Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) yawateua 8 kuwa Wabunge wa Viti Maalum CUF

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
Kwa mujibu wa Ibara ya 78(4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ikisomwa pamoja na kifungu cha 86(8) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, sura ya 343, Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika kikao chake cha tarehe 27 Julai 2017imewateua wafuatao kuwa Wabunge wa Viti Maalum katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Wananchi (CUF).

1- Ndugu Rukia Ahmed Kassim;
2- Ndugu Shamsia Aziz Mtamba;
3- Ndugu Kiza Hussein Mayeye;
4- Ndugu Zainab Mndolwa Amir;
5- Ndugu Hindu Hamis Mwenda;
6- Ndugu Sonia Juma Magogo;
7- Ndugu Alfredina Apolinary Kahigi; na
8- Ndugu Nuru Awadh Bafadhili,

Uteuzi huu umefanyika baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye kwa mujibu wa Kifungu cha 37(3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 alitaarifu Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwepo kwa nafasi waza nane (8) za Wabunge wa Viti Maalum kupitia Chama cha Wananchi CUF.

IMG_20170727_152042.jpg

IMG_20170727_162349.png

 
CDM Walimvua Zitto Uanachama Lakini Alibaki Na Ubunge Zaidi Ya Mwaka, Kwanini Hawa Wa CUF Spika Karidhia Harakaharaka hivi? Kuna Nini?

Sielewi dhumuni la spika utafikiri walipanga haya mambo
Naona kama vile kuna "Quoram" maalumu (2/3) inatafutwa bungeni kwa ajili ya kupitisha jambo muhimu maana kikao kiliandaliwa lini wakati spika ni jana tuu katamka?
 
Back
Top Bottom