Tumeamini Katiba ni maridhiano

Tumeamini Katiba ni maridhiano

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,004
Wazanzibari wametutoa jasho. Wameshaharibu mianya ya kupata akidi. Punde,timu ya kimkakati tumetua Dodoma kutafuta maridhiano. Maridhiano ya kiakidi. Kuongea na wanahapana ili wajiunge na wanandiyo. Kanuni ziko kimya juu ya kurudia au la upigaji wa kura. Tunahitaji wanahapana wachache wahamie kwa wanandiyo.

Kura za siri nazo ni shubiri. Hapana zhmetamalaki. Napo panahitaji maridhiano. Ikibidi,tutatafuta maridhiano hata na wanaUKAWA kuokoa jahazi. Sasa kama chama tawala tumeamini kuwa Katiba ni jambo la maridhiano na si majivuno. Tusameheni.

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam (kwasasa Dodoma)
 
sasa wanaona umuhimu wa maridhiano badala ya ubavu na ubabe ambao umeshindwa kutimiza akidi
ccm ni chama cha mazuzu
 
Hahahahaha, kanuni zinakubali kura ZIRUDIWE kypigwa ili tu zipatikane za NDIYO au hata zile za NDIYO ziwe HAPANA?
Mzee Rusharusha tujuze
 
Wazanzibari wametutoa jasho. Wameshaharibu mianya ya kupata akidi. Punde,timu ya kimkakati tumetua Dodoma kutafuta maridhiano. Maridhiano ya kiakidi. Kuongea na wanahapana ili wajiunge na wanandiyo. Kanuni ziko kimya juu ya kurudia au la upigaji wa kura. Tunahitaji wanahapana wachache wahamie kwa wanandiyo.

Kura za siri nazo ni shubiri. Hapana zhmetamalaki. Napo panahitaji maridhiano. Ikibidi,tutatafuta maridhiano hata na wanaUKAWA kuokoa jahazi. Sasa kama chama tawala tumeamini kuwa Katiba ni jambo la maridhiano na si majivuno. Tusameheni.

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam (kwasasa Dodoma)
Mzee tupa tupa CCM waliamini hivyo... Ndio maana maridhiano yako kwenye kanuni za hilo hilo Bunge, sio kwamba wamejua leo...Labda wewe ndio umejua leo....

CCM though walijua makundi yenye kukwamisha Katiba ni Bara au Zanzibar....

UKAWA wangekuwa Bungeni pia wangepiga HAPANA na maridhiano yangehitajika tu, especially Kwa Zanzibar hiyo hiyo...

upuuzi wetu hatusemi document ndio zuri/baya... Tunazungumzia mambo mengine ya kijinga na ya kupita with time.
 
Tukisamehewa,hizo hela walizotuonya tusizichezee zitarudije?
Au tusamehewa kwa kukaidi na kufuja fedha kwa pamoja?
Kwenu,Watanzania.Sameheni jamani maana hujafa hujaumbika
 
Hakuna msamaha. Ni bora mchakachue kuondoa aibu/mfadhaiko
 
Wanaogopa kuchekwa! Sitta akitoka huko sujui atasali wapi maana amewaita maaskofu wapuuzi, maaskofu aliowasifu siku anaapa kuwa mwenyekiti wa bunge maalumu.
 
Tukisamehewa,hizo hela walizotuonya tusizichezee zitarudije?
Au tusamehewa kwa kukaidi na kufuja fedha kwa pamoja?
Kwenu,Watanzania.Sameheni jamani maana hujafa hujaumbika

Aibu watakayo ipata ya kukosekana kwa katiba inatosha kabsa kuwa adhab yao
 
Wazanzibari wametutoa jasho. Wameshaharibu mianya ya kupata akidi. Punde,timu ya kimkakati tumetua Dodoma kutafuta maridhiano. Maridhiano ya kiakidi. Kuongea na wanahapana ili wajiunge na wanandiyo. Kanuni ziko kimya juu ya kurudia au la upigaji wa kura. Tunahitaji wanahapana wachache wahamie kwa wanandiyo.

Kura za siri nazo ni shubiri. Hapana zhmetamalaki. Napo panahitaji maridhiano. Ikibidi,tutatafuta maridhiano hata na wanaUKAWA kuokoa jahazi. Sasa kama chama tawala tumeamini kuwa Katiba ni jambo la maridhiano na si majivuno. Tusameheni.

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam (kwasasa Dodoma)
Bora Mchawi kuliko mnafiki.
 
Wazee wa kitonga wajiandae kutafuta kwa jasho.. kuna mpambe nuksi hapo juu anakuambia acha unafiki.. na rasimu yao ya kufungia maandazi.. Rasimu ya Warioba ndio habari ya mujini.
 
Ili mradi ikifika tarehe nne mtoke huko na kuacha kufuja KODI zetu hayo makubaliano na kutafuta NDIYOOoooo tafuteni kwenye muda wenu wa ziada / wa bila malipo, au kwa email na FAX kama mlivyoshaamua
 
kuwasamehe kwa haya mliyotenda ni sawa na KUMKUFURU MUNGU , siwezi kukufuru endeleeni kuwafanyia unyama wananchi na kumtukana MZEE WARIOBA tuone mwisho wenu .
 
Hawa jamaa wanatakiwa watoe matokeo leo maana hakuna kanuni inayoruhusu RASIMU NZIMA kupigiwa kura mara mbili. Nimesoma KANUNI zinaruhusu Ibara (chache ) kura kupigwa kwa mara ya pili.
 
Wazanzibari wametutoa jasho. Wameshaharibu mianya ya kupata akidi. Punde,timu ya kimkakati tumetua Dodoma kutafuta maridhiano. Maridhiano ya kiakidi. Kuongea na wanahapana ili wajiunge na wanandiyo. Kanuni ziko kimya juu ya kurudia au la upigaji wa kura. Tunahitaji wanahapana wachache wahamie kwa wanandiyo.

Kura za siri nazo ni shubiri. Hapana zhmetamalaki. Napo panahitaji maridhiano. Ikibidi,tutatafuta maridhiano hata na wanaUKAWA kuokoa jahazi. Sasa kama chama tawala tumeamini kuwa Katiba ni jambo la maridhiano na si majivuno. Tusameheni.

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam (kwasasa Dodoma)

Mzer hata juzi nimeulizia hapa jf kwamba Mzee Tupa Tupa yuko wapi?Maana siku zote taarifa zako somehow verified tofauti na wanaccm wenzako kama Lizaboni,Chaburuma,Ritz,n,k.Wao ilimradi kila asubuhi watumiwe bundle toka Lumumba basi wanapost kila porojo ilimradi matumizi ya bundle yaonekane na buku 7 iandikiwe vocha.
 
Back
Top Bottom