Tumeingizwa mkenge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tumeingizwa mkenge

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mlalahoi, Feb 17, 2010.

 1. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #1
  Feb 17, 2010
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,066
  Likes Received: 393
  Trophy Points: 180
  Kwa mujibu wa taarifa ya kiuchunguzi ya kipindi cha Newsnight BBC2,kuna habari kwamba teknolojia ya ugunduzi wa mabomu,madawa ya kulevya,nk kwa kutumia kifaa kiitwacho GT200 ni feki na tayari serikali ya Thailand imechukua hatua ya kusitisha ununuzi wa kifaa hicho.Wataalam mbalimbali wa milipuko waliohojiwa na Newsnight wamethibitisha kuwa kifaa hicho hakina uwezo wa kugundua mabomu,drugs,nk na kampuni inayojihusisha na uzalishaji/uuzaji wake ni sawa na matapeli.Pia serikali ya Uingereza imepiga marufuku exportation ya kifaa hicho.

  Taarifa zinaonyesha kuwa kuna nchi mbalimbali zilizonunua kifaa hicho ikiwa ni pamoja na TANZANIA ambapo kimekuwa kikitumika kupambana na ujangili wa nyara ( link hii HAPA)

  Bei ya unit moja ni paundi za Kiingereza 22,000 lakini haifahamiki sie tulinunua units ngapi,excluding the usual teni pasenti.
   
Loading...