Tumechoka kuandamana (sms sent)

Tumechoka kuandamana (sms sent)

tofyo

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2013
Posts
2,759
Reaction score
768
Kwanza naomba mnielewe maandamano ni haki ya kisheria na sina mashaka na hilo.
Lakini inavyooneka suala la katiba limeshanunuliwa na wanasiasa.
Na kwavile wanasiasa hawaaminiki(rejea kauli ya ZITTO)
yawezekana wakawa waongo,walaghai,walubuni au waponzaji.
Tunaomba warudi mezani au kama wanataka kuandamana,basi waende wao na familia zao .
Tumeshaandamana sana lakini linapokuja suala la chai na juice ya magogoni tunajikuta tumerudi kulekule alikosema ZITTO.

Tulieni dawa iingie (by H.KIGWANGALA).
 
Wapenda mandamano njooni msome uzi huu yericko,ben saaanane na wengine wenye mawazo ya kuandamana na kufanya fujo.
 
Maandamano ni haki lakini pale yanaporuhusiwa kisheria.

Mkiandamana bila ruksa mtaishia kufariki na kuacha familia zenu vibaya uku wao wakienda kupoozwa kwa juice na chai magogoni.
 
Tatizo la wapinzani nao ni walewale, wakiitwa na ma interahamwe huko magogoni wanatia timu! Toka mwanzo hawakustahili kushiriki kwenye bunge hili lenye ma interahamwe wengi kuliko maelezo! Tatizo mshiko wa 300000 kwa siku.
 
Pole sana kwa kuchoka kuandamana. Wenzako kuhusu Katiba wala hatujaanza kuandamana bado, wewe umeshachoka. Tuna usongo. Tutaandamana hadi kieleweke kama itakuwa kwamba hiyo ndiyo njia pekee ya kupata Katiba ya Wananchi kama hali inavyoashiria sasa.
 
Kwanza naomba mnielewe maandamano ni haki ya kisheria na sina mashaka na hilo.

Lakini inavyooneka suala la katiba limesha nunuliwa na wanasiasa.

Na kwavile wanasiasa hawaaminiki(rejea kauli ya ZITTO)

yawezekana wakawa waongo,walaghai,walubuni au waponzaji.

Tunaomba warudi mezani au kama wanataka kuandamana,basi waende wao na familia zao .

Tumeshaandamana sana lakini linapoku suala la chai ya magogoni tunajikuta tumerudi kulekule alikosema ZITTO.

Tulia dawa iingie (by H.KIGWANGALA)

Kama umechoka wewe kalale upumzike utuachie sie wenye nguvu zetu tuandamane.. KANYAGA TWENDE UKAWA.
 
Maandamano ni haki lakini pale yanaporuhusiwa kisheria.

Mkiandamana bila ruksa mtaishia kufariki na kuacha familia zenu vibaya uku wao wakienda kupoozwa kwa juice na chai magogoni.

Sikujua kama uwezo wa fikra zako uko chini kiasi hiki. Wewe nenda kajadili mambo ya kina Wema na Diamond haya sio saizi yako. Ni ushauri tuu.

Sent from my iPad using JamiiForums
 
Watu wana usongo sana na maandamano hayo kinachosikitisha zaidi hawa walimu wapya wapo moto sana
 
Kwanza naomba mnielewe maandamano ni haki ya kisheria na sina mashaka na hilo.

Lakini inavyooneka suala la katiba limesha nunuliwa na wanasiasa.

Na kwavile wanasiasa hawaaminiki(rejea kauli ya ZITTO)

yawezekana wakawa waongo,walaghai,walubuni au waponzaji.

Tunaomba warudi mezani au kama wanataka kuandamana,basi waende wao na familia zao .

Tumeshaandamana sana lakini linapoku suala la chai ya magogoni tunajikuta tumerudi kulekule alikosema ZITTO.

Tulia dawa iingie (by H.KIGWANGALA)

Pengine unapoint ya maana lakini USHABIKI na utoto umeharibu maudhui ya bandiko lako... Maandamano hufanyika kwa ajili ya kufikisha ujumbe kwa walengwa ikiwemo Jamii ya kimataifa!! Kuandamana ni haki ya msingi kwa kila mwananchi wala haihitaji kibali kwani vyombo vya usalama kazi yao ni kusaidia maandamano yafanyike kwa amani... suala la Maridhiano (wewe unaita juicy) ni muhimu sana kwa ustawi wa Jamii yetu! Haiwezekani Rais wa watu million 5 akaacha kukaa meza moja na viongozi wenye kuwakilisha watu zaidi ya million 30! Nchi haitakuwa salama... Binafsi nawasifu hao waliokwenda kunywa juicy kwa maslahi ya wananchi wao!... Pasipo maridhiano umoja na utaifa wetu utatoweka kama nuru ya mchana wakati Giza linapoingia... I bet wewe huna mpenzi ama umeachika ndiyo maana huwezi kuona umuhimu wa ku - compromise ili mambo yaende mbele...
 
Hao viongozi wanaowakilisha watu milioni 30 ni wepi? Ni hawa hawa akina Mbatia, Lipumba na Mbowe ambao idadi ya wanachama na wafuasi wao hawazidi milioni tatu? Au una maana gani? Hakika siasa za kilaghai UKAWA zimewaponza. CCM tuko wengi ndani na nje ya bunge
 
usipotambua umuhimu wa maandamano utarazimika urudi shule.Maandamano yana umuhimu sana kuliko unavyofikiri na kuwaza.Nchi zenye demokrasia wanatambua umuhimu wake.watu wengi wanatoa majibu mepesi mno kuliko ukweli wenyewe.Niulize,wewe umekwenda kutoa maoni then maoni yako si chochote,hivyo wanaamua kuyazika na kutengeneza ya kwao.TUWAZE NA KUFIKIRI ZAIDI.
 
Compromise ipo bungeni.rudini mkamalizie wajibu wenu mliotumwa.
Hakika Mkuu, kwanza hawa wapinzani wajinga kweli. Wameshindwa kuchangia watu walioathirika na mafuriko halafu wanajifanya eti wanapeleka chama kwa wananchi.
 
Hizo ni fikra mgando,kama kweli unataka katiba sahihi yenye kutufikisha 50yrs later hatuna budi kuzingatia maoni ya wananchi.vinginevyo tunaweza kutengeneza katiba ya upande mmoja then baadae ikawa moto au shubili.
 
Back
Top Bottom