Tume ya Utangazaji Zanzibar yazipa onyo kali Online TV zinazofanya kazi bila leseni

Tume ya Utangazaji Zanzibar yazipa onyo kali Online TV zinazofanya kazi bila leseni

Just Pray

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,142
Reaction score
4,779
Tume ya Utangazaji Zanzibar, katika utekelezaji wa kazi zake imebaini kuna vituo vya Utangazaji vya Maudhui ya Mtandaoni vinavyofanya kazi ya Utangazaji bila ya kuwa na leseni.

Kwa Mujibu wa kifungu cha 11 cha Sheria ya Tume ya Utangazaji Zanzibar, Sheria namba 7 ya mwaka 1997 "ni marufuku kwa mtu yeyote kuendesha huduma za Utangazaji bila ya kuwa na leseni inayotambulika".

Hivyo, Tume ya Utangazaji Zanzibar inawataka wamiliki na waendeshaji wa vituo vifuatavyo kufika katika Ofisi ya Tume ya Utangazaji Zanzibar ili kufanya usajili wa vituo vyao bila ya kukosa si zaidi ya tarehe 20/10/2025, vituo vyenyewe ni:-

BUSATI ONLINE TV
VUGA ONLINE TV
KASUSI ONLINE TV
TIFU ONLINE TV
DIGITAL ONLINE TV
LEADERS ONLINE TV
ZANZIBAR YETU
MAWENGI ONLINE TV
JIMBI ONLINE TV
MARHABA ONLINE TV
MU ONLINE TV

Tume ya Utangazaji Zanzibar, haitasita kuchukua hatua za kisheria kwa mtu yeyote anayeendesha Shughuli za Utangazaji Bila ya kuwa na Leseni.

Soma pia ZAMECO yalaani hatua za kudhibiti Vyombo vya Habari, yatetea Haki ya kupata Taarifa kipindi cha Uchaguzi
 
hapo ni mwendo wa kubanwa matokeo ya uchaguzi kusambazwa kabla hayajachakachuliwa
 
Back
Top Bottom