Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,158
- 25,406
Binafsi, jana tarehe 12/10/2019, nimejiandikisha kwenye Orodha ya Wapigakura wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika mwezi ujao nchi mzima. Niliamua kujiandikisha kabla hata ya uhamasishaji nilioushuhudia ukifanywa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, viongozi wa CCM na wale wa CHADEMA Kibaha Mjini.
Nilifika kwenye Kituo cha Uandikishaji kwenye Ofisi za Serikali ya Mtaa ya Visiga A, Kata ya Visiga, Kibaha Pwani kwa ajili ya kujiandikisha. Nimejiandikisha kwakuwa naamininkatika demokrasia na hali zangu kama raia wa Tanzania ikiwemo hali ya kuchagua na kuchaguliwa kwenye chaguzi zinazoratibiwa na NEC.
Kituoni nilipofika kulikuwa na wahusika wawili. Mmoja alijitambulisha kwetu kama ndiye Mwandikishaji na mwingine ni Wakala, bila kuweka wazi ni Wakala wa chama au taasisi gani hasa. Tulikuwa watu watatu kwa jumla tuliohitaji kujiandikisha, wawili wakiwa wamenitangulia kwenye mstari.
Kwa nilichokishuhudia kwenye uandikishaji, uandikishaji huo una kasoro za wazi, unatia mashaka na nawaasa TAMISEMI kufanya marekebisho kwenye zoezi hilo. Waandikishwaji wanataja majina yao matatu kwa ajili ya kuandikishwa na umri wao kabla ya kutia saini zao pasipo ushahidi wowote wa mambo hayo.
Hawatakiwi kuonyesha kitambulisho chochote kuhusu majina au umri wao. Hili linawezekanaje? Udanganyifu wa majina na umri ni mkubwa mno.
Inashindikanaje kwa waliojiandikisha kurudi tena na majina na umri mwingine? Kwa uwezekano huo, naliona zoezi hilo lilivyo na kasoro na kutia mashaka.
TAMISEMI MNA jambo la kufanya katika hili ili kuhakikisha kuwa uchaguzi ujao unakuwa huru na haki. Kwa uandikishaji ulivyo, kuna kila dalili za uandikishaji batili. Nineongea nanyi TAMISEMI kwa nia njema kabisa.