TUMEDANGANYWA NA UTANDAWAZI (media) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TUMEDANGANYWA NA UTANDAWAZI (media)

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Tabutupu, Dec 26, 2010.

 1. Tabutupu

  Tabutupu JF-Expert Member

  #1
  Dec 26, 2010
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 5,650
  Likes Received: 4,412
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  TUMEDANGANYWA NA UTANDAWAZI

  1. Hivi ni kweli kuwa kila tunacho kiona kwenye medi ndio maisha halisi ya Mzungu .
  2. Je kuna umihimu wowote kuendeleza tamaduni zetu ambazo tuliachiwa na babu zetu.

  Mi e binafsi naona kama tunajidanganya kwani mara nyingi tumeingizwa mkenge kwa kutokujua kwanini tunafanya vile. Kila kitu kinacho fanywa na binadamu kina maana kwake. Mungu alituumba weusi kwa sababu zake na hakukosea ( acheni mikorogo).

  Wazo mcharuko
  1. Kuna wanawake wanafikiri kuvaa suruali ni kwenda na wakati (Ati uonekana ni mwanamke wa kizungu) na si vazi ambalo wanalivaa kwa sababuza msingi wakati huohuo kuna wanaume kamwe hawata oa mwanamke ambaye anava suruali wakiamini kuwa ni ishara ya tabia mbaya.

  2. Kuna wanawake wanaamini kuto vaa kimini ni kuto kwenda na wakati na kuna wanaume wapo wanao amini mwanamke akivaa kimini mi mhuni (Ati nafsi zao zinaumizwa).

  3. Kuna binadamu wanaamini wakijichubua ndio wanakuwa binadamu wa kweli ( wazungu).

  4. Wapo vijana ambao wanaamini kutofanya mapenzi hadi ndoa ni ushamba mkubwa .

  5. Kuna binadamu wanaamini kuwa kutoka ndani ya ndoa ni kitu cha kawaida ili mradi mume au mke asijue eti kwa kuwa kwa wazungu sio issue ( eti wazungu ndio walivyo).

  6. Kubwa zaidi ni kuwa tumefika hadi kutojali watoto wanapo kosea na kujiingiza katika mapenzi na hata tumeona ni kitu cha kawaida . Sipingani na hio ila kwa ni tusiwe fundishe moral values wajue kabisa kufanya mapenzi hairuhusiwi hadi aoe au aolewe.

  Yapo mengi ambayo kutokana na kuzing'ang'ania desturi za kigeni tumejikuta tukifanya mambo ambayo hata wenyewe tunao wasingizia wanafanya hawafanyi.

  Je Tunacho kiona katika media ni kweli ndio uhalisia wa maisha tunayo takiwa tuyaishi au ni kweli kwamaba mara nyingi vitu vya onyo onyo ndivyo vinavyo pendwa na na jamii.

  [​IMG]
   
 2. Gurta

  Gurta JF-Expert Member

  #2
  Dec 26, 2010
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 2,246
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Kudos

  Kweli tupu hii kitu. Ila mi nitachangia kwa hizi tamthili(y)a ambazo sku izi zimekuwa maarufu kweli. Imefikia pahala watu wanataka hata kuendesha maisha yao ya kimapenzi kufuata namna walivyoona kwenye tamthilia.
   
 3. baha

  baha Member

  #3
  Dec 26, 2010
  Joined: Oct 18, 2009
  Messages: 44
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Kwa bahati mbaya sana ume-address hayo kwa kuonesha kutoridhishwa nayo yote. Haujakosea kama hivyo ndivyo dhamiri yako imekuonesha. Nami kwa upande wangu sikubaliani na yote hayo na pia siyakatai yote. Ukweli ni kwamba siku zote kitu bora hupatikana katikati ya "continuum" au panapokuwa na "normal distribution" kwa lugha ya kitakwimu. Hii inamaanisha ya kwamba kitu chochote kilicho pembeni zaidi mara nyingi hakiwezi kutoa "reflection" ya "population" kwa maana tunaviita "outliers" ambavyo ni sharti virekebishwe ili kutegemea kupata uhalisia wa kitu. Hata hivyo kila mtu anaweza kusema kadri anavyofikiria juu ya hili kutegemea na "school of thought" aliyonayo.

