Tume ya Taifa ya Uchaguzi kutumia Sh. Bilioni 1 ktk Uchaguzi wa Marudio Kinondoni

Nasikia kuwa sh. 1 billion itatumika kugharamia uchaguzi wa kumrudisha tena Mtulia kwenye ubunge Kinondoni. Watanzania wangefanya mangapi kwa sh. 1bil zao?
 
Dawa ni kuhakikisha mna mpigia kura za kutosha katika kuchagua mgombea mnaye mtaka.

Ili akitangazwa tofauti na mliye mpigia kura zote za ndiyo basi mjue kuwa tume huru ndiyo suluhisho hapo 2020.
 
Akichaguliwa tena huyu nadhani kinondoni iitwe shithole na sio kinondoni..haiwezekan mtu mlimchagua kwa mapnz Yale anajiuzulu then agombe tena na mmpe tena..billion 1 ingetumika kujenga barabara za mtaa hapo kinondoni, zingepatikana km zaidi ya 20 za Lami...
 
Unajua hizi figure mnavyozitaja muwe serious kidogo,mtu mmoja anafanya ufisadi kama huu alafu bado mnatuaminisha fisadi ni lowasa,huyu mtulia laana yake sio ndogo
 
Sehemu kubwa ya hiyo hela haitapotea. Itaingia mikononi mwa walipa kodi wa nchi hii na kuzalisha pesa zaidi. Hii ni njia mojawapo ya kuingiza pesa mwenye mzunguko ambazo kuna watu walisema zimepotea
Ndugu uelewe unaweza kuingiza kwa kujenga dispensary
 
Hivi ndivyo tunavyokichangia chama watanzania woote bila kujitambua.
Mara EPA, mara Escrow, yoote michango ya ya kisirisiri. Hakuna sababu za kutosha kuamini mpango na matumizi kama haya
 
Nimeshindwa kabisa kuvielewa vyama vya siasa na hata Magufuli. Kitendo cha chama cha siasa kuwakumbatia wabunge wanaosema wanahama vyama vyao ili kumuunga mkono Magufuli, na kukubali kuwarudisha hao watu wakagombee kwenye hayo majimbo tena, ni kinyume kabisa na kauli ya serikali na Magufuli kwamba tuko katika kubana matumizi ya serikali.

Serikali na hata Magufuli walipaswa kukemea ufujaji huu wa fedha ambao ni gharama kubwa sana ya kumuunga mkono raisi. Kama hawa wabunge wana moto wa kumuunga mkono Magufuli basi wajitolee kutoa fedha za kuendesha uchaguzi mpya kwenye majimbo yao!

Je, kimya cha Magufuli juu ya jambo hili ina maana anafurahia kitendo cha wabunge wanaojiuzuru ubunge ili kumuunga mkono kwa gharama ya serikali ya zaidi ya Tshs bilioni moja?

Kumbuka kwamba Tshs bilioni moja ndio kadirio la gharama ya chini ya kurudia uchaguzi.

Hili ni jambo si tu linapaswa kukemewa, bali pia kutafutiwa suluhisho ambalo halitaitia serikali hasara kwa ubinafsi wa baadhi ya watu kufuja fedha za serikali kwa kisingizio cha kumuunga mkono magufuli.

upload_2018-1-25_10-25-3.png
 
Achana na siasa, kujizatiti na ku weaken opposition ni kipaumbele kwa wanasiasa kuliko kero za wananchi, hata ulalamike kivipi hawatakuelewa, uhakika wa madaraka kwanza, wewe raia baadaye..
 
Siri kali hii inaweza kuwa na ufisadi wa kutisha kuliko inavyo jitanabaisha.
 
Back
Top Bottom