Rufiji
Platinum Member
- Jun 18, 2006
- 1,952
- 1,153
Wanasayansi wa mambo ya afya wanapotafutaga dawa ya kutibu ugonjwa fulani, mara nyingi wanatumia muda mwingi kujifunza juu ya wadudu wanaosababisha ugonjwa. Watajifunza juu ya hao wadudu wanavyoishi na vitu gani wanaweza kufanya katika kuyaharibu maisha yao. Mimi nadhani sisi Watanzania inabidi tujifunze kitu kutoka kwa hawa wataalamu! Ni lazima tutafute chanzo cha hili tatizo, ili tuweze kulitatua. Na ndio maana nauliza tumefika-fika vipi hapa? Nadhani hilo swali ni muhimu na kila anayelitakia mema taifa letu la Tanzania inabidi ajiulize. Kuendelea kutoa kauli kama za kina Mheshimiwa Rais na Maggid hazitatatua kitu. Ni lazima tukae chini kama watu wazima tujiulize maswali ya msingi, mbona hatukuwa na hayo matatizo huko nyuma? Je Wakristo hawakuwepo huko Zanzibar?