Tumekataa matokeo kituo kwa kituo. Uvivu wetu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tumekataa matokeo kituo kwa kituo. Uvivu wetu

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mdanganywa, Nov 2, 2010.

 1. M

  Mdanganywa JF-Expert Member

  #1
  Nov 2, 2010
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 542
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 60
  Wote tumeponzwa na uvivu wetu wa kupenda kujumlishiwa matokeo na Tume. Matokeo yake hata yalipochelewa hakuna aliyekuwa anaweza kusema fulani ana kiasi gani hata kufanya kauli "lete data" itawale kwa wingi.

  Munkari kwa matokeo ya ubunge unapungua kadiri wanavyotangazwa.

  Lakini matokeo ya urais tunapiga porojo nyingi wakati tungekuwa tumejiandaa kupata kituo hadi kituo basi JF ina wtalaamu wa kila aina na kwa maesabu yao tungekuwa tunaongea lugha yetu.

  Kwa sababu tumeruhusu uvivu kuhusu hilo tukae kimya tusubiri wachakachue wanavyotaka. Na uwezo wa kuchakachua watakuwa nayo kwani hakuna mmoja wetu anayeweza kusema ni kituo kipi kilichakachuliwa.

  Si kwamba wazo la matokeo ya kituo kwa kituo halikuletwa. Liimeletwa, tukalipuuzia na hakuna anayelichangamkia kila linapojitokeza.

  Ukitaka kuhakikisha angalia thread zote zilizosisitiza suala la matokeo ya kituo kwa kituo. Hatushishambulii. Hakuna hata moja iliyozidi page mbili au tuseme 10 responses. Lakini thread za tetesi zipo zilizozidi zimezidi page 15!

  Ona kama hii {https://www.jamiiforums.com/results-matokeo/83377-kujumlisha-matokeo-kunatushinda-tuweze-nini-duniani.html}

  Na nyingine ni hii { https://www.jamiiforums.com/results-matokeo/83558-poor-media-houses-and-journalists.html}

  Hapo ndipo unapoweza kutupima uwezo wetu wa priorities, kama vile unavyoweza kutupima kwa priorities za kupenda kurundikana kwenye viko vya harusi wakati wenzetu wanarundikana kwenye harambee za kujenga shule.

  TUmejiadhibu wenyewe na Tume ya Uchaguzi wana akili sana maana wanatujua akili zetu zitakakokibilia. Hakika wamefaulu!
   
 2. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #2
  Nov 2, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Subiri uone shughuli itakayofuata baada ya hii sinema ya tume ya uchaguzi
   
 3. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #3
  Nov 2, 2010
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  I Beg to differ kwenye hiyo point yako ya mwisho.

  Tume ya Uchaguzi hawana akili yeyote katika kufanya yote haya wayafanyayo, wanapigishwa Joyce Wow wow wow na CCM. Ni puppet wa CCM.

  Mara nyingi mahali pengi duniani Wezi,Wnyang'anyi na hata wauaji wanaitwa watu wenye akili. This is more than being Wrong

  Watu wanao tumia hila zote kujineemesha katika nafasi zao wanaitwa wenye akili au wajanja, pia watu waliochangamka.
  Kifupi watu waovu wakusanyao mali zilizo katika form zote kuanzia fedha mpaka mamraka ya kufanya lolote kinyume cha Kanuni Sheria na taratibu wanaitwa watu wenye akili.
  Kinyume chake watu wenye maadili, malemgo ya muda mrefu waadilifu watu wa kiasi na wasio walafi jamii imewabatiza jina la kutokuwa na akili vilaza aua mabwege. Kuna watu wenye nafasi kubwa kabisa serikali kwa masikio yangu mwenyewe niliwasikia wakisema Mwalimu Nyerere alikfa masikini kwa sbabu alikuwa mjinga na Mbinafsi. Wakashau kwamba bila yeye wasingali soma hadi chuo kikuu bure kwani angetaka kusomesha Watu wa Musoma pekee yao asingeshindwa kufanya hivyo hata kidogo.

  Kifupi tume ya Uchaguzi ina watu waliosoma sana lakini wanafanya mambo ya mtu asiye na akili hata kidogo. Wnashindwa kusoma alama za nyakati. Wanadhani wataendelea kujificha chini ya kivuli cha CCM na CCM wataendelea kijificha Chini ya Mwavuli wauitao AMANI NA UTULIVU.
  Ni wasomi, ni watu waliomakini katika sheria, lakini wanatumiwa kama ya ndani na CCM

  Mengine yote uliyosema nakuunga mkono.

  Hapa JF tuna watu wana vichwa kweli kweli, tatizo kama uliovyosema hatukujiandaa kuleta matokeo ya kituo kwa kituo.
  Hata hivyo hatujachelewa. Mara ujuapo makosa yako unaanzakujisahihisha mara moja.

  Hii ni sawa na kuandika Software, ukijaribu ku compile function ikagoma unarudi nyuma unaanza kuangalia mstari kwa mstari kuona kama kuna logic za kutosha kisha unakwenda kunangalia je umeiita function kwa jina lake au Function inaitwa Yohana wewe unaiita kwa jina la Yahya??

  Wakati tunapiga uchaka Kule Mafinga JKT miaka ya 80 tulijifunza mbinu za kushambulia na kuregroup na kutathmini shambulia kabla ya kuanzisha shambulio jipya au kuwithdraw.

  Naamini kabisa ndani ya Chadema au hapa JF mtu fulani mwenye Access anafanya zoezi hilo.
   
 4. M

  Malunde JF-Expert Member

  #4
  Nov 2, 2010
  Joined: Jun 16, 2010
  Messages: 311
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45


  Huu ni wito, mtu anayeweza atuwekee, hatujachelewa.
   
 5. k

  kingwipa1 JF-Expert Member

  #5
  Nov 2, 2010
  Joined: Jul 2, 2008
  Messages: 335
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Madela Wa-Madilu,
  Umenena mkuu.
   
Loading...