Tume ya Uchaguzi imevamiwa?

Tume ya Uchaguzi imevamiwa?

klaymoo

Member
Joined
Oct 3, 2018
Posts
7
Reaction score
19
Unaweza kusema hivyo kwa kuwa hadi leo hakuna anayefahamu sababu za mkurugenzi mkuu wa tume hiyo ya uchaguzi Dkt Athumani Kihamia kupewa cheo hicho akitokea Jiji la Arusha ambako alifanya vurugu nyingi sana na kupelekea kuundwa tume ya kumchunguza na alikuwa anafanya kazi za siasa zaidi kuliko za utendaji huku akimjeruhi kila mtumishi wa jiji aliyepinga falsafa zake tata huku akiungwa mkono na RC Gambo na DC Dakaro na Catherine Magige mbunge wa viti maalum.

Tunasema tume imevamiwa kwa kuwa falsafa za Dkt Kihamia ni ngumu kutekelezeka katika utawala wa sheria kwa kuwa anachoamini yeye ndicho kitakachotekelezwa na atakayempinga atakuwa adui na atashughulikiwa tena hadharani na ndiyo maana baadhi ya vikao vya kamati na baraza la madiwani vilitawaliwa na vurugu za aibu na hata wakati mwingine watu kupigana ngumi mbele ya wananchi na wakati mwingine kuvunjika vikao hivyo. Jiji hilo lilikuwa likiendeshwa kama kikosi cha jeshi yaani amri zilikuwa nyingi kuliko utawala wa sheria.

Viongozi wa namna hii hawafai kuwa watendaji wakuu, huyu ni mwanasiasa kiasili tena wale wenye roho ngumu. Ushahidi wa hili ni kesi inayomkabili hadi leo kule Arusha akihusishwa kupanga na kutekeleza mkakati na kufanikiwa kumteka Mwalimu Batuli Hamadi Kisaya wa shule ya msingi Unga limited iliyopo jijini Arusha mnamo septemba 2016 akishirikiana na mbunge Catherine Magige na Mrisho Gambo RC Arusha, kesi ambayo bado inaendelea, sababu za mwalimu huyo kutekwa, kuteswa na kutupwa porini kabla ya kuokotwa na wasamaria wema na kupelekwa hospitali ya rufaa ya mount meru na kulazwa wiki 2 ambapo alisema alitekwa maeneo ya nyumbani kwake akitokea dukani kwa kutishiwa kwa bunduki na vijana 6 ambao inasemekana ni wafuasi wa UVCCM.

Mwl Batuli alikuwa akimlalamikia mkurugenzi huyo kwa kumvua madaraka ya uratibu elimu kata bila sababu za msingi. Mkurugenzi huyu aliwakomoa watendaji wa kata na vijiji wengi kwa kuwahamishia maeneo yenye mazingira magumu na kuna wakati baadhi ya watumishi waliamua kuacha kazi wakiwemo wanasheria 4 maafisa utumishi 2 wahasibu 3 maafisa manunuzi 4 na kusitisha ajira halali 66 za watumishi wa mikataba na kufuta ajira 22 za mgambo wote wa jiji huku akiwashitaki mahakamani madiwani 2 kwa tuhuma ambazo hazina mashiko na akamsweka ndani naibu meya kwa siku moja baada ya kulumbana kwenye kikao ambapo polisi hawakuona kosa la naibu meya huyo.

Kitendo cha utekaji ni kibaya sana ambacho hakiashirii mema hata huko TUME wajiandae kufanyiwa ubabe, vurugu na hata kutekwa hasa akibishiwa sera zake zenye utata.

Naamini Mhe. rais hamjui vizuri huyu mtekaji angemjua asingemteua.

TUKEMEE HALI HII
IMG_20181012_151248_679.jpeg
 
Cha msingi kinachoangaliwa ni kumfurahisha yule tu aliyemteua.

Hayo mengine yanabaki theory tu. Hayawezi kuonekana kwa nchi hii kwa sasa.
 
Fitna inaendelea yani mti wenye matunda lazima watu waupopoe tu. Piga kazi Dkt. Kihamia achana na hao ntimanyongo
 
Sasa imekuwa too much yani mpaka utekaji anahusika? Ila mbona hakuna sehemu alipotiwa hatiani? hapa sio mahakamani kama una hoja yenye mashiko peleka mahakamani
 
Ukimuona mtu anatumia muda mwingi kumjadili kiongozi fulani anayechapa kazi kwa uaminifu kwa manufaa ya Taifa ujue ana matatizo na anahitaji kuombewa! Mtoa post unapoteza muda wako bure tumia muda wako kufanya kazi acha umbeya na zaidi ya hayo

1. Unamuogopa
2. Maslahi yako maovu yameguswa
3. Uwezo wako wa kufikiri mtu umefikia ukingoni
4. Umbeya umekutawala akili yako yote
5. Unatumika tu na muda ukiisha Unafyekelewa mbali
 
Mtoa post unaweweseka aisee! Pia unadharau hata kwa Rais kwamba hamjui vizuri mtu aliyemteua unatafuta kick na huruma! Wewe ni sikio la kufa kafie mbaliiiii
 
Cjaelewa mkuu, ina maana huyu ni MTU asiejulikana
Huyu anajulikana sema tu anawakanyagia waya wale wezi, wavivu, mafisadi na watu wa konakona wasiopenda kunyoosha mstari. Nasikia alikuwa anawanyoosha kwa rula huko Arusha. Mtu bingwa sana huyu Dkt. Kihamia. Chadema Arusha waligeuza kama shamba la bibi.
 
