Tumedhulumiwa ardhi hivi hivi

Abraham Moshi

Member
Jan 16, 2012
20
8
Naomba ufafanuzi kujua haki itatendekaje ili tuweze kupata ardhi yetu, iliyouzwa na mwanaume aliyekuwa anaishi na marehemu dada yetu. Huu mji tulikuwa tunaishi sisi familia baadaye wazazi wetu wakahamia maeneo ya mashambani dada yangu na huyo mwanaume wakawashauri wazazi kwamba, huu mji wautengeneze iwe sehemu ya biashara ya familia wazazi wakakubali wakaanza ujenzi baadaye mzazi wetu akataka kushughulikia lease ya hilo eneo, dada yangu akamwambia mzazi wetu kwamba asihangaike atashughulikia yeye na huyo mwanaume wake, mzazi akakubali akawaachia wafuatilie lease mpaka ikapatikana. lakini imeandikwa jina la dada na huyo mwanaume mzazi akauliza mbona mumebadlisha jina la mmiliki dada yangu akamwambia, wamefanya vile ili yule mwanaume afanye mpango wa kukopea pesa benki na wakimaliza kulipa deni la benki watakwenda kubadilisha jina la mmiliki. Kifamilia hatukubaliana na ujanja iliofanyika wakati mchakato unaendelea kwa bahati mbaya dada yetu ameugua na amefariki dunia. mwanaume hajazungumzia lolote juu ya hili eneo alichofanya ametafuta mteja na kuliuza. Naombeni mchango wenu wa mawazo na kisheria
 
Wapo watakuja pole sana mimi nasisitiza usikae umwamini mtu hata mume /mke kuwa mjanja sana POSSIBLY NINAWASIWASI NAHICHO KIFO CHA DADAYAKO INAWEZEKAN ANAHUSIKA
 
Wapo watakuja pole sana mimi nasisitiza usikae umwamini mtu hata mume /mke kuwa mjanja sana POSSIBLY NINAWASIWASI NAHICHO KIFO CHA DADAYAKO INAWEZEKAN ANAHUSIKA

Hata mimi nina wasiwasi Mkuu
 
Poleni sana kwa msiba. Ngoja waje watu wa Sheria watakusaidia sana
 
Back
Top Bottom