Hivi TCRA mnatunga sheria kwa sababu ya kumsaidia mwananchi au kumkomoa

Wazolee

JF-Expert Member
Sep 1, 2018
2,699
3,088
Kuna mwananchi amevamiwa na vibaka ameporwa mkoba wake ndani yake mna laini zake za simu na vitambulisho vyake amenda kurudisha imeshindikana kwa kuwa hana kitambulisho.

Sheria ya TCRA ili urudishe laini yako iliyopotea lazima uwe na kitambulisho barua ya serikali ya mta haikubaliki
Kibaya zaidi katika laini ya Tigo mna laki 5 na katika Voda mna laki 7

Ameshindwa kuzirudisha kwa kuwa aliibiwa kila kitu.

Sasa hi sheria ya TCRA hapa ina muumiza nani Tigo,Voda, kibaka aliyeiba au Raia mwema aliyeibiwa vitu vyake

Jibu anaeumia hapa ni raia mwema ambaye vibaka wamemuibia vitu vyake na TCRA wameweka sheria ya Kumkomoa ili asivipate tena vitu vyake na wamewaambia mitandao ya simu wakimrudishia mtu laini ambae hana kitambulisho faini dola 500
Mambo yake yote yamesimama mwezi sasa umeisha inauma sana

Hana alternative way hana pa kwenda ni kwa sababu ya sheria zilizo wekwa na TCRA kana kwamba wametunga hizi sheria kwa ajili ya wakimbizi kumbe ni kwa ajili ya watanzania walipa kodi zinazowalipa mishahara yao

Nahisi kama wanahitaji kurudi shule mimi siamini kama mtu aliye elimika anaweza kutunga sheria kama hizi

Maana hata katika ving'amuzi ndio hivyo hivyo eti wananchi wenye ving'amuzi vya Kulipia hawaruhusiwi kuona local channel
 
Labda ajaribu kupata barua ya utambulisho kutoka serikali ya mtaa wake awapeleke

Ova
 
Haya wewe ulieelimika kuliko hao TCRA
 
Tz karibu kila jambo ili kutengeneza mazingira ya rushwa.
 
Unalaumu TCRA bure hapa wenye tatizo ni nida wanatakiw watoe kitambulisho kwa wakati au process ya kupata kitambulisho kilichopotea iwe rahisi. Wizi wa simu unaenda mwisho lazima tuelewe dunia ya sasa mambo yaa short cut yanakishwa.
 
Back
Top Bottom