PreGE2025 Tume ya Taifa ya Uchaguzi yatangaza awamu ya pili ya kuandikisha wapigakura kuanza Mei Mosi mwaka huu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
2,439
Reaction score
6,691
Wakuu,

Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura awamu ya pili utafanyika sambamba na uwekaji wazi wa Daftari la Awali la Wapiga Kura kuanzia tarehe 01 Mei, 2025 na kukamilika tarehe 04 Julai, 2025.

Akizungumza jijini Dodoma leo tarehe 14 Aprili, 2025 Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Rufani, Mhe. Jacobs Mwambegele amesema zoezi la uboreshaji wa Daftari litafanyika kwa mizunguko mitatu ambapo mzunguko wa kwanza utajumuisha mikoa 15, mzunguko wa pili mikao 16 na mzunguko wa tatu utajumuisha vituo vya magereza na vyuo vya mafunzo.

Ameitaja mikoa itakayohusika kwenye mzunguko wa kwanza wa uboreshaji kuwa ni pamoja na Geita, Kagera, Mara, Shinyanga, Mwanza, Simiyu, Rukwa, Tabora, Katavi, Kigoma, Iringa, Ruvuma, Mbeya, Njombe na Songwe ambapo zoezi hilo litafanyika tarehe 01 hadi 07 Mei, 2025.

Soma pia: Uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura Dar es Salaam Kufanyika Machi 17-23, 2025. Wapiga Kura wapya 643,420 kuandishwa

Mikoa ya mzunguko wa pili ni pamoja na Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Tanga, Morogoro, Pwani, Singida, Dodoma, Dar es Salaam, Lindi, Mtwara, Mjini Magharibi, Kaskazini Unguja, Kusini Unguja, Kaskazini Pemba na Kusini Pemba ambapo zoezi hilo litafanyika tarehe 16 hadi 22 Mei, 2025.

“Mzunguko wa tatu wa zoezi la uboreshaji wa Daftari utahusisha vituo 130 vilivyopo kwenye magereza ya Tanzania Bara na vituo 10 vilivyopo katika Vyuo vya Mafunzo Tanzania Zanzibar kwa wakati mmoja na utafanyika kwa muda wa siku saba kuanzia tarehe 28 Juni, 2025 hadi tarehe 04 Julai, 2025,” amesema Jaji Mwambegele.

Ameongeza kuwa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa awamu ya pili, utafanyika ngazi ya kata kwa Tanzania Bara na ngazi ya jimbo kwa Tanzania Zanzibar, ambapo jumla ya vituo 7,869 vitahusika, vituo 7,659 vipo Tanzania Bara na vituo 210 vipo Tanzania Zanzibar.

“Tunatarajia kuwa katika awamu ya pili ya uboreshaji, wapiga kura wapya 1,396,609 wataandikishwa, wapiga kura 1,092,383 wataboresha taarifa zao na wapiga kura 148,624 watafutwa kwenye Daftari kwa kukosa sifa za kuendelea kuwepo kwenye Daftari,” amesema Jaji Mwambegele.
 
Kuna sababu gani ya mimi mpiga kura kujiandikisha kupiga kura, halafu mwisho wa siku kura yangu haiheshimiwi? Yaani anayeamua nani ashinde ni msimamizi wa uchaguzi, akishirikiana na polisi! badala ya mimi mpiga kura!

Sasa si bora kupotezea tu! Au na huu nao ni UHAINI!!
 
Sio lazima wewe ukajiandikishe, wapo wenye uhitaji wa kujiandikisha
 
  • Nzuri
Reactions: Tui
Wakuu,

Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura awamu ya pili utafanyika sambamba na uwekaji wazi wa Daftari la Awali la Wapiga Kura kuanzia tarehe 01 Mei, 2025 na kukamilika tarehe 04 Julai, 2025.

Akizungumza jijini Dodoma leo tarehe 14 Aprili, 2025 Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Rufani, Mhe. Jacobs Mwambegele amesema zoezi la uboreshaji wa Daftari litafanyika kwa mizunguko mitatu ambapo mzunguko wa kwanza utajumuisha mikoa 15, mzunguko wa pili mikao 16 na mzunguko wa tatu utajumuisha vituo vya magereza na vyuo vya mafunzo.

Ameitaja mikoa itakayohusika kwenye mzunguko wa kwanza wa uboreshaji kuwa ni pamoja na Geita, Kagera, Mara, Shinyanga, Mwanza, Simiyu, Rukwa, Tabora, Katavi, Kigoma, Iringa, Ruvuma, Mbeya, Njombe na Songwe ambapo zoezi hilo litafanyika tarehe 01 hadi 07 Mei, 2025.

Soma pia: Uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura Dar es Salaam Kufanyika Machi 17-23, 2025. Wapiga Kura wapya 643,420 kuandishwa

Mikoa ya mzunguko wa pili ni pamoja na Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Tanga, Morogoro, Pwani, Singida, Dodoma, Dar es Salaam, Lindi, Mtwara, Mjini Magharibi, Kaskazini Unguja, Kusini Unguja, Kaskazini Pemba na Kusini Pemba ambapo zoezi hilo litafanyika tarehe 16 hadi 22 Mei, 2025.

“Mzunguko wa tatu wa zoezi la uboreshaji wa Daftari utahusisha vituo 130 vilivyopo kwenye magereza ya Tanzania Bara na vituo 10 vilivyopo katika Vyuo vya Mafunzo Tanzania Zanzibar kwa wakati mmoja na utafanyika kwa muda wa siku saba kuanzia tarehe 28 Juni, 2025 hadi tarehe 04 Julai, 2025,” amesema Jaji Mwambegele.

Ameongeza kuwa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa awamu ya pili, utafanyika ngazi ya kata kwa Tanzania Bara na ngazi ya jimbo kwa Tanzania Zanzibar, ambapo jumla ya vituo 7,869 vitahusika, vituo 7,659 vipo Tanzania Bara na vituo 210 vipo Tanzania Zanzibar.

“Tunatarajia kuwa katika awamu ya pili ya uboreshaji, wapiga kura wapya 1,396,609 wataandikishwa, wapiga kura 1,092,383 wataboresha taarifa zao na wapiga kura 148,624 watafutwa kwenye Daftari kwa kukosa sifa za kuendelea kuwepo kwenye Daftari,” amesema Jaji Mwambegele.
NO REFORM NO ELECTION

AND THEREFORE MIZUNGUKO HIYO HAINIHUSU
 
No reforms no election nimejiandikisha ila msipo jua umuhimu wa maamuzi yetu basi sipigi kura
 
Wananchi walio KOSA vitambulisho watajiandikisha...
 
Back
Top Bottom