  Kuangalia na kuiga si kitu kibaya hata siku moja. Hakuna binadamu aliyekisiwa kiasi cha kutoathiriwa na mazingira yake. Kwa hili la mazingira naomba liwe ndo utandawazi! Katika jamii inayohubiri utawala bora hili ni haki ya wananchi wake almradi hawavunji sheria. Uzuri wa mtu anaujua yeye mwenyewe. Mtu kutaka kujichubua ili awe kama mzungu haina tatizo kwa maana yeye ataka kuwa mzuri na hata hivyo hagombani na yeyote katika hilo. Tumia "logic" hii katika kujadili yote hayo mengine.

  Kwa upande wa nini mababu zetu walituachia nakubali lakini kwa sharti la kukaa mengine. Unataka ulazimishe mwanamke avae sketi na kujifunga kanga kisa mababu walisema? Kwangu mie huu ni utamaduni wa jamii ambao si lazima uwe sahihi sehemu zote na wakati wote. Nikukumbushe kama unafahamu au basi nikueleze kama hufahamu ya kuwa utamaduni unatokana na Falsafa, Jiografia na Historia na hubadilika kulingana na sehemu X na wakati Y. Kinachotakiwa kutumika katika kuamua bila kuangalia jamii fulani ni "Ethics" au maadili kama hili ni neno sahihi lenye kubeba maana pana ya neno hilo la kiingereza. Kinachoepukwa kuumiza uhuru wa mtu bila ya sababu ya msingi ni kutumia utamaduni fulani kama nanga ya maamuzi.

  Hata kama hutaki hayo yatendeke huwezi kuzuia kwa sheria na udhibiti wa nguvu bali uwezo wa kutongoza wahusika kisaikolojia kuchukua uelekeo "unaofaa" kwa kuweka machaguo mengi zaidi na rahisi kuyakwepa. Lazima ujiulize: Je, kufanya kitu au kutofanya kuna tofauti?
  Asante.
   
 4. Tabutupu

  Tabutupu JF-Expert Member

  #4
  Dec 26, 2010
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 5,650
  Likes Received: 4,412
  Trophy Points: 280
  Nashukuru kwa mawazo yako mazuri japo naona hujasoma vizuri kwani nimezungumzia mawazo ya watu sijalazimsisha. Inawezekana tupo sahihi lakini tatizo ni kuwa je tunajua nini kwa yale tunayo yafuata??. Ndio uhuru tunao wa kufanya kila tupendacho lakini, tusije kuwa tunafanya makosa kwa kkosa elimu au maarifa fulani. K

  Mfano, Nimeandika kama mwanamke atavaa suruali yake kwa sababu ni vazi la kawaida sioni tatizo, lakini akifanya hivyo ili aonekana mzungu , je ni sahihi. Na je Wanaume wanao wanaona wanawake kama hao ni kizazi kilicho potoka nao tuwasemeje??.
   
 5. baha

  baha Member

  #5
  Dec 26, 2010
  Joined: Oct 18, 2009
  Messages: 44
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Nilisoma vizuri lakini hiyo haimaanishi ungenielewa vizuri pia. Hata hivyo ndo maana ya majadiliano ili hatimaye tuelewane vizuri.
  Ndo maana nilimalizia kuuliza: kufanya au kutofanya kitu ilhali haibadili matokeo kuna tofauti? Mtazamo wangu ni kwamba, bila kujali mtu anafanya kitu fulani ama kwa kujua sana mwanzo wake au hajui kama haimdhuru yeye wala watu wengine basi hakuna tatizo katika hilo. Wanaume wanaohukumu kisa tu wanawake wanafanya wasiyotaka wanaume hawa basi ni kukosa uelewa wa kwamba kila mmoja ana uhuru ambao hautokani na utashi wa mtu mwingine awaye yote yule. Na kwa hili niko tayari hata kama sheria zetu zinazuia haya basi zirekebishwe ili watu wafurahie maisha ndani ya utawala bora.
   
 6. Tabutupu

  Tabutupu JF-Expert Member

  #6
  Dec 27, 2010
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 5,650
  Likes Received: 4,412
  Trophy Points: 280
  Hapo nimekupata .
  Lakini je tunaweza tukawa na taifa huru kiasi cha kuwa turekebishe sheria ili kila mtu afanye kile atakacho ili mradi kwke yeye ni sawa???
   
 7. baha

  baha Member

  #7
  Dec 27, 2010
  Joined: Oct 18, 2009
  Messages: 44
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Hicho haswaaa ndo kinachotakiwa almradi kitendo chenyewe hakimdhuru mtenda wala watu wengine
   
Loading...