Tulieni moto unawafikia taratibu mafisadi nyie!
We Mwajuma ndala mbili na huku umo?
Nyïe mmekula wapinzani sasa mnaanzana wenyewe,hakuna tone la damu litalomwagika bure,litali na nyie na anayewatuma mpaka kizazi cha nne
 
yani mtu alïyeleta vurugu Arusha,mtekaji,anayependelea chama Tawala ndio unampa NEC?

Alafu mkiambiwa mna kisonono na Gonorhea mnalia lia hapa

Wewe huijui Arusha ndio maana unapiga kelele, nenda kamuulize Lema ana majibu mazuri kuliko huu upuuzi wako unaoandika!
Arusha will never back kwenye siasa za kihuni chini ya wahujumu uchumi kama wewe!
 
We Mwajuma ndala mbili na huku umo?
Nyïe mmekula wapinzani sasa mnaanzana wenyewe,hakuna tone la damu litalomwagika bure,litali na nyie na anayewatuma mpaka kizazi cha nne
Nchi hii ina amani mpaka kizazi cha nne plus plus, yani milele. Ila wenye roho mbaya kama wewe ndio hamtapata amani mpaka kizazi cha nne.
 
Unaweza kusema hivyo kwa kuwa hadi leo hakuna anayefahamu sababu za mkurugenzi mkuu wa tume hiyo ya uchaguzi Dkt Athumani Kihamia kupewa cheo hicho akitokea Jiji la Arusha ambako alifanya vurugu nyingi sana na kupelekea kuundwa tume ya kumchunguza na alikuwa anafanya kazi za siasa zaidi kuliko za utendaji huku akimjeruhi kila mtumishi wa jiji aliyepinga falsafa zake tata huku akiungwa mkono na RC Gambo na DC Dakaro na Catherine Magige mbunge wa viti maalum.

Tunasema tume imevamiwa kwa kuwa falsafa za Dkt Kihamia ni ngumu kutekelezeka katika utawala wa sheria kwa kuwa anachoamini yeye ndicho kitakachotekelezwa na atakayempinga atakuwa adui na atashughulikiwa tena hadharani na ndiyo maana baadhi ya vikao vya kamati na baraza la madiwani vilitawaliwa na vurugu za aibu na hata wakati mwingine watu kupigana ngumi mbele ya wananchi na wakati mwingine kuvunjika vikao hivyo. Jiji hilo lilikuwa likiendeshwa kama kikosi cha jeshi yaani amri zilikuwa nyingi kuliko utawala wa sheria.

Viongozi wa namna hii hawafai kuwa watendaji wakuu, huyu ni mwanasiasa kiasili tena wale wenye roho ngumu. Ushahidi wa hili ni kesi inayomkabili hadi leo kule Arusha akihusishwa kupanga na kutekeleza mkakati na kufanikiwa kumteka Mwalimu Batuli Hamadi Kisaya wa shule ya msingi Unga limited iliyopo jijini Arusha mnamo septemba 2016 akishirikiana na mbunge Catherine Magige na Mrisho Gambo RC Arusha, kesi ambayo bado inaendelea, sababu za mwalimu huyo kutekwa, kuteswa na kutupwa porini kabla ya kuokotwa na wasamaria wema na kupelekwa hospitali ya rufaa ya mount meru na kulazwa wiki 2 ambapo alisema alitekwa maeneo ya nyumbani kwake akitokea dukani kwa kutishiwa kwa bunduki na vijana 6 ambao inasemekana ni wafuasi wa UVCCM.

Mwl Batuli alikuwa akimlalamikia mkurugenzi huyo kwa kumvua madaraka ya uratibu elimu kata bila sababu za msingi. Mkurugenzi huyu aliwakomoa watendaji wa kata na vijiji wengi kwa kuwahamishia maeneo yenye mazingira magumu na kuna wakati baadhi ya watumishi waliamua kuacha kazi wakiwemo wanasheria 4 maafisa utumishi 2 wahasibu 3 maafisa manunuzi 4 na kusitisha ajira halali 66 za watumishi wa mikataba na kufuta ajira 22 za mgambo wote wa jiji huku akiwashitaki mahakamani madiwani 2 kwa tuhuma ambazo hazina mashiko na akamsweka ndani naibu meya kwa siku moja baada ya kulumbana kwenye kikao ambapo polisi hawakuona kosa la naibu meya huyo.

Kitendo cha utekaji ni kibaya sana ambacho hakiashirii mema hata huko TUME wajiandae kufanyiwa ubabe, vurugu na hata kutekwa hasa akibishiwa sera zake zenye utata.

Naamini Mhe. rais hamjui vizuri huyu mtekaji angemjua asingemteua.

TUKEMEE HALI HII
View attachment 901688
Viongozi wanaotakiwa sasa ni wale wanaoweza kuubomoa upinzani bila soni.
 
Back
Top Bottom