GE2025 Tume ya Uchaguzi (INEC) inazungumza na Wazalishaji wa Maudhui ya Mitandaoni, leo Agosti 3, 2025

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
4,783
Reaction score
14,975
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) inaendelea na mchakato wa maandalizi kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 2025.

Tume imekuwa ikifanya vikao vya Wadau mbalimbali, leo Agosti 3, 2025 kikao kinafanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuwajengea uwezo zaidi ili kutimiza majukumu yao kwa ufanisi wakati wa uchaguzi mkuu 2025.

Your browser is not able to display this video.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele amewataka watengeneza maudhui ya Mtandaoni kuwa makini na matumizi ya Akili Unde (Artificial Intelligence (AI) wakati wa Uchaguzi Mkuu 2025 kwa kuwa yakitumika vibaya yanaweza kuwa na madhara katika ufikishaji ujumbe kwa Jamii.

Ameyasema hayo wakati wa kikao cha INEC na Wadau hao leo Agosti 3, 2025 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City kwa ajili ya kuwajengea uwezo zaidi ili kutimiza majukumu yao kwa ufanisi wakati wa mchakato huo.


Jaji Mwambegele: Hatujui kama kuna Watu waliokufa kwenye Daftari la Wapiga Kura
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele:

Daftari la Wapiga Kura ni la Kudumu, lipo na litaendelea kuwepo, linaboreshwa kila baada ya miaka mitano kwa kuongeza wale ambao hawakuwa wametimiza vigezo pamoja na kuondoa ambao hawakustahili kuwemo.

Daftari la Wapiga Kura lina Watu waliokufa, hilo sisi hatujui, tunategemea kupewa taarifa, mchakato wa utoaji taarifa unahusisha kujaza fomu ili kuonesha huyu amefariki, hivyo aondolewe kwenye Daftari.

Inawezekana kweli wapo Watu waliofariki na majina yao bado yapo kwenye Daftari la Wapiga Kura kwa kuwa hatuna taarifa zao.

Sisi (INEC) Hatujaandikisha Watu milioni 37 wakati huu, tumeandikisha Wapiga Kura wapya takribani Milioni 8, tumeongezea wale waliokuwepo awali amba oni Milioni 29.

Inawezekana wapo watu waliofariki wapo kwenye daftari hatuwezi kumuondoa mtu kama hatua taarifa zao, tunaomba kwa yeyote anayejua atusaidie kubaini Watu waliofariki kwa kufuata mchakato wa kujaza fomu kisha tutawaondoa, itasaidia kuweka namba sawa.

Lakini uhalisia ni kuwa hakuna Mtu ambaye amefariki anaweza kuja kupiga kura, tusaidieni kutoa hizo taarifa.
 
Ndio wanakuja kuzuia ambao hawakusoma

USSR
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…