Tumeichoka TCRA, ni geresha tu hatuitaki

Tumeichoka TCRA, ni geresha tu hatuitaki

Yusomwasha

JF-Expert Member
Joined
Dec 5, 2014
Posts
2,092
Reaction score
844
Nashindwa kuandika hapa kwa hasira dhidi ya TCRA. Hebu angalia vingamuzi vinapanda gharama za kulipia everyday, local channel hakuna mpaka ulipie. Hili ni jipu tena hatuitaki tena wameshindwa kazi!

Serikali iishughulikie TCRA. Mamia ya barua yameandikwa kwa TCRA kuhusu vingamuzi lakini wapo kimya. Narudia tena TCRA ni chombo cha makampuni ya mawasiliano na si watanzania. Ni kama geresha tu hatuitaki!
 
Hao ni majipu tu, hawana faida kwa watanzania.Ifutwe tu FULL STOP
 
Utangazaji uko katika mifumo minne:

1. Satelitte Free to Air na Satelite kwa Subscription.

A: Free to air unanunua na kufunga dish lako na unapata channel zote za bure zilizoko kwenye satelaiti, ili mradi vituo husika viko hewani bure.

B: Satellite by Subscription (Huduma za Malipo) ambapo DSTV, AZAM Na ZUKU wamo! Ili kuona matangazo humu lazima ulipie. Free to air kuwemo ni offer ya kampuni na fedha ikiisha channel local za kitaifa haziinekani.

2. Cable Tv Z Broadcasting, Mfumo Huu ni wa malipo Na channel za bure 5 za kitaifa utaziona ukiwa umelipa tu.

3. IPTV Tv Broadcasting, njia ya matangazo kupitia internet. Zipo huduma za bure na za kulipia.

4. Terrestrial Tv Broadcadting (Mifumo iliyosimikwa juu ya ardhi). Mfumo Huu ndio mfumo mpya wa utangazaji ambao Local channel Za kitaifa 5 zinapaswa kuoneshwa bure. Analojia ilivyozimwa waliingia MUX operator watatu wenye ving'amuzi vinne, Agape, Basic Transmission (Continental na Digiteck), Star Times. Hawa ndio kwa mujibu wa sheria na Kanuni za Utangazaji wanapaswa kuonesha channel 5 zenye leseni za kitaifa bure.

ZUKU, AZAM na DSTV wakiziweka ni "added value" baada ya kukubaliana na wenyewe! Lakini ukiushiwa fedha huwezi kuona bure! Hii ni business model ingine na tulitoa ufafanuzi vizuri kabisa! Satellite haikubadilika kwani siku zote wako digital.
 
Wakati wa huduma za bure unayoyoma. Channeli ya kitaifa ni TBC tu hizo zingine zinafanya biashara
 
Back
Top Bottom