Mzalendo2015
JF-Expert Member
- Aug 14, 2012
- 6,697
- 9,048
Kwa heshima na taadhima niwaombe Tume ya Taifa(NEC)watoe tangazo rasmi la kuzuia kuhamahama vyama bila utaratibu kuanzia leo. Kwamba iwe ni marufuku kwa mtu yeyote aliyechaguliwa kwa kura kuwa Mbunge au Diwani (kwa kupigiwa kura au kuteuliwa)kuhama chama kwasababu za kishabiki tu!!!Hii ni kwasababu kama NEC wataendelea kuruhusu Wabunge na Madiwani kuhama hama bila utaratibu kunalisabishia Taifa kuingia gharama za mamilioni/Mabilioni kurudia chaguzi kwenye majimbo na kata husika!!!
NEC waweke wazi na kuwe na sheria rasmi ya kwamba Uchaguzi utarudiwa tu pale Mbunge au Diwani anapojiuzulu kwasababu za Kiafya/Ugonjwa, Mbunge anapofariki au kubatilisha Uraia wa Tanzania. Kuanzia sasa iwe ni marufuku kujiuzulu na kuhama chama ukiwa Mbunge au Diwani kwani watu walipochagua walichagua sera za Chama na siyo mtu. Madai ya kuwa Diwani au Mbunge anahama chama ati kufuata Utawala ambao yeye haukumpa Ubunge au Udiwani ni ulimbukeni.
Kama NEC watanyamzia hili jambo nchi itajikuta inaingia kwenye gharama mpya za marudio ya Uchaguzi. Nitakuwa tayari kuwaunga mkono NEC iwapo wataweka wazi kuwa pale Mbunge au Diwani anapojiuzulu basi yule aliyekuwa mshindi wa PILI kwenye Uchaguzi Mkuu apewe hiyo nafasi ya Ubunge au Udiwani. Hii itasaidia kuepusha gharama za kipuuzi na zisizo za lazima. Wale wote wanaojiuzulu wasiruhusiwe kugombea nafasi za Ubunge au Udiwani mpaka Uchaguzi Mkuu mwingine unaofuata na si vinginevo.
Naomba kuwasilisha.