Tumechoka kuumizwa!

bora yetu tunaumizwa kuliko nyie MNAJERUHI na kuacha makovu mioyoni mwa watu.
 
Ukweli ni kuwa both parts ni sawa kuwa wanaumizwa, but ninachojua ni kuwa mwanamke akimpenda mwanaume anampenda kiukweli, but kama mwanaume atapenda au mpenzi wako wa kiume akikupenda, basi jamii, rafiki hata ndugu zake watasema amepewa limbwata na maneno hayo yakizidi mna anaamua kupunguza kuonyesha kuwa anakupenda na kukujali ili tu watu wasimuone yuko crazy juu yako, aepuke kuitwa mume *****, mwanaume mwengine hata yeye mwenyewe akisikia habari za limbwata, anafikiri hata we umeshamwekea ndio maana anakupenda mno, akiwa mpumbavu, ataanza kupunguza kukupenda na kuishi na wewe kama rafiki zake wanavyomshauri, utasikia aah, hiyo cheni ya gharama hivyo unamnumnulia ya nini, si umeshamuoa, usijipe gharama kama ndio unamtongoza, wao yanawahusu nini, kama yeye na mkewe wamezoea kupeana zawadi mara kwa mara, waacheni waishi wanavyotaka, mwanaume mwingine akiwa mpumbavu ataacha kweli kununua hiyo cheni kwa ajili ya mkewe, halafu utakuta hao marafiki watataka uwanunulie bia kwa ile hela ya cheni au atakuambia ana shida anaomba umkopeshe hiyo hela, kumbe anaipeleka kwa kimada wake, pendeni wake zenu, ni mara chache sana nasikia mwanaume anasingiziwa anaenda kwa mganga ili mkewe ampende ila wanawake ndio kila kukicha, hata mume akifa wanasema mkewe ndiye kamuua, eeh mbona mwanamke akifa kabla ya mumewe, hamsemi hivyo hata kama ni kweli, wanataka mke ndio afe wa kwanza, ndivyo mlivyosema siku ya ndoa au, tupendane, tusiwajudge watu kiujumla sana kila mara, mtu anaweza kuwa tofauti na tabia ambazo watu wengine kutoka kabila, rika, dini au jinsia aliyopo, wamezoeleka kuwa nayo.
 

Du! Pole sana dear!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…