital?
Anyway, ndoa za siku hizi zina changamoto sana ....wanawake ndio wanaongoza kwenda kwa waganga...hata huyo rafiki wa jamaa katekwa kimazingara sio bure!
 
Back
Top Bottom