Ni aibu kubwa chama kikongwe kama CCM kutumia hoja muflisi kama inavyoshughudiwa katika kipindi cha kampeni za uchaguzi.
Imekuwa ni kawaida kwa Chama hiki kuibuka na hoja zenye lengo la kuzua hofu au kuchochea mgawanyiko kwa watanzania kwa nia ya kuhakikisha chama hiki kinaendelea kutawala Taifa hili kinavyotaka.
Kwa mfano:-
Mwaka 2000 CCM ilizusha hoja ya vita vya wenye kwa wenyewe kuzuka kama upinzani utapewa kuongoza nchi.
Mwaka 2010, Kwa kujua dhahiri kuwa upinzani utachukua nchi, wakaja na hoja ya udini hasa ukatoliki ili kuchafua taswira ya mgombea wa wakati huo Dr, Slaa na Chama chake CHADEMA, dhidi ya wasiokuwa wakristo na pia dhidi ya wasiokuwa wakatoliki.
Mwaka huu 2015, ambapo hatari ya CCM kupumzishwa imekuwa kubwa zaidi, Waimeibuka na hoja nyingine TATU,
KWANZA, Wameibua tena udini na hasa ULUTHERI kwakua tu mgombea wa upinzani ni Mkristo (MLUTHERI);
PILI, Wamekuja na hoja ya Ukanda, kwa maana ya atokako mgombea wa upinzani, hoja ya ukaskazini.
TATU, nimeshughudia hapa Tanga leo, ambapo tokea asubuhi wanazunguka kuwaomba watu wahudhurie mkutano wa magufuli hapo kesho, wakiwatangazia wananchi kuwa CHADEMA ni FREE MASONS.
Kwa vyovyote vile pamoja na kwamba uelewa na mwamko wa wananchi wengi umekua sana hasa katika uchaguzi huu, bado sio vyema kauli hili hizi zikaachwa bila kukemewa kwani hata cheche moja huweza kuzua moto mkubwa sana ukamaliza pori.
Ni vema Tume ya Uchaguzi, kama mwamuzi wa mtanange huu, ikakemea siasa za kibaguzi kama hizi za CCM.
Hii ni bila kusahau kauli tata za CCM hii kuwa watashinda "HATA KWA BAO LA MKONO" na pia hawako tayari kumpisha mtu ikulu kwa "USHINDI VYA VIKARATASI".